Kibaki amerudi Ikulu

yaani hii inaonyesha kibaki amecheza dirty game,mtu akishinda kihalali utaalika marafiki, ndugu na jamaa usherekee nao! sasa kibaki hataki kuita rafiki na majirani kwanini? hata angeita hata mafisadi wezake ingekuwa disguise nzuri! afrika moto
 
Quote:-

"We dont have to time ya Ku-analyze ikiwa Uchaguzi hakuwa Fair..."

Kwenye kila uchaguzi kuna two sides, ya academic na ya malalamiko ya kufanyika kwa uhuni, kama vile uchaguzi wa US mwaka 2000,

Gore, alitaka kura za baadhi ya majimbo ya uchaguzi ambayo alikuwa akijua wazi kuwa hayo majimbo ni ya Democrat kule Florida, yarudiwe kuhesabiwa kura, huku akijua wazi kuwa sheria za US zinasema wazi kama ni kurudiwa kwa kura, basi ni kura zote za State of Florida zilitakiwa zirudiwe kuhesabiwa, alijua kuwa zikihesabiwa zote za State, hatashinda, ingawa haibadilishi ukweli kuwa kuna mchezo mchafu ulichezwa na political system nzima ya State of Florida, ambayo ilikuwa ni Republican,

Ukiangalia Kenya, ni kwamba political system nzima ya huko ni Kikuyus, je kweli wangeweza kumpitisha Odinga? Sawa kuna mchezo mchafu umefanyika, lakini pia kuna makosa yaliyofanywa na ODM kwa kuelewa wazi kabla hata ya kuanza uchaguzi kuwa haitakuwa rahisi kushinda system ya nchi yao ambayo ni dominated na the Kikuyus, kwa chama cha Kikuyus, kwa kweli kuna mengi ya kujifunza academically, ingawa pia huwezi kuangalia mchezo mchafu uliochezwa pia!
 
Kibak..(nashawishika kumalizia na "a") ataongoza tu kama anavyofanya Mugabe, na nafuu aliyo nayo ni kwamba wazungu hawajatangaza kumtenga, kwa hiyo ataendelea kula vya "kunyonga". Kumbuka hii ilikuwa coalition ya mafisadi dhidi ya demokrasia, kwa hiyo haishangazi wametumia mbinu za kifisadi pia. Wapo wengi sana wanaolinda interest zao hapo nyuma ya mgongo wa huyo babu, sidhani kama yeye binafsi anafaidika chochote na huu urais wa uzeeni. Ndivyo ilivyokuwa kwa H.E Ngwazi Dr Hastings Kamuzu Banda, na ndivyo ilivyo pia kwa "Jongwe" Comrade Robert Gabriel Mugabe!
 
nakuambia,

sio tu kuwa inachekesha ila inasitisha kufurahia uafrika. Kazi kweli iko mbele yetu.

Hapana tena wacha kujidharaulisha ,maendeleo katika kasi na dira mpya hayakuanza hapa Afrika,hivi mlisahau kama ukoo wa George Bush uliiba kura na kumwangusha Dole au wale weupe wanayoyafanya ni sawa au ni ya wazungu kama maepol.
Tuombe mapambano yapite mbali nakumbuka vita ya maumau kule kenya si watu wa amani kama hapa Tanzania,huko mambo yakichafuka basi wanaweza hata kujigawa na kukatika mapande mawili.Na suluhisho lake ni vita ya weyewe kwa wenyewe ,yaani ni kama ile hadithi ya Nyoka yupo mwanza alafu wengine wanaitikia na apite..Nyoka huyu alikuwepo Zaire,Burundi Rwanda Somalia ,huku tunaitikia na apite ,sasa jamani Nyoka anaikaribia kenya ?
 
Quote:-

"We dont have to time ya Ku-analyze ikiwa Uchaguzi hakuwa Fair..."

Kwenye kila uchaguzi kuna two sides, ya academic na ya malalamiko ya kufanyika kwa uhuni, kama vile uchaguzi wa US mwaka 2000,

Gore, alitaka kura za baadhi ya majimbo ya uchaguzi ambayo alikuwa akijua wazi kuwa hayo majimbo ni ya Democrat kule Florida, yarudiwe kuhesabiwa kura, huku akijua wazi kuwa sheria za US zinasema wazi kama ni kurudiwa kwa kura, basi ni kura zote za State of Florida zilitakiwa zirudiwe kuhesabiwa, alijua kuwa zikihesabiwa zote za State, hatashinda, ingawa haibadilishi ukweli kuwa kuna mchezo mchafu ulichezwa na political system nzima ya State of Florida, ambayo ilikuwa ni Republican,

Ukiangalia Kenya, ni kwamba political system nzima ya huko ni Kikuyus, je kweli wangeweza kumpitisha Odinga? Sawa kuna mchezo mchafu umefanyika, lakini pia kuna makosa yaliyofanywa na ODM kwa kuelewa wazi kabla hata ya kuanza uchaguzi kuwa haitakuwa rahisi kushinda system ya nchi yao ambayo ni dominated na the Kikuyus, kwa chama cha Kikuyus, kwa kweli kuna mengi ya kujifunza academically, ingawa pia huwezi kuangalia mchezo mchafu uliochezwa pia!

FMES,

Haya masuala ya Afrika hayajali political system gani inatumika, ni mambo ya cronyism. Wale ambao wanaishi kwa neema ya system iliyopo madarakani, hawataki kuondoka na wanatumia kila mbinu kubaki madarakani. Tumeyaona Zanzibar, Zimbabwe na hata Zambia ambako Kaunda alikataa alipofuatwa na tume ya uchaguzi kwamba wabadili matokeo.

Nafikiri ifike mahali vijana wa Afrika tukatae huu ujinga hata kama tunafaidika nao.

Labda imefika wakati kwa baadhi ya hawa viongozi kuwekwa vitanzi kama yule wa Romania kama tishio kwa wengine wote.

Inasikitisha sana kwenye system kuna mijitu mingi mibovu mno, wanashindwa hata mambo ya kawaida ya kuendesha nchi, hao hao ndio wa kwanza kupamba ujinga, uwizi ili wabaki kula pesa za wananchi, huku wananchi wenyewe wanazidi kuwa maskini.

Hizo ni nchi zetu wote, kama kuwaondoa kwa demokrasia imeshindikana, kuna siku wataondoka kwa nguvu.
 
Hapana tena wacha kujidharaulisha ,maendeleo katika kasi na dira mpya hayakuanza hapa Afrika,hivi mlisahau kama ukoo wa George Bush uliiba kura na kumwangusha Dole au wale weupe wanayoyafanya ni sawa au ni ya wazungu kama maepol.
Tuombe mapambano yapite mbali nakumbuka vita ya maumau kule kenya si watu wa amani kama hapa Tanzania,huko mambo yakichafuka basi wanaweza hata kujigawa na kukatika mapande mawili.Na suluhisho lake ni vita ya weyewe kwa wenyewe ,yaani ni kama ile hadithi ya Nyoka yupo mwanza alafu wengine wanaitikia na apite..Nyoka huyu alikuwepo Zaire,Burundi Rwanda Somalia ,huku tunaitikia na apite ,sasa jamani Nyoka anaikaribia kenya ?

Mwiba,

Huu ndio ujinga wa sisi Waafrika, kutumia failure moja ya Wazungu kuhalalisha failures zetu 1000.

Wamarekani wana system yao in place hata kukitokea tatizo kama lile la Bush bado effect yake kwa wananchi wa kawaida ni ndogo sana.

Effects za failures zetu, ni vifo, ujinga na umaskini kwa maelfu ya watu.
 
Hebu tujaribu kuwa analytical kwa kuweka kwanza kando swala la wizi wa kura at least kwa sasa! Kwa maoni yangu;

1. Kura za maoni predicted a neck to neck contest- na matokea haywajawa tofaoti sana na kura za maoni!

2. Ndo maana nikasema Kalonzo factor is key! If Kalonzo was assured VP na ODM na akampigia debe Raila- huku Ukambani wangempa kura Raila! Hizi kura za Ukambani nyingine zimeenda kwa Kibaki kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa Kalonzo kuwa Makamu wa Raisi kwa Kibaki! This assuarance was not evident if Raila had won as he already miscalculated in declaring Mudavadi as arunning mate!

Remember Kibaki was hasitent in declaring a running mate- na sheria Kenya haimbani kama hapa Tanzania!

That is why Kilonzo can be used as a deciding factor of winning or loosing for both candidates!
 
Kura za maoni pia zilisema John Kerry na Al Gore wameshinda urais wa marekani!

2. Ndo maana nikasema Kalonzo factor is key! If Kalonzo was assured VP na ODM na akampigia debe Raila- huku Ukambani wangempa kura Raila! Hizi kura za Ukambani nyingine zimeenda kwa Kibaki kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa Kalonzo kuwa Makamu wa Raisi kwa Kibaki! This assuarance was not evident if Raila had won as he already miscalculated in declaring Mudavadi as arunning mate!

Hapa ndio unaonyesha kabisa kuwa hujui siasa za kenya au hukufuatilia kilichotokea. Kama Kalonzo angekuwa VP na basi akampa Raila kura za ukambani, vipi kuhusu kula za waruhya wa western waliompiga chini hadi VP wa kenya wa sasa ili Raila awe rais?

Rudi tena katafute spin mpya.

Remember Kibaki was hasitent in declaring a running mate- na sheria Kenya haimbani kama hapa Tanzania!

That is why Kilonzo can be used as a deciding factor of winning or loosing for both candidates!

VP aliyechaguliwa na Raila ni wa kabila gani? na je raia amefaidiika vipi huko?
 
Mwiba,

Huu ndio ujinga wa sisi Waafrika, kutumia failure moja ya Wazungu kuhalalisha failures zetu 1000.

Wamarekani wana system yao in place hata kukitokea tatizo kama lile la Bush bado effect yake kwa wananchi wa kawaida ni ndogo sana.

Effects za failures zetu, ni vifo, ujinga na umaskini kwa maelfu ya watu.

Kweli kabisa Mtanzania,

ukiangalia watu wengi wanaojaribu kutetea ufisadi uliofanyika hapa kila mara wanatumia uchaguzi wa marekani kama mfano as if kama wazungu ndio bench mark na wakifanya wizi basi kila mtu awe mwizi.
 
Wasiwasi wetu tulio wengi ni kwamba, iwapo tu katika kusubiria matokeo ya kura zilizochelewa kuhesabiwa yamesababisha vurugu za namna ile, inakuwa vipi kwa matokeo "yaliyopikwa"? Huenda ni sababu hizi zilizofanya jamii za Waasia waliopo Kenya kukimbilia nchi jirani ya Tanzania ili kukaa mbali na shari itakayotokea iwapo hali isingekuwa kama vile wavavyotarajia.
Hizi tiktak inatakiwa vijana wa Afrika tuzikatae, inabidi tuinuke na kupinga upishi wa matokeo.
 
It is really sad kuona watu kwanapigwa changa la macho hivihivi sijui kitu gani kitatokea kwa ndugu zetu wa kenya kwani wamesema hawatakubali mpaka kieleweke.
 
....

Kwenye kila uchaguzi kuna two sides, ya academic na ya malalamiko ya kufanyika kwa uhuni, kama vile uchaguzi wa US mwaka 2000,

Gore, alitaka kura za baadhi ya majimbo ya uchaguzi ambayo alikuwa akijua wazi kuwa hayo majimbo ni ya Democrat kule Florida, yarudiwe kuhesabiwa kura, huku akijua wazi kuwa sheria za US zinasema wazi kama ni kurudiwa kwa kura, basi ni kura zote za State of Florida zilitakiwa zirudiwe kuhesabiwa, alijua kuwa zikihesabiwa zote za State, hatashinda, ingawa haibadilishi ukweli kuwa kuna mchezo mchafu ulichezwa na political system nzima ya State of Florida, ambayo ilikuwa ni Republican,

hapa ndio umekosea tena sheria za marekani mkuu, sheria ya marekani inasema kura za kituo chochote zikiwa na kasoro zinaweza kupingwa na kuhesabiwa bila kufanya state nzima kama hakuna pingamizi na mgombea mwingine.

kasome vizuri fact zako za marekani maana inaonekana unakosea mamabo mengi sana.

Ukiangalia Kenya, ni kwamba political system nzima ya huko ni Kikuyus, je kweli wangeweza kumpitisha Odinga? Sawa kuna mchezo mchafu umefanyika, lakini pia kuna makosa yaliyofanywa na ODM kwa kuelewa wazi kabla hata ya kuanza uchaguzi kuwa haitakuwa rahisi kushinda system ya nchi yao ambayo ni dominated na the Kikuyus, kwa chama cha Kikuyus, kwa kweli kuna mengi ya kujifunza academically, ingawa pia huwezi kuangalia mchezo mchafu uliochezwa pia!

hapa pia unazidi kukosea. Population ya kikuyus ni less than 50% kwa hiyo ODM alitegemea tribes zingine zote zingeungana na kushinda. Mkuu vipi leo mbona kuna gaffs kibao kwenye facts zako ingawa wewe huwa ni mtu wa dataz sana?
 
Najua Mkuu wa Majeshi ni Mkikuyu mwenzake na Mkuu wa Polisi ni Msomali Mkenya , ila naamini watakuwa wise sana na kuacha kuwaua wapinzania maana itawaumiza sana . Ni ajabu sana na aibu kubwa .Yaani ameogopwa kupigwa Mahakamani ama ni kitu gani ? Jeshi lilikuwa limeshika Nchi we all knew that .

Anyway niko Kiserian sasa hapa Nairobi yapata km 60.Napata simu kwamba maeneo mengi ya Kenya vurugu ni kubwa sana .Watume jifungia majumbani . Naongea na mtu mmoja Eldoret hapa sasa hata kuwasha taa hataki anasema Estate nzima ni ngumu na hajui nani atapona .

Kibaki ana wabunge wachache sana ukilinganisha na ODM wana wabunge 90+ je anadhani kuwa rais pekee kutatosha yeye kuwa mtawala wa Kenya ?
 
this is when those guys we call freedom fighters seems to be free madaraka fighters.
vijana wa afrika tuna kazi kubwa. huu ni wakati wa kutafuta uhuru wa kweli na kuachana na unafiki wa akina Nyerere, Kenyata etc. ni wakati wa kuiuliza kwamba kama Nyerere asingezaliwa, wakoloni wasingeondoka tanzania wakati ilikuwa imefika time ya wazungu kubadilisha kutoka direct conization na kuingia indirect colonization?
vijana tuna kazi, lazima tustop kuwa mbuzi wa shughuli na kupelekwa pelekwa tu
 
Usisahau pia kuwa jaji mkuu wa mahakama kuu ni mkikuyu na rafiki mkubwa wa Kibaki. Jaji huyu ameongezewa muda karibuni tu na Kibaki maana alitakiwa awe amestaafu saa hii.

Jamaa walipanga huu wizi muda mrefu na akabadilisha tume ya uchaguzi miezi michache kabla ya uchaguzi kwa kujaza watu wake na akajua kuwa hata akiiba kura kesi ikienda mahakamani bado tu atashinda.

Umemsikia pia Kibaki akitangaza kuwa kesho ni siku ya mapumziko ili kusiwe kabisa na nafasi ya kwenda mahakamani mpaka jumatano kama watu watakuwa wamesalia maana sasa hivi report ta media zinaonyesha fujo tu na labda jamaa ikifika jumatano atatangaza hali ya hatari na mchezo utakuwa umekwisha.

Anyway niko Kiserian sasa hapa Nairobi yapata km 60.Napata simu kwamba maeneo mengi ya Kenya vurugu ni kubwa sana .Watume jifungia majumbani . Naongea na mtu mmoja Eldoret hapa sasa hata kuwasha taa hataki anasema Estate nzima ni ngumu na hajui nani atapona .

Stay safe mkuu taifa na JF inakutegemea.

Kibaki ana wabunge wachache sana ukilinganisha na ODM wana wabunge 90+ je anadhani kuwa rais pekee kutatosha yeye kuwa mtawala wa Kenya ?

kibaki ana wajumbe wachache lakini kumbuka kuwa very likely atampendekeza kalonzo kuwa VP na kupata wabunge wa ODM-k (15) na atachukua wabunge kama 10 wa kanu, na vyama vidogo vidogo vingi vitaenda kwake so atapona kura ya no confidence.

Kwa sasa ndio imetoka hivyo na tusubirie zimbabwe nyingine kwenye northern border.
 
this is when those guys we call freedom fighters seems to be free madaraka fighters.
vijana wa afrika tuna kazi kubwa. huu ni wakati wa kutafuta uhuru wa kweli na kuachana na unafiki wa akina Nyerere, Kenyata etc. ni wakati wa kuiuliza kwamba kama Nyerere asingezaliwa, wakoloni wasingeondoka tanzania wakati ilikuwa imefika time ya wazungu kubadilisha kutoka direct conization na kuingia indirect colonization?
vijana tuna kazi, lazima tustop kuwa mbuzi wa shughuli na kupelekwa pelekwa tu

Kamala,

Tatizo sio akina Nyerere au Kenyatta ambao angalau walituletea uhuru.

tatizo ni hawa ambao walikuwa wadogo wakati nchi zetu zinapata uhuru, hawakushiriki kwenye mapambano ya kuzikomboa nchi zetu na ndio walitakiwa wafanye mapinduzi ya kiuchumi. Hawa ndio wabaya mno, ndio wanaiua Afrika.

Sasa sisi wengi tuliozaliwa baada ya uhuru, tumeanza kuchoshwa na ujinga wao. Inabidi ifike mahali hata bakora zitembee vinginevyo tutakuwa wajinga mpaka lini?

Hii story ya mkoloni sasa imechuja, tunataka maendeleo kwa ajili ya watu wetu, full stop.

Hata JK wala hata wasiwasi hana maana anajua hata wananchi wakichukia, ataiba tu kura.

Yaani mimi leo nimechukia sana kama nilivyochukia 1995, 2000 na 2005 kuhusu Zanzibar.

Tatizo kubwa la Afrika ni hao cronies wao ambao wanaona kwasababu wanafaidi sasa basi system inafaa. Wanachosahau ni kwamba tumewaona akina Mangula wakiporomoka na kurudi kulima ambako hata bei wanapunjwa.

System iliyo fair ni pension ya maisha kwa kila mtu.
 
Asante sana mtanzania,

unajua kuna watu wanapenda sana kuhamisha uovu wao na matatizo kwenda kwa wengine. Utaona kiongozi wa afrika anaiba kura kisha anasema kuwa hata marekani wanaiba kura. Kina Mugabe wanapigiwa kelele na wananchi wao wanasema mbona hata Bush hapendwi na wamarekani lakini hajiuzulu.

Wengine kama Kamala wakiona hakuna mzungu au mwarabu wa kulaumiwa basi wao wanaanza kulaumu viongozi waliopita ili tu basi wao wasionekane kuwa na makosa au nafasi ya kulaumiwa.

Kuna mfano mmoja Mkandara aliwahi kuutoa hapa kuhusu Nyerere na wale ambao wanasingizia matatizo ya afrika kwa kumlaumu nyerere na kina kaunda.

Mkandara alisema kuwa (nitajaribu kuitafuta hii post baadaye) kwa sasa ninaparaphrase: 'kama ukizaliwa kwenye familia ambayo baba ni mlevi na hajali kabisa familia, anakataa kuwasomesha nyie kama watoto wake, na kutumia mali yote kwenye pombe, je wewe nawe ukikua mkubwa na ukawa na familia yako utaacha kufanya chochote kuisaidia familia yako na kubaki ukilia na kumlaumu baba yako kuwa ndio amesabababisha hayo? je the same game iendelee pia kwa watoto wako?'

Ifikie hatua waafrika na vijana wa sasa tusema NO na tukatae kwa nguvu zote huu unyonyaji na unyanyaswaji ili hata watoto wetu nao waje kuwa na mataifa bora na sio kama haya tunayorithi kwa wazazi wetu wa sasa.
 
Hebu tujaribu kuwa analytical kwa kuweka kwanza kando swala la wizi wa kura at least kwa sasa! Kwa maoni yangu;

1. Kura za maoni predicted a neck to neck contest- na matokea haywajawa tofaoti sana na kura za maoni!

2. Ndo maana nikasema Kalonzo factor is key! If Kalonzo was assured VP na ODM na akampigia debe Raila- huku Ukambani wangempa kura Raila! Hizi kura za Ukambani nyingine zimeenda kwa Kibaki kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa Kalonzo kuwa Makamu wa Raisi kwa Kibaki! This assuarance was not evident if Raila had won as he already miscalculated in declaring Mudavadi as arunning mate!

Remember Kibaki was hasitent in declaring a running mate- na sheria Kenya haimbani kama hapa Tanzania!

That is why Kilonzo can be used as a deciding factor of winning or loosing for both candidates!

Mzalendohalisi,

Mambo kama yaliyoandikwa hapa chini, utafanya strategy gani ambayo ingefanya kazi kwa Odinga? Huu ni ujambazi, ingelikuwa mitaani Dar Vibaka wanapigwa viberiti, sasa Kibaki naye Wakenya wamfanye nini?

The Chief Observer of the EU Election Observation Mission (EU EOM), Alexander Graf Lambsdorff, Member of the European Parliament, issued the following statement about the announcement of the winner of the presidential election in the Republic of Kenya:

“Once again, we would like to commend Kenyan citizens for the strong commitment to peace and democracy that they showed on election day.

With a view to the presidential elections, however, we believe that, at this time, the ECK, despite the best efforts of its chairman, has not succeeded in establishing the credibility of the tallying process to the satisfaction of all parties and candidates.

We regret that it has not been possible to address irregularities about which both the EU EOM and the ECK have evidence. The result for the Molo constituency, for example, was announced in the presence of EU EOM Observers at the constituency tally center as 50.145 votes for President Kibaki, while the ECK today declared the result for the President to be 75.261 votes. Because of this and other observed irregularities, some doubt remains as to the accuracy of the result of the presidential election as announced today.

We call on the leaders of Kenya to maintain this spirit of peace and democracy so admirably shown by the people of Kenya on Thursday.”
 
Back
Top Bottom