Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 17,871
- 33,236
Kwenye bandiko hili pale litakapotumika neno Jaji au Majaji ndiyo itajumuisha pia na mahakimu toka mahakama za mwanzo mpaka Mkoa.
Sisi kama Taifa tumerithi mfumo wa kale na maarufu zaidi wa kuwa na serikali ya kijamhuri (Republic). Ndani ya mfumo huo kunakuwa kuna mgawanyo wa kimadaraka kati ya matawi matatu yanayounda serikali, yaani Bunge, Mahakama na Utawala.
Kwa mfumo huo matawi mawil ya Bunge na Utawala huongozwa na wanasiasa wakati tawi la Mahakama huongozwa na Majaji wanaoteuliwa pia na wanasiasa. Kinadharia matawi haya matatu hutakiwa kuwa huru na kila tawi kuwa na uwezo fulani wa kusimamia msawaziko wa tawi Jingine.
Kwa Tanzania inaonekana kuwa Mahakama yetu inaendeshwa zaidi kwa kufuata matakwa ya tawi la Utawala na hata wanasiasa waliomo kwenye tawi la utawala wakati fulani hugoma kutekeleza maamuzi ya Mahakama na mahakama huwa inakaa kimya.
Wengi wetu tuna uzowefu kwamba jambo la kisiasa likipelekwa kwenye mahakama zetu kama liko kinyume na maslahi makubwa na tawi la Utawala ama chama kilichoko madarakani, basi mahakama hushindwa kufanya maamuzi kwa wakati ama ikifanya maamuzi ni lazima yaegemee upande wa Watawala au chama kilichoko madarakani yaani CCM.
Kuanzia uamuzi wa Mgombea binafsi mpaka Ubunge wa Lissu kule Singida Mashariki na sasa kesi ya Wabunge 19 wa CHADEMA, bado mtu wa kawaida kabisa mtaani anashangaa ni kwa nini jambo la wazi kama la hao wabunge linaweza kuchukua zaidi ya miaka 3 kuamuliwa.
Nimeandika makala haya baada ya kusisimuliwa na Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Pakistan kutangaza kwamba kukamatwa kwa kiongozi wa chama cha siasa cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) Imran Khan, kuwa kulikuwa batili.
Yaani Khan kakamatwa Jumanne na leo Mahakama Kuu inatoa uamuzi kwamba kukamatwa kwake ni batili, kwa Tanzania inawezekana kweli? Mahakama zetu linapokuja suala dhidi ya watawala ama CCM huwa haina uwezo wa kufanya maamuzi kwa wakati.