Kesi za epa-wafanyakzi wa bot jela miaka 5

Kesi za epa-wafanyakzi wa bot jela miaka 5

exactly mkuu, hawa walipewa amri watoe pesa, wengi wao ni maskini wa kutupa, wale waliotajirika na hizi pesa, rostam, lowasa, mangula, jk wako mtaani wakijinafasi.
Mungu atakuwa na hawa
ukikubali kutumiwa na wanasiasa madhara yake ndio hayo. sioni haja ya kufungwa miaka 5 wakiwa wametumia vyeo walivyo navyo kuididmiza uchumi wetu hapa tunadanganywa tu ili ionekane wanatekeleza kile tunachokitaka
 
issue nzima ya epa ni usanii mtupu maana aliye anzisha kuchota ni ile kampuni inayo julikana kama kagoda lakini hiyo kampuni haisungumzwi kabisa kwenye hiyo kesi na watanzania tunaona sawa mali ya umma wacha iliwe"belongs to all belongs to no body"
 
Tuwekee majina ya hao waliofungwa maana wasiwe wamebambikwa watu wengine. Na je naeao wakitoka watafirisiwa mali zao kama akina malando? Na nizepi mali zao
 
huo ni uonevu tuuuuu!mafisadi papa wanatesa mtaani,masikini ndiye anayehukumiwa.Tangu lini mwizi anaambiwa arudishe hela thn anasamehewa?

Ndio serikali ya chukua chako mapema (CCM). Pole zao. Wao wamewajibishwa kama wao..work ethics! Na kwa mwendo huu wangeingia mawizarani aka taasisi tungeumia wengi. Jaji mkuu angeifanyia kazi ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali..magereza hayangetosha.

Je na bodi ya BOT si waliidhinisha vilevile mbona wadogo tuuu.. twafa sisi wadogo papa wanapeta na hela zao uswiss CDM ikichukua nchi haoooo wanapaa. +
 
Naona hii ni wiki ya mvua tuu,tukianza na marehemu Fundikira na hii ya EPA,whats next,nasikia na ya yule Mwarabu aliedaiwa kupeleka watu Utumwa Yemen hukumu yake ni wiki ijayo?tutege masikio tuone matokeo!!!!!!!
 
Hao ni wafanyakazi wa BOT vp wezi wenyewe kina jeetu patel, rostam, n.k kesi zao zikoje, huu ni mchezo mwingne mchafu wa mfumo mzma wa sheria, hao wametolewa km chambo tu ili wezi wenyewe waendelee kupeta.
 
Mbona kila siku anafungwa "Malanda" tu "mbao" zenyewe vipi? Aliyekwiba nyingi ni KAGODA lkn haguswi yeye wala "Kasturi" huu ni usanii tu, unamuacha aliyevunja kontena na kuingiza fuso kuchota mali unaangaika na aliyeokoteza vitu vilivyoanguka wakati wa tukio. Nimependa wezi kufungwa lkn sikubaliani na hii biased categolisation ya wizi.
 
Hili ni somo kwa watumishi wa umma kwamba watawala hawapaswi kusaidiwa kutenda dhambi kupitia watumishi kisa eti wanatekeleza maagizo ya majizi. Hizi ni salam pia kwa mkurugenzi wa TBC kwamba ipo siku wananchi tutamshitaki na ajiandae kuwajibika kwa kutusababishia kuichukia TV yetu

Aisee mku, TBC ni janga la Kimataifa!! Ile TV itakufa au huduma zitadorora kiasi kwamba haivutii hata matangazo. Ila ninakua kile chama chetu kitainusuru maana inawasaidia kupiga debe. Kazi nzuri aliyofanya Tido Mhando imepotea bure.
 
Safi sana JK pambana na mafisadi.

Aaaa wapi? Mafisadi wapi hao? Papa au vidagaa? Tunaitaka Kagoda, Deep Green na wenzake!! Mfadhili wenu RA vipi? The king maker!!
 
Miaka 5 ni mazingira ya kutoka kwa msamaha wa rais
 
Makampuni 13 yanayotajwa kwenye ripoti ya CAG kuhusika na scam hii:
  1. Kagoda Agricultural Ltd.
  2. Bancon Int. Ltd
  3. VB & Associates Co. Ltd
  4. Bina Resorts Ltd. of Tanzania
  5. Venus Hotel Ltd of Tanzania
  6. Njake Hotel & Tours Co. Ltd of Tanzania
  7. Money Planners and Consultants
  8. Bora Hotels & Apartments Ltd.
  9. BV Holdings
  10. Ndovu Soaps Ltd.
  11. Navy Cut Tobacco (T) Ltd
  12. Changanyikeni Residential Complex na
  13. Mahan Mining Co. of Tanzania

Mkaguzi alitaja kuwa mengi ya hayo makampuni hayalipi kodi, au yanalipa kodi ndogo mno. Mawili kati yao hayakuwa na usajili wa Brela.

Mkaguzi pia alishauri makampuni hayo yachukuliwe hatua za kisheria pamoja na wakurugenzi wake.

Wanaojua nini kilitekelezwa na serikali watujuze.
 
Back
Top Bottom