Kesi ya Lema: Lissu amkaanga Profesa Shivji

Kesi ya Lema: Lissu amkaanga Profesa Shivji

sheria si msahafu. Tundu yuko sahihi kuwa mazingira ya kisiasa na ushindani uliopo unasababisha sheria kubadilishwa, na ndio maana kuna marekebisho ya sheria na katiba

Sheria haijabalishwa mkuu. Ila msisitizo umewekwa kwamba mpiga kura afungue kesi endapo haki zake zimepokwa mfano kanyimwa haki ya kupiga kura. Ndivyo nilivyoelewa mimi ninayesoma agriculture
 
Mimi naamini Prof. Shivji ameisoma hukumu na hajanukuliwa vibaya. Huo ndio msimamo wake (maoni yake) juu ya hukumu hiyo.
Kwa gwiji wa sheria kama yeye sidhani kama anaweza kutoa comment nzito kiasi hicho kabla ya kujiridhisha kwa kuisoma hukumu husika.
na yeye ni binadamu na si malaika,huenda shivji alipotoka kidogo. Wapiga kura wawe na haki ya kufungua kesi kwa yale yanayowahusu na si vinginevyo!
 
Tatizo kubwa la Pro-Chadema JF tatizo wamejikita zaidi kiushabiki wa kisiasa akili zao zimeganda Chadema.

Prof Issa Shivji yeye kajikita zaidi kwenye fani yake katafsiri sheria, ajapinga Lema kushinda rufaa yake alichopinga ni mpiga kura kuwa hana haki ya kumshitaki mgombea.

Tundu Lissu hana uwezo wa kupambana na mwalimu wake Prof Shivji.
 
Wenyewe kwenye utetezi wao kule Mahakama Kuu walidai "walijisikia vibaya sana" jinsi Buriani alivyokuwa "akitukanwa". Pengine "kujisikia vibaya" nayo ni kuvunjiwa haki
pia (just through common sense) ila kosa lao walishindwa kuishawishi mahakama ya juu. Kuna haja ya Katiba kuainisha kwa mapana na marefu "WAJIBU NA HAKI ZA MPIGA KURA".

...hapo kwenye "kujisikia vibaya" pamenikumbusha stori moja ya rafiki yangu kutoka DRC...aliniambia huko kwao Kongo ukimpa msichana mimba alfu ukakataa kwamba sio wewe uliyehusika na huo ujauzito kuna-namna wazee wanafanya,siku ya huyo dada atakapokuwa anajifungua basi uchungu wote wa kujifungua unampata huyo aliyeikataa hiyo mimba...
 
Hawa Mwananchi naona wameamua kukomaa na hukumu ya Lema kama habari yao ya wiki ya kuuzia gazeti kwa wiki hii. Sijui wiki ijayo watatoka na heading gani.

Unashangaa nini, wakati HabariLeo wao kwa muda wa wiki mbili mfululizo wanauza gazeti lao kwa habari moja kubwa kuhusu mgogoro wa KKKT.
 
Tatizo kubwa la Pro-Chadema JF tatizo wamejikita zaidi kiushabiki wa kisiasa akili zao zimeganda Chadema.

Prof Issa Shivji yeye kajikita zaidi kwenye fani yake katafsiri sheria, ajapinga Lema kushinda rufaa yake alichopinga ni mpiga kura kuwa hana haki ya kumshitaki mgombea.

Tundu Lissu hana uwezo wa kupambana na mwalimu wake Prof Shivji.

Na lisu hapingi mpiga ukura kushtaki pale haki zake zimepokwa. Sioni ajabu mwanafunzi kumwelimisha mwalimu wake
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Nilisema jana kuwa ama Shivji hakuifuatilia kesi ya Lema kiundani (mazingira) ama gazeti lilimnukuu vibaya!

Sasa Lissu kaweka mambo hadharani!
 
Tatizo kubwa la Pro-Chadema JF tatizo wamejikita zaidi kiushabiki wa kisiasa akili zao zimeganda Chadema.

Prof Issa Shivji yeye kajikita zaidi kwenye fani yake katafsiri sheria, ajapinga Lema kushinda rufaa yake alichopinga ni mpiga kura kuwa hana haki ya kumshitaki mgombea.

Tundu Lissu hana uwezo wa kupambana na mwalimu wake Prof Shivji.

Kwa namna yoyote ile, ili wapigakura wapate kufungua kesi dhidi ya mshindi wa kiti cha Ubunge au Diwani ni lazima waonyeshe kuwa haki zao zimevunjwa na kuathiri mwenendo wa haki zao za kupiga kura au kuchaguliwa na sio vinginevyo.

Sheria haiwezi kutoa haki au hukumu kwa mtu/watu wasiohusika.

Otherwise, wewe RITZ unaleta stupid and unmatured politiks.

Reading and understanding the Court of Appeal Judgment on Lema's case, there is nowhere the bench said that Voters are barred to institute petitions against washindi wa uchaguzi, BUT what the CAT said is LET THE PETITIONERS SHOW VIPI WAMEATHIRIWA.

I endorse the court's judgmnt.
 
Nyani!

Nilikuambia haya jana;hukumu ya Lema HAIJATENGUA maamuzi ya Mahakama Kuu dhidi ya Chadiel Mgonja(Same)ya mwaka 1980 kwani kesi hizi 2 zinawalalamikaji wenye malalamiko tofauti kabisa!

Kesi ya Mgonja ilijikita kwenye haki za mpiga kura Same wa kutopiga kura kwenye uchaguzi wa mwaka 1980 lkn kesi ya Lema wapiga kura hawa walikubali kabisa kuwa walipiga kura kumchagua Mbunge wao lkn wakasema wamefungua kesi kwa sababu Lema alimtukana Mama Batlida!

Hakuna haki yao ya msingi iliyopotea kwa wapiga kura hawa na kesi hii haikuwa ya uchaguzi bali ni ya kashfa na sheria za kesi za kashfa ni yule aliyetukanwa au Jamhuri tu ndiyo wenye haki ya kufungua kesi!

Nina imani kuwa gwiji Shivji alinukuriwa vibaya!
 
Prof ajapata hii hukumu kwa undani, nafikiri akii ipitia yote atabadili mtazamo, halafu mwalimu si Mungu kwamba asi jadiliwe anapopotoka.
 
Japo natumia commonsense zaidi kuliko sheria, lakini maelezo ya Lissu yako more clear kuliko ya Prof. Natamani sana pawekwe live mdahalo juu ya hili kwa ajili ya wananchi kuchuja nani mwenye point kati ya prof na Lissu. Uzuri hawa jamaa wote wawili hawakimbii midahalo kama akina JK na Nape.
 
Tatizo kubwa la Pro-Chadema JF tatizo wamejikita zaidi kiushabiki wa kisiasa akili zao zimeganda Chadema.

Prof Issa Shivji yeye kajikita zaidi kwenye fani yake katafsiri sheria, ajapinga Lema kushinda rufaa yake alichopinga ni mpiga kura kuwa hana haki ya kumshitaki mgombea.

Tundu Lissu hana uwezo wa kupambana na mwalimu wake Prof Shivji.

Si vizuri kuleta ushabiki wako wa kisiasa, hapo Mahakama imeweka 'Obita dicta' ili kupunguza watu kutumiwa ovyo kufungua kesi, aliyetukanwa ni mwingine we kinakuuma nini hadi ushadadie kufungua kesi?!
 
Nikimsoma vizuri Lissu ni kama anaonyesha hiyo sheria ilikuwa inakuwa abused. Kama ni kweli basi mahali pa kuirekebisha ni bungeni na wala sio mahakama kutunga sheria mpya.

Kama waliona hiyo sheria inatumika vibaya, kwanini miaka yote hiyo hawakupendekeza ibadilishwe au ifanyiwe marekebisho bungeni?
 
Chintu,
Kama unajua uhusiano wa serikali, mahakama na bunge basi maelezo ya Lissu yanathibitisha kile alichosema prof. Shivji.

Kilichofanyika sio tafsiri ya sheria bali kusema hii sheria haifai kwahiyo tunaiwekea ukomo. Bahati mbaya hiyo sio kazi ya mahakama na badala yake ni kazi ya bunge.

Japo natumia commonsense zaidi kuliko sheria, lakini maelezo ya Lissu yako more clear kuliko ya Prof. Natamani sana pawekwe live mdahalo juu ya hili kwa ajili ya wananchi kuchuja nani mwenye point kati ya prof na Lissu. Uzuri hawa jamaa wote wawili hawakimbii midahalo kama akina JK na Nape.
 
nafikiri gazeti lilimnukuu profesa shivji vibaya,mahakama haikuzuia mpiga kura kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani ila mpiga kura ni lazima awe specific ni ipi haki yake imekiukwa katika uchaguzi and its clearly stipulated haki zipi ni za mpiga kura
 
Huyo ni Muhindi lazima atetee CCM ni wahindi wachache sana majasiri na huwasikii wakipiga kelele.CCM wanadhani wakimtumia Prof ndiyo nini? Kuna wajuvu zaidi ya Prof wa sheria .
 
Malafyale,
Maelezo ya Lissu ndio yanathibitisha kabisa kwamba kilichofanyika sio tafsiri ya sheria bali kutengeneza sheria mpya.

Kama wangeona sheria ya mwaka 1985 ina makosa au inakiuka katiba basi wangelisema hivyo. Ila kusema sheria inakuwa abused kwahiyo tunaifuta au tunaiwekea ukomo sio kazi ya mahakama, hiyo ni kazi ya bunge.

Nyani!

Nilikuambia haya jana;hukumu ya Lema HAIJATENGUA maamuzi ya Mahakama Kuu dhidi ya Chadiel Mgonja(Same)ya mwaka 1980 kwani kesi hizi 2 zinawalalamikaji wenye malalamiko tofauti kabisa!

Kesi ya Mgonja ilijikita kwenye haki za mpiga kura Same wa kutopiga kura kwenye uchaguzi wa mwaka 1980 lkn kesi ya Lema wapiga kura hawa walikubali kabisa kuwa walipiga kura kumchagua Mbunge wao lkn wakasema wamefungua kesi kwa sababu Lema alimtukana Mama Batlida!

Hakuna haki yao ya msingi iliyopotea kwa wapiga kura hawa na kesi hii haikuwa ya uchaguzi bali ni ya kashfa na sheria za kesi za kashfa ni yule aliyetukanwa au Jamhuri tu ndiyo wenye haki ya kufungua kesi!

Nina imani kuwa gwiji Shivji alinukuriwa vibaya!
 
Bado naamini ama Shivji hajaisoma hukumu au hakunukuliwa sahihi. Lakini ikiwezekana basi waitwe magwiji hao kwenye mdahalo, si lazima iwe juu ya kesi ya Lema, lakini inaweza kuwa kama case study pamoja na masuala mengine.

Lakini kwa kweli kwa namna ambavyo jana watu wengi walimsoma Shivji, hata layman wa sheria, mlakini anaweza kuchakata mawazo yake vizuri, itakuwa ngumu kukubaliana naye, hata kama baadhi yao, nikiwemo mimi binafsi, tunampenda na kumuamini kweli profesa.
Prof.Shivj kanunuliwa na CCM.Haiji akilini prof.mwenye weledi kama huyu kukurupuka kutoa hoja pasipo kuisoma hukumu hiyo. KWA HAKIKA KATUMWA, na ametumika vibaya. Atapoteza heshima yake. Awaache CCM walipe gharama za kesi,zigo hilo lao CCM.
 
Karl Popper and Thomas Kuhn at work! Waacheni wabishane ila sikuhizi mwanafunzi anaweza kumzidi mwalimu wake.
 
Tatizo kubwa la Pro-Chadema JF tatizo wamejikita zaidi kiushabiki wa kisiasa akili zao zimeganda Chadema.

Prof Issa Shivji yeye kajikita zaidi kwenye fani yake katafsiri sheria, ajapinga Lema kushinda rufaa yake alichopinga ni mpiga kura kuwa hana haki ya kumshitaki mgombea.

Tundu Lissu hana uwezo wa kupambana na mwalimu wake Prof Shivji.
Hujajua historia, Isaac Newton alifanya nini kwenye mtihani wake uliozua utata?
Labda JK hamwezi mwalim wake Rey C kwenye.......
 
Back
Top Bottom