WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 15.
Job Mrema: Kwa hiyo, kwa maana hiyo, moja ya majukumu yako ni kuhabarisha umma?
Brenda: Ndiyo.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba moja ya sheria inayosimamia masuala ya habari ni Media Services Act?
Brenda: Ni sahihi.
Job Mrema: Na wewe ukiwa kama Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi huwa unaitumia?
Brenda: Huwa inatumika.
Job Mrema: Inatumika na nani?
Brenda: Walio chini yangu na mimi huwa naitumia.
Job Mrema: Wewe umesoma nini?
Brenda: Accounting.
Job Mrema: Nitakuwa sahihi nikisema wewe siyo Mwandishi wa Habari?
Brenda: Mimi siyo Mwandishi wa Habari.
Job Mrema: Na wewe hujasoma habari?
Brenda: Sijasoma.
Job Mrema: Ndugu Shahidi, umewahi kusikia neno Kishoka?
Brenda: Sijawahi kulisikia.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba mtu yeyote anayefanya kazi ya kutoa huduma ya habari na hana sifa ya kutoa huduma hiyo ya habari anakiuka maadili ya utoaji habari hapa nchini?
Brenda: Sijui.
Job Mrema: Ni sahihi sasa kwa majibu yako, unawaeleza Waheshimiwa Majaji kwamba uliokuwa unafanya CHADEMA kazi ya kuhabarisha umma, huhitaji kuwa na sifa za sheria ya habari?
Lissu: Waheshimiwa Majaji, ni sahihi wakili anapiga makelele kwa shouting?
Jaji Ndunguru: Naomba tuamini kwamba ni sauti yake.
Job Mrema: Ni sahihi sasa kwa majibu yako, unawaeleza Waheshimiwa Majaji kwamba uliokuwa unafanya CHADEMA kazi ya kuhabarisha umma, huhitaji kuwa na sifa za sheria ya habari?
Brenda: Siyo sahihi.
Job Mrema: Kama nimekusikia vizuri, Ndugu Shahidi, ulieleza Mahakama hapa kwamba taaluma ya habari siyo requirement katika hiyo idara ya habari?
Brenda: Siyo sahihi.
Job Mrema: Wewe sasa, kama afisa na kama Mkurugenzi wa Mawasiliano usiye na sifa zinazoainishwa katika sheria ya habari...
Brenda: Siyo sahihi.
Job Mrema: (Anapekua kamusi) Utakubaliana na mimi mtu yeyote anayefanya kazi ya kuhabarisha umma asiye kuwa na sifa ni kanjanja?
Brenda: Sifahamu.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, nina shida na hilo. Wakili analeta maneno ya kikabila chao, anataka shahidi anayajue.
Jaji Ndunguru: Ndiyo maana tulitaka arudie.
Job Mrema: Utakubaliana na mimi mtu yeyote anayetoa huduma ya utoaji habari na hana sifa ya utoaji habari kwa mujibu wa sheria, atakuwa hana sifa ya utoaji habari?
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI