Kesi ya Mbowe: Watanzania hatuhoji uhalali au uwezo wa Mahakama, bali uwezo wa Majaji - Msimamizi uko wapi- Kwanini mnaichosha Mahakama ya Rufaa?

Hakuna mahakama hapo hilo ni tawi kuu la CCM
 
Uteuzi wa majaji inabidi uangaliwe upya na sifa isiwe urafiki, ukoo, kujuaana, udini na ukabila iwe ni uwezo wa mtu na afanyiwe interview kwenye public
 
Hakuna kesi, ndiyo maana hawajui hata wanachosikiliza na kuhukumu ni kipi...
 
Watuhumiwa wote wanasema maelezo yao yalichukiwa sehemu moja, barua hiyo ingewafanya Jamuhuri walete vithibitisho maana ni kazi yao ku- prove and kudisi-prove na yanayosemwa na watuhumiwa- hii ndio njia pekee ya mahakama kulinda haki za mtumiwa. Mahakama iko pale kulinda haki za watu wote ikiwemo washtakiwa na washtaki
 
Mahakama Kuu Tanzania lindeni hadhi yenu, hii kesi inafuatiliwa na dunia nzima, msije mkajikuta kwenye ranking ya ubora mpo sawa na Somalia pamoja na Afghanistan.
 
Na hili kombola lililolushwa jana na shaidi wa pili wa upande wa utetezi si la kitoto hata kidogo, litampa shida sana jaji na mawakili wa jamuhuri.
Jaji kashidwa kulinda haki ya mshitakiwa, Mshitakiwa katamka wazi hakuwahi kupeledwa Central - Jaji kakataa upande wa Jamhuri kuleta ushahidi wao kuonyesha ni kweli walimfikisha ama hawakumfikisha.

Mahakama haina mzani, na hii ni kitu mbaya sana... kwa hili Jaji umechemka tena saaana.
 
Niwakumbushe Jaji Mkuu Mstaafu alipoenda Ikulu kumuona Rais mwendazake alisema hakuna kitu kinachowapa shida kama vimemo vya maelekezo ya maamuzi ya kesi! Neno hili kwa nchi zenye utawala wa sheria ni zito sana japo sisi lilionekana ni maongezi ya wacheza bao! Jaji anayeapishwa na Rais anawajibika kutoa uamuzi ambao Rais anautaka, vinginevyo acha kazi na utakiona cha mtemakuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…