Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,657
- 22,251
Zoezi hilo afanye unayemdhania? Subiri mwendazake atakaporudi.Kesi ya Mbowe ingali ikirindima. Hata hivyo tayari kuna ambayo hatukuyajua ambayo leo tunayajua zaidi.
Kumbe pana Makomando wengi wanaweza kuwa walipotea baina 2015 - 2021.
Nani ajuaye huenda wanaendelea kupotea leo.
Hawa ni watanzania, wananchi na binadamu wenzetu wenye haki zao za msingi wanazostahili, zikiwamo za kuishi.
Pana haja ya kufanya sensa ya kujua waliko makomando hawa hasa kwa waliokuwa demobilized. Kujua wako wapi, wanafanya nini na hata kujihusisha katika ustawi wa maisha yao.
Ni muhimu kulinganisha idadi ya waliopotea na waliookotwa kwenye viroba. Hii inaweza kusaidia kutanzua kitendawili kigumu cha utambuzi wa watu hasa wale ambao hawakuweza kutambulika.
Ni vyema zoezi hili likafanyika sasa kwani panga pangua siku moja zoezi hili litafanyika.
Zoezi hili ni muhimu likaambatana na fidia stahiki kwa wahanga (zikiwamo adhabu) ikigundulika watumishi wa umma walihusika kwenye kadhia hii.
Mshiriki katika kufichua maovu ni mshirika katika haki.
Mshiriki katika kuficha maovu ni mshirika katika uovu.