Kesi ya Sabaya: Ushahidi wa Video za CCTV waonesha shahidi akitoa fedha benki alizomkabidhi Ole Sabaya

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imelazimika kuahirisha kuendelea kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya shahidi wa 10, Francis Mrosso kudai kuwa anajisikia vibaya.

Leo Novemba 24, 2021 shahidi huyo wa Jamhuri alipomaliza kuongozwa kutoa ushahidi wake na Mawakili Waandamizi wa Serikali Tarsila Gervas na Felix Kwetukia aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi kesho.

Shahidi huyo alidai kuwa hali yake siyo nzuri na hajisikii vizuri baada ya kuona ‘clips’ sita za video zikionyesha matukio mbalimbali ya Januari 22, 2021 akiwa Benki ya CRDB tawi la Kwa Mromboo, Arusha alipoenda kutoa Sh90 milioni.

Leo ni siku ya tatu tangu aanze kutoa ushahidi wake kuanzia Novemba 22,2021 shahidi huyo leo alimalizia ushahidi wake ambapo mahakamani hapo iliwekwa flash yenye clip sita kutoka Benki hiyo, zikimuonyesha namna alivyoenda kutoa fedha hizo akiwa na baadhi ya watuhumiwa wenzake Sabaya.

Mrosso ambaye ni mmiliki wa gereji ya Mrosso Injector Pump Service alionekana kuwa kimya wakati video hizo zikionyeshwa kwa vipande vipande mahakamani hapo.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo, shahidi huyo alipomaliza kuongozwa kutoa ushahidi wake aliiomba mahakama impe muda atoke nje kwa dakika chache kabla ya kurejea kuanza kuhojiwa na mawakili wa utetezi, ombi ambalo liliridhiwa na mahakama.

Baada ya kurejea ndani ya chumba cha mahakama hiyo, Mrosso alimuomba Hakimu aahirishe kesi hiyo hadi kesho kwani hajisikii vizuri baada ya kuona matukio hayo kutoka kwenye CCTV Camera yaliyoonyeshwa mahakamani hapo.

“Mheshimiwa Hakimu baada ya kuona matukio haya, hali yangu sijisikii vizuri naomba tuendelee kesho,”alisema Mrosso

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofmed Mtenga aliomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kama alivyoomba shahidi kwa kuieleza mahakama kuwa hayuko sawa baada ya kuona video hizo za Januari 22, 2021.

Hakimu Kisinda aliridhia ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 29, mwaka huu ambapo shahidi huyo ataanza kuhojiwa na mawakili wa utetezi.

Awali akiongozwa na Mawakili hao, shahidi huyo kupitia video hizo aliwatambua washitakiwa watatu ambao ni Enock Mnkeni, John Aweyo na Jackson Macha ambao wanaonekana katika matukio mbalimbali kwenye benki hiyo.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano ambapo kati ya hayo Sabaya peke yake anakabiliwa na makosa matatu,makosa wanayodaiwa kuyatenda Januari 22,2021 jijini Arusha
 
Huyo shahidi aonyeshe akimpa Sabaya pesa. Huo ndio unaweza kuwa ushahidi. Kwa hiyo wote waliotoa pesa siku hiyo walitoa ili kumpa Sabaya?
 
Back
Top Bottom