Kesi ya Mbowe: Yatokanayo, yasipuuziwe

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,854
35,862
Kesi ya Mbowe ingali ikirindima. Hata hivyo tayari kuna ambayo hatukuyajua ambayo leo tunayajua zaidi.

Kumbe pana Makomando wengi wanaweza kuwa walipotea baina 2015 - 2021.

Nani ajuaye huenda wanaendelea kupotea leo.

Hawa ni watanzania, wananchi na binadamu wenzetu wenye haki zao za msingi wanazostahili, zikiwamo za kuishi.

Pana haja ya kufanya sensa ya kujua waliko makomando hawa hasa kwa waliokuwa demobilized. Kujua wako wapi, wanafanya nini na hata kujihusisha katika ustawi wa maisha yao.

Ni muhimu kulinganisha idadi ya waliopotea na waliookotwa kwenye viroba. Hii inaweza kusaidia kutanzua kitendawili kigumu cha utambuzi wa watu hasa wale ambao hawakuweza kutambulika.

IMG_20211202_092804_863.jpg

Ni vyema zoezi hili likafanyika sasa kwani panga pangua siku moja zoezi hili litafanyika.

Zoezi hili ni muhimu likaambatana na fidia stahiki kwa wahanga (zikiwamo adhabu) ikigundulika watumishi wa umma walihusika kwenye kadhia hii.

Mshiriki katika kufichua maovu ni mshirika katika haki.

Mshiriki katika kuficha maovu ni mshirika katika uovu.
 
Wakati wa uchaguzi I think 2015-2016 hapo

Ninarejea kwenye vaults ku refresh. Habari ya ndege hii si ngeni.

Ya akina komando Malema, Urio, Lijenje, Mhina na wenzao yana "shock effects" zenye kuweza kumfanya mtu akapata mtafaruku wa kumbu kumbu.

Hakutabaki jiwe juu ya jingine.
 
Back
Top Bottom