Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda aendelea kutoa ushahidi

Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda aendelea kutoa ushahidi

Tukiachana masihara Brenda ni mkali sana...
Pisi ya kwenda ile

Mwehh wewe yule Brenda si Dadako kichama ❗️naww si Chadema au ww CCM kama mm

Nyinyi Chadema yule Dada yenu mumpe Heshima yake🫎🫎❗️
Shida zake zengine ni sisi CCM ndio tutatatua Ebo
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI BRENDA RUPIA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 15.

Job Mrema: Kwa hiyo, kwa maana hiyo, moja ya majukumu yako ni kuhabarisha umma?

Brenda: Ndiyo.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba moja ya sheria inayosimamia masuala ya habari ni Media Services Act?

Brenda: Ni sahihi.

Job Mrema: Na wewe ukiwa kama Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi huwa unaitumia?

Brenda: Huwa inatumika.

Job Mrema: Inatumika na nani?

Brenda: Walio chini yangu na mimi huwa naitumia.

Job Mrema: Wewe umesoma nini?

Brenda: Accounting.

Job Mrema: Nitakuwa sahihi nikisema wewe siyo Mwandishi wa Habari?

Brenda: Mimi siyo Mwandishi wa Habari.

Job Mrema: Na wewe hujasoma habari?

Brenda: Sijasoma.

Job Mrema: Ndugu Shahidi, umewahi kusikia neno Kishoka?

Brenda: Sijawahi kulisikia.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi kwamba mtu yeyote anayefanya kazi ya kutoa huduma ya habari na hana sifa ya kutoa huduma hiyo ya habari anakiuka maadili ya utoaji habari hapa nchini?

Brenda: Sijui.

Job Mrema: Ni sahihi sasa kwa majibu yako, unawaeleza Waheshimiwa Majaji kwamba uliokuwa unafanya CHADEMA kazi ya kuhabarisha umma, huhitaji kuwa na sifa za sheria ya habari?

Lissu: Waheshimiwa Majaji, ni sahihi wakili anapiga makelele kwa shouting?

Jaji Ndunguru: Naomba tuamini kwamba ni sauti yake.

Job Mrema: Ni sahihi sasa kwa majibu yako, unawaeleza Waheshimiwa Majaji kwamba uliokuwa unafanya CHADEMA kazi ya kuhabarisha umma, huhitaji kuwa na sifa za sheria ya habari?

Brenda: Siyo sahihi.

Job Mrema: Kama nimekusikia vizuri, Ndugu Shahidi, ulieleza Mahakama hapa kwamba taaluma ya habari siyo requirement katika hiyo idara ya habari?

Brenda: Siyo sahihi.

Job Mrema: Wewe sasa, kama afisa na kama Mkurugenzi wa Mawasiliano usiye na sifa zinazoainishwa katika sheria ya habari...

Brenda: Siyo sahihi.

Job Mrema: (Anapekua kamusi) Utakubaliana na mimi mtu yeyote anayefanya kazi ya kuhabarisha umma asiye kuwa na sifa ni kanjanja?

Brenda: Sifahamu.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nina shida na hilo. Wakili analeta maneno ya kikabila chao, anataka shahidi anayajue.

Jaji Ndunguru: Ndiyo maana tulitaka arudie.

Job Mrema: Utakubaliana na mimi mtu yeyote anayetoa huduma ya utoaji habari na hana sifa ya utoaji habari kwa mujibu wa sheria, atakuwa hana sifa ya utoaji habari?


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Maswali si hana na pia anataka kumchanganya

Nimegundua kitu kua msomi I mean kwenda darasani

Halafu unatikiwa uwe na uwezo wa kutumia maarifa uliyopata darasani

Naweza kusema watu wanaojinasibu ni wasomi baadhi yao ni weupe mnooo
Anaweza kuwa na akili ila asikwambie mtu kutetea uongo na unajua kabisa huu ni uongo na unataka uwe ukweli ni kitu kigumu sana hapa ndipo Kuna wakati mawakili wanatokea nje ya mstari na Hana jinsi kwasababu ya kutaka maslahi ndio anajikuta afanye hivyo.Moja kati ya kazi ngumu ni kuwa wakili kama umeokoka au unampenda Mungu hii kazi hupaswi kuifanya labda kama ukae kwenye upande wa haki ila reality hela nyingi ipo kwa wasio na haki.
 
Job Mrema: Utakubaliana na mimi mtu yeyote anayetoa huduma ya utoaji habari na hana sifa ya utoaji habari kwa mujibu wa sheria, atakuwa hana sifa ya utoaji habari?
Job Mrema: anauliza swali ambalo jibu lake lipo kwenye ibara ya 18(b) ya katiba.
"Kila mtu anayo haki ya kutafuta, kutoa na kupokea habari bila kujali mipaka ya nchi".
 
Jamani, Manyanza hivi Tawabu jinsia gani.? Kumradhi lakini nataka kujua maana maswali yake nataka kuyapima kwenye ujinsia pia sijamaanisha ujinsia wake ni udhafu wa maarifa yake kwenye uulizaji wa maswali...
Asante
Ni mwanamke Fulani hivi mweusi, nafikiri Kuna page moja Leo imeonyesha video yake akiwa anaingia mahakamani
 
Back
Top Bottom