Kesi ya Uhaini ya Lissu: Serikali hii ni ya laana, imewatafuta watu wenye dhiki ya maisha na kuwafanya mashahidi wa kificho

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
6,512
Reaction score
15,096
Kwenye kesi bandia iliyotengenezwa na watawala dhidi ya Lisu, kila mmoja alishangaa kuona wale mawakili wa mchongo wa serika wakikazania kuwa na mashahidi wa kificho. Watu mbalimbali walitoka na hisia tofauti tofauti. Baadhi mpaka walifikia kusema kuwa labda wale waliokuwa viongozi wa CHADEMA na kisha kuhamia chama cha CHAUMMA, ndio watakuwa mashahidi wa kificho. Sasa ukweli ndiyo umewekwa wazi hawa mashahidi wa kificho ni watu wa namna gani na kwa nini ilikiwa haiwezekani kuwaweka wazi:

Katika hiyo kesi ya kubumba, wale mawakili mchongo wa watawala, kwa kuwa hawana mashahidi kwenye hiyo kesi ya kubumba, wameamua kuwatengeneza mashahidi. Na kwa vile mtu mwenye akili timamu na ambaye anajimudu kimaisha hawezi kukubali kutumika kwenye huo ushahidi shetani, hawa watu wameamua kutumia umaskini na dhiki za watu ili kufanikisha uharamia wao.

Wamewatafuta watu wa kipato cha chini sana, na kisha kuwaahidi malipo mazuri kwa kukubali kutumika kwenye uharamia. Lakini changamoto waliyokutana nayo mawakili mchongo wa watawala, watu hawa wana uelewa wa chini na wanaweza wasiwe na kumbukumbu nzuri hata baada ya kufundishwa.

Hivyo wakatengenezewa majibu ya maswali watakayoulizwa, na pale wanapoulizwa, wao wanatakiwa kusoma tu kile walichoandikiwa. Kwa vile hawawezi kusoma majibu huku majaji, mshtakiwa na wahudhuriaji wengine wa mahakama wakishuhudia, ndiyo wakaja na hiyo hila ya shahidi wa kificho.

Shahidi anakuwa kwenye kachumba, akiulizwa swali, anaposoma majibu aliyoandikiwa, hakuna anayemwona, lakini wenye akili timamu, shahidi wa namna hiyo, anaposoma, inakuwa ni wazi kabisa kuwa huyu anasoma, maana hata usomaji wao umekuwa wa kubabaisha. Ndiyo maana wakili mchongo akikosea akamwuliza swali la mbele, shahidi wa kificho anajibu kwa kusoma jibu la swali jingine ambalo lipo kwenye mpangilio wa majibu aliyopewa ayasome, na hakika inabakia ni kichekesho mbele ya wasikilizaji.

Mashahidi mchongo wa kificho, ni orodha inayojumuisha baadhi ya bodaboda na machinga.
Kwa leo, fuatilieni majibu ya shahidi Mchongo wa Kificho:
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Leo February 13, 2026

Jana tuliishia Part 167 so leo tunaendelea na-;

Part 168

Mahakama imeanza muda huu saa tatu na nusu.

Mhe. Lissu anaingia akiwa amevaa kombati nyeusi.

Sauti ya High Courttt inapigwa kila mtu anasimama na kelele za kumsalimia Mwenyekiti zinasimama kidogo.

Majaji wanaandika kidogo pale mbele.

Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude anasema yupo na Ajuaye, Katuga, Ignas, Cathbert na Winiwa na wote tunawakilisha Jamhuri na Mshitakiwa yupo.

Sisi tuko tayari kuendelea na leo tumekuja na P6 yuko tayari, endapo Mshitakiwa atakuwa tayari.

Mhe. Lissu anaulizwa na yeye anasema yuko tayari.

Jaji Ndunguru: Naomba shahidi aje sasa.

Shahidi analetwa kama Bangi kule mbele kwenye kibox hatumuoni chochote tunaona milango tu inafunguliwa sijui amevalishwa baibui.😂

Mlango wa kizimba umefunguliwa muda huu.

Shahidi anaulizwa umri wake anasema miaka 24 na ni Mkristo so anaapishwa muda huu.

Jaji anauliza nani atamuongoza? Anajibiwa ni Cathbert Mbiringe Wakili wa Serikali ndio atamuongoza.

Anamuuliza unanisikia.

Haya mkazi wa wapi?

Mimi natokea Ruvuma Songea na kazi yangu ni Afisa Usafirishaji Bodaboda, nafanyia huko huko Songea shughuli zangu.

Mwezi October 2024 ni mwaka ambao nilianza kushirikisha siasa za Chama cha Chadema.

Wakili: Ulishiriki kivipi?

Shahidi wa kificho P6: Nilianza kushiriki kwenye mikutano ya hadhara na kuwafuatilia viongozi mbalimbali wa Chadema na nikafanikiwa kuwafahamu Mhe. Lissu na baadhi ya Viongozi waliokuwepo Songea.

Wakili: wakiwepo akina nani?

Shahidi wa kificho P6: nilimfahamu Katibu wa Vijana Songea.

Wakili: Alikuwa anaitwa nani?

Shahidi wa kificho P6: alikuwa anaitwa Chiza au Mwamba wa Kigoma maarufu kwa jina hilo.

Wakili: January 2025 unakumbuka nini?

Shahidi wa kificho P6: Nilianza kuwa nimeshiriki siasa za Chadema na kuvutiwa kuwa mwanachama wa Chama hicho.

Nikaanza jitihada za kutafuta viongozi waliopo Songea, nikamfuata kiongozi wa Vijana Chiza na kumueleza nia yangu ya kutaka kuwa mwanaChama.

Wakili: Nini kiliendelea baada ya hapo?

Shahidi wa kificho P6: Alinipokea na kunisifia kwa uamuzi mzuri. Akasema napaswa kuwa na kadi ya Chama, nilifuatilia hiyo kadi na nikaambiwa nisubiri mashine bado ni mbovu na ataendelea kunishirikisha kwenye shughuli za Chama.

Wakili: Zipi hizo shughuli za Chama?

Shahidi wa kificho P6: Sisi bodaboda huwa tunakuwa kwenye misafara ya Chama na bendera.

Wakili: Tar. 04/04/2025 kilitokea nini?

Shahidi wa kificho P6: Hiyo tarehe nikiwa sehemu yangu ya kazi pia nikiwa na simu yangu ya mkononi aina ya infinix smart 8 nikiwa naangalia mtandao wa Youtube.

Wakili: Youtube ni nini?

Shahidi wa kificho P6: ni mtandao wa kijamii ambao unamuwezesha mtu kutuma video, audio na maudhui mengine.

Huyu Bodaboda wa miaka 24 anavyoelezea mambo unashangaaa ni kama anajibu essay huyu atapata tabu kwenye maswali. 😂

Anaendelea kuwa simu yake ilikuwa na internet na aliingia google kumuwezesha kuingia youtube.

Shahidi wa kificho P6: Niliingia kwenye account ya Jambo TV nilifanikiwa kuona na kusikiliza hotuba aliyokuwa anatoa Mwenyekiti wa Chama cha Chadema ambapo alionekana akihutubia watu akisema bila mabadiliko hakuna uchaguzi hivyo tunaenda kukinukisha.

Tunakwenda kuvuruga Uchaguzi pia nilisikia na kuona akisema tunakwenda kukinukisha na yeyote atakayekuwa pamoja nasi tutakwenda nae na ambae hatataka tutamuacha pia alisema kama kuna mtu yeyote anatarajia kugombea asahau jambo hilo.

Wakili: Pia akasemaje?

Shahidi wa kificho P6: Pia hata mimi kugombea uenyekiti msahau pia akasema bila mabadiliko hakuna Uchaguzi.

Wakili: Kingine kipi?

Shahidi wa kificho P6: Pia akasema watasema tunafanya uasi ni kweli utakuwa ni uasi kwasababu bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 169

Mazingira aliyokuwa anayatolea ilikuwa ni kama sehemu ya Ukumbini, ndo nilimuona hapo.

Muda huu ameingia Mtaalamu, Wakili Msomi Peter Kibatala wakati kesi inaendelea.

Amekaa pale karibu na Kizimba cha Mhe. Tundu Lissu, nimeona wanasalimiana kimya kimya Mhe. Lissu anacheka anamuonyeshea kidole cha Upendo ni kama anamwambia wewe kijana wangu wewe.😂

Wakili wa Serikali: Muonekano wa Lissu ulikuwaje?

Shahidi wa kificho P6: Alivaa Kombati ya Kaki.

Namfahamu Tundu Lissu kama mwanasiasa mkongwe na mwanasiasa maarufu.

Wakili: Baada ya kuona hiyo hotuba wewe ulifanya nini?

Shahidi wa kificho P6: Nilivyoona hiyo video maneno yake yaliniingia moyoni na kunishawishi.

Hiyo agenda ya kukinukisha ni kufanya vurugu au kuharibu miundombinu.

Wakili: huo uchaguzi ni upi?

Ukisikiliza majibu ya huyu Shahidi wa kificho ni wazi kaingia na desa anasoma majibu.

Anajibu hapa ni Uchaguzi Mkuu wa 2025 unaohusisha wabunge na Rais na Madiwani.

Wakili: Ikawaje baada ya kushawishika?

Shahidi wa kificho P6: Nikamfuata Mwenyekiti wa Vijana wa Songea alikuwa anaitwa Chiza maarufu kama Mwamba wa Kigoma.

Wakili: ikaendelea nini?

Shahidi wa kificho P6: Nikamueleza nilivyoshawishika na maneno ya Mwenyekiti na kutaka kuwa miongoni mwa watu tutakaokinukisha.

Wakili: Kikaendelea nini?

Shahidi wa kificho P6: Alinisifia sana kwa uamuzi mzuri na wakishujaa na akanipongeza na kuniambia Vijana kama nyie ndio vijana mnaotakiwa kulikomboa Taifa.

Wakili: Nini kikaendelea?

Shahidi wa kificho P6: Aliniambia ataniunganisha kwenye magroup yanayojadili mipango ya kuzuia Uchaguzi, akaniunga Group la SIASA YETU.

Group lilikuwa linaitwa SIASA YETU UPDATES.

Wakili: Nini kikaendelea?

Shahidi wa kificho P6: Niliendelea na shughuli zangu na yeye akaendelea.

Tarehe 06/04/2025 nilipata taarifa kuwa Mwenyekiti wa Chadema atakuwa ziarani mkoani Ruvuma.

Wakili: Mwenyekiti ni nani?

Shahidi wa kificho P6: Ni Mh. Tundu Lissu, hiyo taarifa nilipata kutoka kwa ndugu Chiza.

Wakili: Ikakutaka ufanye nini?

Shahidi wa kificho P6: Ilitutaka tufanye maandalizi na tarehe 10/04 atakuwepo Songea.

Wakili: Mlipanga nini kuhusu mkutano?

Shahidi wa kificho P6 ; Tulipanga mkutano ufanyike uwanja wa matalawe. Tarehe 09/04/2025 nilipata taarifa kuwa Mwenyekiti amekamatwa Wilaya ya Mbinga akiwa kwenye ziara ya Mikuta.

Watu wanashangaa mikuta ndio nini? Mashahidi wa siri wanasoma.. 😂😂😂

Shahidi wa kificho P6: Nilimtafuta Chiza kumuuliza kuhusu taarifa za Mwenyekiti kukamatwa Wilaya ya Mbinga.

Wakili: ikawaje?

Shahidi wa kificho P6: Akanijibu ni kweli amekamatwa lakini ratiba ya Mkutano wa Tarehe 10/04/2025 itakuwepo palepale. Kwahiyo jiandae kuwepo eneo la Mkutano Tarehe 10.

Wakili: hiyo Tarehe 10 sasa nini kikaendelea?

Shahidi wa kificho P6: Tulikusanyika uwanja wa Matalawe kusubiri viongozi walioambatana na Mwenyekiti kuhutubia mkutano.

Alikuwepo Godbless Lema na Dr. Wilbroad Slaa pia alikuwepo Mh. Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Mh. Heche.

Wakili: nini kikaendelea?

Shahidi wa kificho P6: Wakati tunasubiria likatokea gari ya Polisi na kusema kwa siku hiyo hakuna mkutano utakaofanyika eneo hilo. Na haruhusiwi mtu kukaa eneo hilo.

Wakili: nini kikaendelea?

P6: Ikabidi tutawanyike na kuelekea ofisi za Chama ili tufahamu kwa siku hiyo nini kitaendelea?

Wakili: Ziko wapi hizo ofisi?

P6: Ziko Songea sehemu inaitwa Mfaranyaki.

Wakili: kikaendelea nini?

P6: tuliwakuta viongozi ambao ni Adel Mayala ambae kwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini.

Wakili: Nini kiliendelea?

P6: Wakaja Polisi wakapiga mabomu ya machozi na kusema watu wote watawanyike.

Wakili: Saa saba mchana nini kiliendelea?

P6: Alikuja kiongozi Makamu Mwenyekiti na kusema kwamba amepokea barua kutoka Polisi kwamba kwa siku hiyo usifanyike Mkutano wa aina yoyote katika eneo hilo.

Wakili: Akasema nini kingine?

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 170

Shahidi wa kificho P6: Akasema tutawanyike na atapanga tarehe nyingine ya mkutano huo.

Wakili: Huyo Makamu Mwenyekiti ni nani?

Shahidi wa kificho P6: Ni Mh. Heche.

Wakili: Tar. 18/04/2025 nini kilitokea?

Shahidi wa kificho P6: Nilipokea taarifa kuwa tarehe 20/04/2025 siku ya pasaka kutakuwa na matembezi ya hiyari ambapo katika matembezi hayo yataambatana na kuvalia tshirt zilizoandikwa agenda ya No Reforms: No Election ili kuendeleza agenda ya Chama.

Wakili: Kingine kilichoendelea?

Shahidi wa kificho P6: Ukafanyika utaratibu wa kuzipata tshrit na tunachangia elfu 10 ndipo zitasafirishwa hadi kutufikia.

Tukaambiwa hadi kufikia tarehe 20 basi tutakutana kwa ajili ya matembezi hayo ya hiari.

Wakili: Tar. 20/04/2025 kikaendelea?

Shahidi wa kificho P6: Tulijikusanya kwa ajili ya matembezi ya hiari kila mmoja alipata tisheti yake na tukakubaliana jioni majira ya saa 10 ndio matembezi ya hiari yatafanyika.

Wakili: Ulipata wapi hizo taarifa:

P6: Group la Siasa Yetu.

Wakili: Matembezi mlikubaliana mkutane wapi?

Shahidi wa kificho P6: Songea Mjini kwa Disi Kitimoto na ilipofika majira ya saa 10 huku tukiwa na bodaboda huku tukisubiri wengine. Mimi nilikuwa kwenye muonekano wa kuvaa tshirt iliyoandikwa agenda ya No Reforms: No Election.

Wakili: Nini kilitokea?

Shahidi wa kificho P6: Wakaja Polisi wakajitambulisha kwa ghafla kuwa wanatokea kituo cha Polisi Songea na wakatuambia tunahitajika kituo cha Polisi Songea kwa ajili ya mahojiano.

Wakili: Nini kiliendelea?

Shahidi wa kificho P6: Walitukamata na kutupeleka kituo cha Polisi Songea na wakatuhoji kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali.

Wakili: nini kikaendelea?

Shahidi wa kificho P6: Wakasema tutatoka kwa dhamana lakini tulihitajika kwenda kuripoti ofisi ya RCO.

Wakili: Tarehe 25/04 nini kiliendleea?

Shahidi wa kificho P6: Tuliripoti Ofisi ya RCO tumuelezee kilichotokea hadi kufika sehemu hiyo.

Wakili: Mhe. Jaji ndio hayo kwa shahidi huyo.

Watu wanashangaa sasa huyu shahidi sijui alikuwa anazungumza nini na kinasaidia nini kwenye Uhaini ni Maajabu, ngoja Tunasubiri aanze kuulizwa maswali hapa.

Jaji Ndunguru: Vipi mshitakiwa tukupe nafasi ujikusanye vizuri?

Mhe. Lissu: Mh. Jaji huyu shahidi nilishajiandaa nae toka juzi.

Sasa shahidi sijui wewe ni Kaka au Dada lakini naomba ujibu maswali yangu sawa?

Shahidi wa kificho P6: sawa.

Mhe. Lissu: Uliandika maelezo Polisi?

Shahidi wa kificho P6: Sijaelewa swali.

Mhe. Lissu: Kitaeleweka tu. Jibu swali langu Bwana.

Shahidi wa kificho P6: niliandika

Mhe. Lissu: Ukionyeshwa hayo maelezo yako utayatambua?

Shahidi wa kificho P6: ndio.

Mhe. Lissu: Ulisaini?

Shahidi wa kificho P6: Sikumbuki.

Mhe. Lissu: Mh. Jaji naomba aonyeshwe maelezo yake.

Shahidi wa kificho P6: Nimeyapata na ndio maelezo yangu niliyoandika Polisi Songea.

Mhe. Lissu: Je yana sahihi yako?

Shahidi wa kificho P6: sahihi yangu ipo ndio.

Mhe. Lissu: Ni maelezo ya Tar. 25/04/2025.

Shahidi wa kificho P6: Sioni hiyo Tarehe.

Mhe. Lissu: Angalia juu mwanzoni, anamsomea hilo eneo.

Shahidi wa kificho P6: Sijayaona hayo maelezo.

Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji nataka ku impeach huyu shahidi, nitamsomea maelezo yake, anamsomea hapa.

Mimi ni mkazi wa Bombambili, kazi yangu Bodaboda na kituo changu ni miembeni.

Ilipofika mwaka 2025 nilimfuata Katibu wa Vijana Essau Chiza alinikaribisha kwenye Chama na kunifanyia mpango wa kadi ya Chama.

Nakumbuka tarehe 04/04/2025 niliona mtandao wa youtube hotuba ya Lissu iliyokua inahusu uchaguzi 2025 iliyokuwa ikihamaisha uasi. Ilinipa moyo wa kijasiri wa kutaka kuvuruga uchaguzi.

Nikamtafuta Essau Chiza ambae ni Katibu kunipa mipango mingine ikiwemo ziara ya Mwenyekiti Taifa.

Anaendelea kumsomea maelezo yake yote hapa.

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 171

Mhe. Lissu anaendelea kumsomea Shahidi maelezo yake.

Amemaliza kusoma maelezo anamuonesha maeneo aliyodanganya au kuleta mkanganyiko.

1. Dini

2. Umri

3. Shughuli za Chama alizoambiwa atakuwa anataka kuzifanya

4. Tar. 04/04/2025 ulikuwa na simu infinix smart 8.

5. Hiyo simu yako lilikuwa na bando la Internet

6. Uliingia kwenye mtandao wa youtube wa Jambo Tv

7. Mimi mtuhumiwa nilisema yoyote atakayekuwa nasi tutaenda nae ambae hatataka tutamuacha.

8. Nilisema anayetaka kugombea udiwani au ubunge asahau na mimi niliyetaka kugombea urais nisahau

9. No Reforms: No Election.

10. Wanasema tutafanya uasi ni kweli tutafanya.

11. Niliitoa hotuba yangu ndani ya ukumbi na kulikuwa na bendera ya taifa na ya Chadema

12. Nilivaa kombati za kaki nayo nataka unioneshe.

13. Kwamba tutazuia uchaguzi kwa kufanya vurugu

14. Nataka niyaone maneno ya Mwamba wa Kigoma.

15. Kwamba Mwamba wa Kigoma alikusifia kwa uamuzi wa kishujaa na wewe ni mojawapo ya vijana mnaotakiwa kulikomboa Taifa.

16. Tar. 06/04/2025 ulipata taarifa kuwa Mh. Tundu Lissu atatembelea Mkoa wa Ruvuma.

17. Ulipewa taarifa ya kumpokea Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Mhe. Lissu anamsomea maeneo ambayo shahidi amedanganya au ameyasema leo lakini kwenye maelezo yake ya Polisi hajasema.

Anaweza msomea maeneo hata 50.

Kwa kifupi anachokifanya kuyataja hayo maeneo ni kama anamuandaa au kumlainisha shahidi kabla ya kuanza kumsokota, kuonyesha uongo wa shahidi.

Ameonyesha maeneo 20.

Mhe. Lissu Lissu: Anamuuliza je ungependa maelezo yako yapokelewe kama sehemu ya ushahidi na mimi nikuhoji sawasawa?

Shahidi wa kificho P6: Amenyamaza hasemi chochote, hapo haya ndo maelezo yangu na kama kuna kitu hakipo mimi ni binadamu siwezi kukumbuka kila kitu na kama kuna kitu nimekizungumza mahakamani siwezi kukumbuka kila kitu.

Mhe. Lissu: Shahidi Kaka yangu ungependa hayo maelezo yako yapokelewe kama kielelezo?

Shahidi wa kificho P6: Maelezo yangu niloyoyaandika Polisi au niliyozungumza hapa Mahakamani ndio nimetakiwa nizungumze mbele ya Mahakama.

Mhe. Lissu: wambie ungependa yawe sehemu ya ushahidi mahakamani.

Shahidi wa kificho P6: Maelezo yangu yawe ushahidi Mahakamani.

Hatimaye amekubali.

Majaji wanaandika sasa.

Huyu Shahidi amesumbua sana kuyakubali maelezo yake ili yapokelewe hapa Mahakamani.

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka?

Renatus Mkude anasema No Objection.

Jaji Nduguru: Basi maelezo haya yatakuwa ni D4.

Mhe. Lissu: Anasema ahsante sana, sasa anaendelea.

Kabla hujaapishwa hapa Mahakamani uliulizwa dini yako ukasema wewe ni Mkristo?

Shahidi wa kificho P6: Kweli

Mhe.Lissu: waeleze majaji kwenye hayo maelezo yako eneo la dini yako umeweka nini?

Shahidi wa kificho P6: Sijaona hapo.

Anasimama Katuga anaweka pingamizi watu wanamzomea.

Jaji anasema tuendelee

Shahidi wa kificho P6: Hapa Dini imeandikwa sioni vizuri.

Mhe. Lissu: Dini imeandikwa Muislamu?

Shahidi wa kificho P6: hapa sioni vizuri.

Mhe. Lissu: Umri wako je?

Shahidi wa kificho P6: Miaka 23 imeandikwa hapa.

Mhe. Lissu: Ulisema shughuli za Chama ulizopewa ni kuongoza misafara ya Chama ukiwa na bendera na pikipiki?

Shahidi wa kificho P6: Ni kweli.

Mhe. Lissu: Sasa hayo maneno yapo kwenye maelezo yako?

Shahidi wa kificho P6: Maelezo yanaonesha nitashiriki kwenye mikutano ni vitu ambavyo sikuviandika.

Mhe. Lissu: Kwahiyo hayo yameandikwa au hayajaandikwa?

Shahidi wa kificho P6: Maelezo yameandikwa kushiriki mikutano.

Mhe. Lissu: We Chadema wa Mapolisi usitupotezee muda, tuambie yapo kama yapo.

Shahidi wa kificho P6: sijui

Mhe. Lissu: Tarehe 04/04 umesema ulikuwa na simu yako infinix smart 8 tuambie kama hayo yapo kwenye maelezo yako?

Shahidi wa kificho P6: sifahamu.

Mhe. Lissu: Sijakuuliza unayafahamu au huyafahamu, nimekuuliza yapo au hayapo?

Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 172

Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P6.

Mhe. Lissu: Mhe. Jaji naomba shahidi ajibu maswali yangu.

Jaji: Hebu muulize tena.

Mhe. Lissu: Hayo maneno ya simu infinix smart 8 yapo au hayapo?

Shahidi wa kificho P6: sifahamu.

Jaji: Nafikiri lengo lako mshitakiwa ni ku empeach credibility ya shahidi kwahiyo akisema hafahamu wakati kielelezo kipo na sisi Mahakama tutakipitia. Basi acha aendelee kusema hafahamu.

Mhe. Lissu: Maneno kwamba ulikuwa na bando la kuingia youtube hebu tuoneshe kwenye maelezo yako hapo?

Shahidi wa kificho P6: Yapo.

Mhe. Lissu: Tuonyeshe.

Shahidi wa kificho P6: Majira ya saa nne niliona mtandao wa youtube hotuba ya Tundu Lissu.

Mhe. Lissu: Swali langu ni ulikuwa na bando la internet.

P6: Hayo hayapo.

Lissu: Kumbe una akili unaelewa. Tukienda hivi itakuwa vizuri. Haya tuendeleee.

Ulisema uliingia katika mtandao ya Jambo TV?

P6: Nilisema niliingia kwenye account.

Lissu: Hivyo hivyo account eheee yapo kwenye maelezo yako?

Shahidi wa kificho P6: Hayapo.

Mhe. Lissu: Umeeleza kwamba wakati nahutubia huo Mkutano nilisema maneno kwamba yeyote atakayekuwa nasi tutaenda nae na asiyetaka tutamuacha, yapo kwenye maelezo?

Shahidi wa kificho P6: Hayapo.

Mhe.Lissu: Ulisema nilisema kuwa kama kuna anayetaka kugombea udiwani asahau na anayetaka kugombea ubunge asahau, hayo nayo yapo kwenye maelezo yako?

Shahidi wa kificho P6: Polisi nilitoa ila hapa kwenye maandishi sioni.

Mhe. Lissu: Ahsante, Polisi ni waongo wamekuibia maneno yako, tuendelee.

Haya umesema nilisema maneno No Reforms, No Election, haya ni maneno yangu kweli nimeyasema sana.

Shahidi wa kificho P6: hayo sikusema. nilisema bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

Mhe. Lissu: Basi twende na hayo hayo, yapo kwenye maelezo au hayapo?

Shahidi wa kificho P6: Hayo maneno siyaoni kwenye maelezo.

Mhe. Lissu: Turudi kwenye simu kwenye maelezo yako yote Polisi nataka uniambie ulisema kama ulikuwa na simu popote pale? Nataka unioneshe humo kwenye maelezo yako?

Shahidi wa kificho P6: nilisema nimejiunga na magroup ya whatsapp kwahiyo maana yake ni simu.

Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama maneno ya bendera za taifa na Chadema yapo kwenye maelezo yako?

Shahidi wa kificho P6: Hayapo.

Mhe.Lissu: Kwamba nilivaa kombati za Kaki nayo pia yapo humo kwenye maelezo?

Shahidi wa kificho P6: Maelezo siyaoni.

Mhe. Lissu: Umemuelezea mtu anaitwa Essau Chiza pia anaitwa Mwamba wa Kigoma sasa tuoneshe Mwamba wa Kigoma kama yapo?

Shahidi wa kificho P6: Hayapo.

Mhe. Lissu: Ulisema Essau ni Katibu sehemu nyingine ni Mwenyekiti kipi ni kipi?

Shahidi wa kificho P6: Mimi sijasema hivyo.

Mhe. Lissu: Sasa wewe leta hayo maelezo nikuoneshe, anamsomea aliposema Mwenyekiti na aliposema ni Katibu.

Shahidi wa kificho P6: Mimi sikusema hivyo watakuwa mapolisi ndio walikosea.

Mhe. Lissu: Pole kwa kuingizwa chaka na mapolisi.

Shahidi wa kificho P6: Ahsante sana.

Watu wanacheka.😂😂😂

Mhe. Lissu: Ulisema ulivyohamasika kufanya vurugu tuoneshe hizo habari nazo kwenye maelezo yako?

Shahidi wa kificho P6: anasoma mambo tofauti kabisa.

Mhe. Lissu: Wewe ulihamasika kwamba utazuia uchaguzi kwa kukinukisha ndio nayataka yapo?

Shahidi wa kificho P6: Mimi binafsi maneno ya Mwenyekiti wa Chama yalinihamasisha na kupata moyo wa kijasiri na kunipa hamasa ya kuvuruga uchaguzi mkuu 2025 kwa kukinukisha.

Mhe. Lissu: Ohoo Hongera sana kumbe wewe na mimi letu lilikuwa moja ila Mwenzangu uko kizimba cha shahidi nashangaaa. Haya tuendelee lakini.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 174

Anaendelea Mhe. Lissu

Mhe. Lissu: Mhe. Jaji hawako serious hawa kwanza ukisoma D4 kila kitu chake kipo hata jina lake hawajaficha lipo na taarifa zake zote zipo, hawajielewi hawa.

Katuga: Anasimama anasema Mh. Sisi ni maafisa wa mahakama aonywe mshitakiwa kwanini anasema hatuko serious.

Mhe. Lissu: Mh. Jaji ni kweli hayupo serious ila nataka niliondoe neno hilo lakini kama anasema nionywe siko tayari kuonywa naomba nifanye submission ya kuonesha ni kwa namna gani hawako serious?

Jaji Ndunguru: Basi Mshitakiwa tuishie hapo kama umesema umeliondoa.

Watu wanacheka sana. 😂😂😂

Mhe. Lissu: je umesema kokote kuwa uliwahi kutishiwa maisha?

Shahidi wa kificho P6: Sijawahi kutishiwa maisha mimi.

Mhe. Lissu: Kuna mwanachadema au kiongozi amewahi kukutishia kukupiga au kukudhuru kwa wewe kwenda kutoa maelezo haya Polisi?

Shahidi wa kificho P6: Hayupo kabisa.

Mhe. Lissu: Je kuna ndugu yako ametishiwa pia?

Shahidi wa kificho P6: Hayupo hata mmoja.

Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu.

Majaji wanaandika kidogo pale mbele.

Kwa sasa ni saa 7 na dakika 15 mchana, huu ni huwa ni muda wa kwenda Break, ngoja tusubiri Kitakachoendelea muda mfupi ujao.

Jaji: Re Examination Jamhuri?

Wakili Cathbert: Hatuna swali lolote Waheshimiwa Majaji.

Jaji Ndunguru Kiogozi wa Jopo la Majaji watatu anateta tena ma wenzake kabla hajasema nini kiendelee.

Anawasha kipaza sauti.

Shahidi umemaliza sasa unaweza kwenda.

Renatus Mkude tunaomba ahirisho tukawaandae mashahidi, lisaa limoja.

Mhe. Lissu: Sawa sina pingamizi.

Jaji Ndunguru: Basi tukutane baada ya lisaa limoja.
 
FB_IMG_17709799228154747.jpg
FB_IMG_17709799143204975.jpg
shahidi wa leo ndio huyu, hawa ndio akina lucas wanaotusumbua humu jf hawajui wanafanya nini akili zao zipo uchi.
 
Nimewahi kuwa shahidi wa watendaji wa serikali walipiga hela. Labda usome maswali ya wakili wako, ila ya wakili wa upande wa pili, utaishia kukenua tu . Utachapwa vibaya sana
 
Kwa maelezo haya, mbona shahidi P6 naye tayari ni mtuhumiwa wa uhaini kama Lisu?

Wajuvi wa sheria, huu ni ushahidi kweli au ni nini?

Sijasikia ama kuona mahali popote huyo shahidi alipoonesha kutokuunga mkono na kuukana huo uasi, badala yake kasema alihamasika kwenda kufanya uasi na machafuko.

Kwanini naye asigeuziwe kibao kwa kutoa ushahidi wa kujiunga na kudhamiria kutenda makosa anayoshitakiwa nayo mwenyekiti?
 
Kesi ya muhalifu Lissu haihitaji shahidi wote tuliona video akisema atafanya Uasi na atazuia uchaguzi na kweli genge lake la Nyumbu wasio na akili walijaribu kufanya uasi ila kwakua hawana akili wengi wameishia kaburini kwahiyo anastahili kunyongwa bila shahidi yoyote kusumbuliwa na serekali kupoteza mafuta kumpeleka na kumrudisha gerezani huyo muhalifu Lissu
 
Jisikitikie kwa kukosa akili. Pole nyingi kwa wazazi wako ambao hawakutegemea kuwa wangeishia kupata jitu lisilo na akili wala utu, jitu lililojaa fikra za ushetani na uovu, kama hivi ulivyo.
 
Huyu SHAHIDI P6 mbona kajiripua mwenyewe. Hivi kulikuwa na haja gani ya kumficha kama kweli alikuwa anamawasiliana na huyo Bwana Chiza. Ni wazi atafahamika baada ya muda mfupi tu ....!!
 
Umasikin ni mbaya sana

Lakin Mimi kwa ujinga kama huu hata kama ni masikin hunipati
 
Nimewahi kuwa shahidi wa watendaji wa serikali walipiga hela. Labda usome maswali ya wakili wako, ila ya wakili wa upande wa pili, utaishia kukenua tu . Utachapwa vibaya sana
Ndio kinachoendelea mahakamani, cha ajabu kwenye hukumu ambayo tayari mahakama wameshaandikiwa, Lisu atakutwa na hatia.!
 
Back
Top Bottom