Kesi ya Mbowe: Yanayoendelea ni taswira ya Uongozi tulionao

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,863
35,872
Alisikika Jaji Mkuu kwenye hafla ya kuapishwa Jaji Siyani:

"Hukumu zenu zizingatie mitizamo ya mihimili mingine."

Tulipo sasa tumemalizana na shahidi ambaye ushahidi wake umepokelewa kama ulivyo. Hii ni pamoja na kukutwa akiwa na maandiko ya chabo yaliyo batili kizimbani.

Huyu ni shahidi anayethibitisha kupokea exhibit (detention register) kutokea mahakamani bila ya yeye kuiomba wala kusaini popote (hali ya kustaabisha).

Exhibit hii anayosema ilikoma kutumika kutokea 12 August 2020, ni yenye kusajili mahabusu kwa jinsi wanavyokuja na kutoka.

Hata hivyo pamoja na kuthibitisha kuwa entries zake hupaswa kufuatana (sequentially) kwa tarehe, kunaonekana:

#392 - Mohammed Ling'wenya 12/8/2020

Wakati entries nyingi nyingine kwa mfano:

#114 kuna mtuhumiwa aliingia 30/7/2021
#156 kuna mtuhumiwa aliingia 3/8/2021

Nk, nk.

Nini maana ya mivurugano hii kutokea kwenye dola, katikati ya haki za watu?

Kwanini njia za kisayansi zilizopo mikononi mwa serikali hazitumiki kuufichua ukweli na kuacha haki kutamalaki?

Au ni kwamba tuna uongozi tu uliodhamiria kuwanyang'anya watu haki zao pasipokuwa na uhalali wowote?

Umoja gani wa taifa lipi unaoweza kutumainiwa wapi katika hali kama hizi?
 
Naskia na leo jaji amekataa pingamizi la utetezi, huko ndiko akili zao wote serikalini zilipohamia, tukipigwa na wajanja wa nishati hata hawana habari.

Hii kesi natangulia mahakama ya rufani kuisubiri, huko mahakama kuu kinachoendelea kwa sasa ni kupotezeana muda tu.
 
Wacha inyeshe tujue panapo vuja.

Baada ya polisi, tiss na bunge kuvuja, mvua hii ya sasa yaonyesha mahakama nayo ikivuja.

Mithali 29:2

[2]Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi;

Bali mwovu atawalapo, watu huugua.
 
Aibu ya Yanayoendelea mahakamani ni zao la fikra za ki CCM, tutawalaumu polisi, TISS na mahakama bure. Ukweli tatizo ni CCM. Polisi wanafikiria ki CCM, TISS ki CCM, Mahakama ki CCM
Katiba na sheria zinakataza watumishi wa uma kujihusisha moja kwa moja au kufanya upendeleo kwa chama fulani cha siasa.
Fikra za msingi za mwananchi yeyote zinatakiwa zianzie hapa kuhusu demokrasia ya vyama vingi.

Maadui wa taifa ni watumishi wa uma wanaotenda kinyume na katiba na wala siyo chama chochote.
 
Yale tuliyokataa na kumwondoa mkoloni mweupe ili tujitawale wenyewe, hadi leo ndio hayo hayo anayotumia huyu mkoloni mweusi kututawala!

Bado tuna safari ndefu sana, kazi iendelee..
 
Katiba na sheria zinakataza watumishi wa uma kujihusisha moja kwa moja au kufanya upendeleo kwa chama fulani cha siasa. Fikra za msingi za mwananchi yeyote zinatakiwa zianzie hapa kuhusu demokrasia ya vyama vingi. Maadui wa taifa ni watumishi wa uma wanaotenda kinyume na katiba na wala siyo chama chochote.

Lakini mkuu serikali iko wapi kuhakikisha haki inatendeka?

Tunachokiona ni mashinikizo kutokea kwa serikali kuona haki inaporwa. Kumbuka hata kuingia mahakamani hakujajakuwa bila misuguano.

Mwenye serikali ana chama. Si ndipo chama mtuhumiwa anapojitumbukiza.
 
Sidhani kama serikali hii wamepungukiwa maarifa mpaka wamfunge Mbowe. Wakimfunga watakuwa wajinga mno kwasababu hilo gereza atakalo fungwa litakuwa sehemu ya Hija kwa watu wote wapenda haki ambao kimsingi kwa asili ya binadamu ndio wengi. Ninacho ona wanamtesa tu na kuwatisha wataka Katiba.
 
Sidhani kama serikali hii wamepungukiwa maarifa mpaka wamfunge Mbowe. Wakimfunga watakuwa wajinga mno kwasababu hilo gereza atakalo fungwa litakuwa sehemu ya Hija kwa watu wote wapenda haki ambao kimsingi kwa asili ya binadamu ndio wengi. Ninacho ona wanamtesa tu na kuwatisha wataka Katiba.
 
Lakini mkuu serikali iko wapi kuhakikisha haki inatendeka?

Tunachokiona ni mashinikizo kutokea kwa serikali kuona haki inaporwa. Kumbuka hata kuingia mahakamani hakujajakuwa bila misuguano ..

Mwenye serikali ana chama. Si ndipo chama mtuhumiwa anapojitumbukiza...
Serikali inaongozwa na wanasiasa (watu wenye tamaa ya madaraka), ndiyo sababu katiba ikaweka katazo la watumishi wa uma ambao siyo wanasiasa kwa mujibu wa ajira zao wasijihusishe na siasa na ikithibitika wafukuzwe kazi na kushitakiwa.

Sasa tatizo lipo kwa wananchi wanaposhindwa kuilinda katiba kwa kuwashughulikia wanaoivunja. Angalizo, katika nchi yoyote kuna wananchi na mapunguani.

Mwananchi ni yule anayefikiria kuhusu raia wengine wa makundi yote pamoja warithi wao wakati punguanini yule anayefikiria kundi au chama chake tu na anaunga mkono mambo yote yanayofanywa na kundi/chama chake yawe ya maana au ya kipuuzi.
 
Rais wa Tanzania yetu hii kwa mujibu wa katiba ni kama Mungu. Akiamua raia yeyote afungwe ama kunyongwa hata kama hana kosa atafungwa/kunyongwa tu
 
Sidhani kama serikali hii wamepungukiwa maarifa mpaka wamfunge Mbowe. Wakimfunga watakuwa wajinga mno kwasababu hilo gereza atakalo fungwa litakuwa sehemu ya Hija kwa watu wote wapenda haki ambao kimsingi kwa asili ya binadamu ndio wengi. Ninacho ona wanamtesa tu na kuwatisha wataka Katiba.
Wakimtesa wanapata faida gani
 
Serikali inaongozwa na wanasiasa (watu wenye tamaa ya madaraka), ndiyo sababu katiba ikaweka katazo la watumishi wa uma ambao siyo wanasiasa kwa mujibu wa ajira zao wasijihusishe na siasa na ikithibitika wafukuzwe kazi na kushitakiwa...
Nina kusoma Kwamba unaitisha vyama vyote vya siasa kuwakabili serikali kwa pamoja. Maana ya kuwa wamepoteza uhalali kwa kushindwa kuizingatia na kuisimamia katiba kinyume cha viapo vyao.

Uthibitisho wako tafadhali.
 
Sidhani kama serikali hii wamepungukiwa maarifa mpaka wamfunge Mbowe. Wakimfunga watakuwa wajinga mno kwasababu hilo gereza atakalo fungwa litakuwa sehemu ya Hija kwa watu wote wapenda haki ambao kimsingi kwa asili ya binadamu ndio wengi. Ninacho ona wanamtesa tu na kuwatisha wataka Katiba.

Kwamba "wanamtesa" kwa uhalali upi?
 
Back
Top Bottom