Kesi ya Lema: Lissu amkaanga Profesa Shivji

Kesi ya Lema: Lissu amkaanga Profesa Shivji

Haki ya mwananchi ipo ya kupinga matokeo lkn iwe inadirect effects kwake mfano kuzuiwa kupiga kura,kura kuibiwa,kura kutoesabiwa,kulazimishwa kupiga kura kwa mtu fulani. Lakini mambo binafsi ya wogembea ambayo hayana effects kwa mpiga kura hayawezi kumvuwa ubunge,udiwani,urais mshindi,Hivyo prof.shvji amekosea pamoja na heshima aliyojiwekea kwenye tasinia ya sheria.
 
Hiyo ni kumjibu ya tafsiri yako hafifu..! Hakuna sehemu amesema taaluma iwekwe pembeni..! Mkiambiwa sheria ngumu mnabisha

kwenye mwananch leo pg 4 para 7 imeandikwa hiv ... INATOKANA NA MSOMI HUYO KUZUNGUMZA KITAALAMU BILA KUANGALIA MAZINGIRA HALISI YA SIASA ZA TZ. mkuu siitaj kusomea sheria kuelewa hapo
 
Mimi si mwanasheri lakini nakubaliana na Mahakama ya rufani kwamba wapiga kura walete kesi kama tu haki zao zimekiukwa basi , lakini wasifungue kesi kwa niaba ya wagombea , kama Katukanwa Buriani wewe Musa Mkanga unahusika vipi ? Je haki yako ipi iliyovunjwa ? Kwa nini mwenyewe Burian hakufungua kesi ? Katika hili Cdm hakikisheni zile gharama za za kesi zinalipwa kwa wakati , ili kukomesha hawa vimbelembele .
 
Hakuna haki isiyokuwa na kikomo. Prof. Shivji na Stola wasijifanye kutojua mazingaombwe yanayofanywa na ccm kupitia kwa the so called wananchi.

“Kwenye rufaa ya kwanza mahakama inaruhusiwa kuibua chochote, sasa hizo ni hoja zinazotolewa na watu ambao marafiki zao wa CCM wameshindwa sasa wanavaa joho la utaalamu kutoa hoja kama hizi zisizo na mashiko.”
 
Nimeipenda sana hii,LIssu ameamua kumchana mwalimu wake live bila chenga!
hapa je hujapapenda "Kwenye rufaa ya kwanza mahakama inaruhusiwa kuibua chochote, sasa hizo ni hoja zinazotolewa na watu ambao marafiki zao wa CCM wameshindwa sasa wanavaa joho la utaalamu kutoa hoja kama hizi zisizo na mashiko."
 
Nafikiri prof. Shivji somehow yuko sahihi, hasa kwa kuiangalia sheria (tukiweka pembeni suala la mazingira ya siasa za Tanzania) Hapa chakuangalia ni namna sheria hii inaweza kuangaliwa upya ili kuzuia watu kutumia haki hii kutumika na wanasiasa wachache wenye fedha kuvuruga wabunge waliochaguliwa na wananchi.
 
Mijadala mingine ni ya kitaalamu sana. Tunapenda kujua zaidi na kwa undani sana, ila haya yatapatikana iwapo sisi mamuma wa sheria, tutawaachia magwiji, wapambane kisheria, nasi tuwe wasikilizaji tu. Cha kusikitisha ni pale mfuatano wa uzi huu unapoingiliwa na ushabiki wa vyama bila hata point za kisheria. Wale mamuma, hapa tusome tu, tusi-comment!!!!

Mkuu hekima na werevu vimekuwepo kwa kuwa kuna ujinga/upumbavu (umaamuma). Wacha maamuma nao wajichangache; usiwazuie, pumba na mchele vitajitenga vyenyewe.
 
hapa je hujapapenda "Kwenye rufaa ya kwanza mahakama inaruhusiwa kuibua chochote, sasa hizo ni hoja zinazotolewa na watu ambao marafiki zao wa CCM wameshindwa sasa wanavaa joho la utaalamu kutoa hoja kama hizi zisizo na mashiko."
Mkuu huu mstari pia umetulia kinoma,wataalamu wetu wakati mwingine wanatukuza sana unafiki!
 
Mangaline pamoja sana..sisi tusiojua sheria tusijifanye kujua tufatilie tupate kuelewa..
 
Last edited by a moderator:
Hakuna asiyejua Rais wa TLS Francis Sitola ni mwanachama mtiifu wa CCM na kadi anayo.Tundu Lissu amempasha bila kumuogopa.Ni wazi katumwa na CCM kuongea ujinga aliiongea
 
Mimi si mwanasheri lakini nakubaliana na Mahakama ya rufani kwamba wapiga kura walete kesi kama tu haki zao zimekiukwa basi , lakini wasifungue kesi kwa niaba ya wagombea , kama Katukanwa Buriani wewe Musa Mkanga unahusika vipi ? Je haki yako ipi iliyovunjwa ? Kwa nini mwenyewe Burian hakufungua kesi ? Katika hili Cdm hakikisheni zile gharama za za kesi zinalipwa kwa wakati , ili kukomesha hawa vimbelembele .

Wenyewe kwenye utetezi wao kule Mahakama Kuu walidai "walijisikia vibaya sana" jinsi Buriani alivyokuwa "akitukanwa". Pengine "kujisikia vibaya" nayo ni kuvunjiwa haki
pia (just through common sense) ila kosa lao walishindwa kuishawishi mahakama ya juu. Kuna haja ya Katiba kuainisha kwa mapana na marefu "WAJIBU NA HAKI ZA MPIGA KURA".
 
Ukiona mwalimu na mwanafunzi wabishana, ujue.....

Mwalimu anakuwa mwalimu pale tu anapokuwa anakuongoza kitaaluma darasani. Kimantinki, kwa wakati huo yeye hujua mambo mengi kuliko mwanafunzi wake...Ikishapita miaka mingi, uwezo wa mwanafunzi katika kuelewa mambo unaweza ukawa mkubwa zaidi ya mwalimu wake ....Ukiendelea kusoma, kutafiti, na kupractise unazidi kuelimika...na unaweza kuwa Manju Mkuu zaidi ya mwalimu wako wa kipindi kile. Tena kwenye masuala ya sheria!! aaaah, Sheria haina mwenyewe bana...
 
Jamani, labda kwa shivji kwa sababu amezoea tu kupata headlines, lakini kwa sitola Francis tunamjua kuwa ni pandikizi, ni usalama wa taifa ndio maana badala ya kufanyia kazi issue ya msingi kabisa ya majaji wasiona sifa waliowekwa na JK kupoka haki za mtanzania, yuko kwenye commentary ya kazi ha heshima iliyofanywa na majaji waliobobea, kwanza hawa sio wataalamu wa haki za binadamu wasomi, tukiwataka hao mwananchi wamtafute prof chris peter au advocate Tom Nyanduga hawa wachumbia matumbo wanyamaze
 
kwenye mwananch leo pg 4 para 7 imeandikwa hiv ... INATOKANA NA MSOMI HUYO KUZUNGUMZA KITAALAMU BILA KUANGALIA MAZINGIRA HALISI YA SIASA ZA TZ. mkuu siitaj kusomea sheria kuelewa hapo
Na mimi ndo nilikuwa nakutafasiria hapo hapo kuwa haina maana kuwa taaluma iwekwe pembeni bali taaluma hiyo itumike sanjari na mazingira yaliyopo.! Have I made myself clear?
 
prof watanzania tunakuamini sana katika utetezi wa haki siamini kama ni faraja kwa wabunge kuwa wanaenguliwa tena wabunge wa wanyonge kwa maslahi ya mafisadi wachache kwa kesi za kutengeneza zinazoratibiwa na wenyewe huku spika zao wakitumiwa wanyonge pia kama MICROPHONE huku sisi tulio wengi tukiangamia kukoswa watetezi
swali langu sheria hii hata kama ipo prof inakufurahisha na haina maana ikarekebishwa ama kukataliwa na mahakama?
 
mbobevu wa sheria lisu anasema hoja ya prof shivji inazingatia zaid taaluma inavyotaka na haizingatii mazngira ya siasa za bongo. kwamba kwa mambo yanavyoenda bongo taaluma iwekwe pemben isizingatiwe? ajabu
Hii ajabu haiishindi ile ya washitaki kutowajua mawakili wao ambao wamewatafuta Dar es salaam ambako hawajawahi kufika na wanawalipa mamilioni wakati hata kununua viatu vyao wenyewe hawawezi. hayo ndiyo mazingira yanayostahili kuzingatiwa. tafakari!
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Kuwa mkubwa siyo sabab ya wewe kujua kila kitu! Wakati mwingine mwanafunzi wako anaweza kuwa na ufahamu kupita wewe(mwlm)! Sawa na Lisu kwa Shivji, naona huyu mzee anaelekea kuzeeka vibaya!
 
Back
Top Bottom