Kesi za epa-wafanyakzi wa bot jela miaka 5

Kesi za epa-wafanyakzi wa bot jela miaka 5

JK ni noma,EPA ilimuingiza ikulu lakini leo wanafungwa mamesenja.ambao hawana hela za kujiua kiaina kama balali.
 
Kuna haja ya kubadili sheria ya maswala kama haya ili iwe fundisho.
Miaka 5 michache mno.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Sheria imechukua mkondo wake kwa hisani ya CCM waliokula hizo mbumba
waliokula mbumba si hawa mkuu wangu, waliokula mbumba wapo miji mikubwa kama cape town, washngton wakitanua kwa majumba makubwa waliojenga, hawa ni mesenja tu, katika utetezi wao walieleza kila kitu, lakini majaji wa voda fasta hawakusikia la kuambiwa badala ya kikikwete. jiulize wewe pale ofisini kwako, unapotekeleza wajibu wako ni vitu vingapi unasaini kwa maagizo ya toka juu? yakikukuta haya utasemaje?
 
un
Kuna haja ya kubadili sheria ya maswala kama haya ili iwe fundisho.
Miaka 5 michache mno.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

una hakika unachoandikia, kwa nini kusiwe na haja ya kuhakikisha mafisadi papa wanafikishwa mahakamani badala ya kuwatosa kafara watu wa aina hii/
 
Ni kweli mkuu, nasikia ni instructions tu zilikuwa zinatoka na wanaamriwa wakatekeleze hata kama ni week end walikuwa wanaitwa na kupigiwa simu na wakubwa ili kufuatilia kama mzigo uko tayari. Wametolewa Kafara kabisa hawa. Hawakuwahi kuwa na kampuni ya kuuiba hela ya EPA.

Hili ni somo kwa watumishi wa umma kwamba watawala hawapaswi kusaidiwa kutenda dhambi kupitia watumishi kisa eti wanatekeleza maagizo ya majizi. Hizi ni salam pia kwa mkurugenzi wa TBC kwamba ipo siku wananchi tutamshitaki na ajiandae kuwajibika kwa kutusababishia kuichukia TV yetu
 
Safi sana JK pambana na mafisadi.
 
Wao hawakuwa na hela za kwenda KUFIA marekani kama Daudi?

Gharama za KUFIA Marekani ni kubwa sana na kwa mawazo yangu-VIFO vingi (maofisa watano) kwa pamoja azima vingekuwa zengwe kubwa ambalo kuliatamia ingekuwa kazi ngumu sana!
Ona KUFA kwa Gavana Balali ambavyo hadi sasa kunatukunisha viungo tukunavyo tukiwaza magumu KUWAZIKA; KUFIA Chezea KUFIA Marekani weweeewee....
 
Nimeweka hapa ripoti yenyewe ya EPA kwa wale ambao walikuwa hawajaiona. Ni ripoti ya CAG juu ya EPA. Ukurasa wenye majina ya waliowekewa fedha kwa udanganyifu ni kati ya page 21 na 22 (kuna kurasa za nyongeza). Iko faint kidogo kwa sababu ya photocopying.
 
Hizi ni baadhi ya kurasa zenye kutaja malipo yenye mashaka, (na cover page).
attachment.php

attachment.php

attachment.php
 
Pages za introduction hizi hapa. Kuna nyingine zimeondolewa hapa, zikiwemo zile zenye saini za waliotayarisha ripoti.
attachment.php


Pages missing here
attachment.php
attachment.php

attachment.php
 
Tukumbushe majina yao Mkuu maana nakumbuka wachache kama Imani Makosya, Esther Komu, Bosco Kimela na wengine wawili sikumbuki. Sema wana kesi tofauti tofauti. Dah!!

Ni kuwaonea tu. Unawafunga hao then vigogo walio-master mind mchongo wote wanapeta. Hiyo ni geresha tu.
 
Wafanyakazi wa bot ambao walikuwa wanshatakiwa kwa kesi zile epa kutoka kitengo cha madeni ya nje, wamapatikana na hatia katika hukumu ilyosomwa jioni na kuhukumiwa miaka 5 jela


source: Mahakamani jioni hii

Na wale waliojichukulia imekuwaje? Je, waliorudisha pesa za wizi nao imekuwaje?

 
hv walishindwa kurudisha?mbona wako waliorudisha wakasamehewa bana?

Hao mkuu ni wafanyakazi wa BoT, eti wamefungwa kwa uzembe si kwa wizi. Wezi wote wako mitaaani wanaendelea na maisha kama kawaida.
 
Back
Top Bottom