Kesi ya Lema: Lissu amkaanga Profesa Shivji

Kesi ya Lema: Lissu amkaanga Profesa Shivji

mbobevu wa sheria lisu anasema hoja ya prof shivji inazingatia zaid taaluma inavyotaka na haizingatii mazngira ya siasa za bongo. Kwamba kwa mambo yanavyoenda bongo taaluma. Iwekwe pemben isizingatiwe? Ajabu

ulitaka amtukane hadharani mwalimu wake....tafuta tafsiri sahihi ya wasomi wa sheria utajua lissu na shivji ni akina nani ktk jamii
 
Nimefurahishwa na kitendo cha Shivji na Rais wa TLS kutoa mawazo yao juu ya hukumu ya rufaa ya Lema hivi ndivyo wasomi wanavyotakiwa kufanya kutoa mchango wao pale wanapoona mambo yanaharibika lakini mbona hatujawasikia wakati lilipoibuliwa swala la majaji wasio na sifa huyo Rais wa TLS alilizungumzia kidogo wakati ile ndio ilikuwa nafasi yake kuonyesha namna gani wanasimamia sheria nchini kwa kifupi aache unafiki akijifanya ana uchungu wakati anaacha mambo mazito yanapita bila kuhoji
Nakubaliana na wewe kwenye ishu ya majaji walimuachia lissu peke yake na kuifanya kuonekana ni suala lakisiasa
 
Mijadala mingine ni ya kitaalamu sana. Tunapenda kujua zaidi na kwa undani sana, ila haya yatapatikana iwapo sisi mamuma wa sheria, tutawaachia magwiji, wapambane kisheria, nasi tuwe wasikilizaji tu. Cha kusikitisha ni pale mfuatano wa uzi huu unapoingiliwa na ushabiki wa vyama bila hata point za kisheria. Wale mamuma, hapa tusome tu, tusi-comment!!!!

Aah wapi. Mkondo wa sheria umekamilika sasa kila mwenye uwezo wa kufikiri anaruhusiwa kutoa mawazo yake. Kuwa mamuma sio utetezi:glasses-nerdy:
 
mbobevu wa sheria lisu anasema hoja ya prof shivji inazingatia zaid taaluma inavyotaka na haizingatii mazngira ya siasa za bongo. kwamba kwa mambo yanavyoenda bongo taaluma iwekwe pemben isizingatiwe? ajabu

Hapana Mheshimiwa, nadhani Tundu Lissu anataka kuweka balance kati ya Taaluma na Mazingira. Ukisoma hoja zake anajaribu pia kutoa ushahidi kwa baadhi ya kesi, kwamba hata mwananchi mwenyewe anayefungua kesi akiulizwa anadai nini huenda hajui, na hapo ndipo kwenye hoja yake ya kusema kuwa kundi kubwa la wanacnhi hao wanatumiwa. Lakini kama mwananchi huyo ana issue ambayo kweli ni haki yake, nadhani Tundu Lissu hana kipingamizi. Kumbe tahadhari anayotoa ni kwamba, kwa nchi kama Tanzania, ni vyema kuweka balance kati ya taaluma zetu na mazingira, ili tuweze kutoa hukumu sahihi !
 
mbobevu wa sheria lisu anasema hoja ya prof shivji inazingatia zaid taaluma inavyotaka na haizingatii mazngira ya siasa za bongo. kwamba kwa mambo yanavyoenda bongo taaluma iwekwe pemben isizingatiwe? ajabu
Frank,

Kama umesoma then husaidii nchi yako then unacheti na ulidesa.


Kwa haraka nimeelewa kuwa wananchi wana haki ya kupinga matokeo pale haki zao - kuwezeshwa na kupiga kura, kuhesabiwa kura na kupata matokeo zinapokiukwa. Suala la nani zimemtosha au la ni la wagombea. Ukimsikia mtu katukana ni kosa la jinai na jamhuri ndo inashitaki.


Sio mwanasheria ila ndo nimeelewa hivo
 
Japo natumia commonsense zaidi kuliko sheria, lakini maelezo ya Lissu yako more clear kuliko ya Prof. Natamani sana pawekwe live mdahalo juu ya hili kwa ajili ya wananchi kuchuja nani mwenye point kati ya prof na Lissu. Uzuri hawa jamaa wote wawili hawakimbii midahalo kama akina JK na Nape.

Hakuna haja ya kuweka mpambano kati ya Lissu na Prof. Shivji.

Hao wote wanajenga nyumba moja ya sheria and for lawyers and legal arena, at large, this must be a very challenging moment.

Kesi ya LEMA must be read, understood and assessed legally not by using macho ya siasa.

I endorse the CAT's findings and Judgment, over.
 
Sheria haijabalishwa mkuu. Ila msisitizo umewekwa kwamba mpiga kura afungue kesi endapo haki zake zimepokwa mfano kanyimwa haki ya kupiga kura. Ndivyo nilivyoelewa mimi ninayesoma agriculture


Huu mjadala wa hii sheria bado haueleweki, especially in the context ya kesi ya Lema. Naona kama upo nje ya point. Kama nakumbuka vizuri, sababu za kukata rufaa kesi ya Lema haikuwa about haki za mpiga kura bali uhamuzi wakijaji hakuwa sahihi kisheria. Sasa imefikaje huku?

Kwa kuongezea tu, inge make sense kama Shivji angetoa ufafanuzi kuhusu haki za mpiga kura in line na mahamuzi haya ya mahakama na kisha, on haki za mpiga kura kama mpiga kura kisheria, bila kuzingatia mazingira anayoyaelezea Lissu.

Kisha aeleze kuna haki gani ya mpiga kura inayokuwa violeted kama mgombea mmoja ataonyesha some misconducts against mgombea mwenzake.

Je mpiga kura huyu anastahiki yoyote katika hili mpaka apinge ushindi wa mbunge, na anashitaki kwa faida ya nani?

Je huyu mpiga kura anashitaki kupinga ushindi au anashitaki misconduct ya mgombea in which case ushindi wa mgombea hauathiriki?

Je upi ni ukomo wa mahakama ya rufaa katika kutoa tafsiri ya haki ya mpiga kura inayolalamikiwa na Shivji?, ikiwa sheria yenyewe haiko wazi kueleza kinagaubaga mazingira ya kesi husika?
 
Katika wasomi wa nchi hii ambaye nilimwona ni mtu ambae anazungumza 'facts' na yuko 'objective' na nilimwamini sana ni Prof. Shivji. Ila kwa siku za karibuni naamini amekengeuka sana na ni msomi ambae chochote atakachokisema lazima nikiangalie kwa jicho la tatu. Alinishangaza pale aliposema eti katiba mpya ya Zanzibar ile iliyounda Serikali ya Umoja huko Zanzibar na kutengeneza nchi ndani ya nchi iko sahihi na haiatarishi muungano. Nawashangaa wale wanaomtetea (akiwemo Lisu) eti hakuisoma hukumu ya Lema au kanukuliwa vibaya, naamini Pro. Shivji siku hizi kapiga teke utaalamu wake na yuko very skewed/subjective. Msikilize kwenye ishu za Muungano kwenye katiba mpya ndo utagundua hili.

Kuhusu kesi ya Lema, nilifuatilia. Nilifuatilia aliyekuwa anamwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali alichokisema kuhusu sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1995 kuhusu lugha isiyofaa kwenye kampeni za uchaguzi. Alisema sheria hiyo haiharamishi lugha zisizofaa kwenye kampeni ... alisema wabunge waliruhusu lugha izo zinazoonekana hazifai ziendelee kutumika sababu wanapenda kutukanana na ndo maana walitunga hiyo sheria hivyo. Kwa kuwa wajibu rufani hawakupinga ushahidi huu, naamini hiyo sheria iko hivyo.

Majaji waliamua kutoa hukumu kwa kuangalia uhalali wa wapiga kura kufungua kesi ambayo wao (wapiga kura) hawakuathirika na wala haki yao haikunyang'ang'anywa na kwa vyovyote vile ata yule aliebaguliwa/kutolewa lugha chafu (Dada yete; Batilda Burian) hakuathirika na ndo maana hakuona haja ya kulalamika mahakamani au popote pale wakati kampeni zinaendelea. Mbona hata kwa Simple Logic inaonesha haki imetendeka. Mimi si mwanasheria, ila kama wachangiaji wanavyosema (Lisu akiwemo), sheria sio swala la kishule tu, ni zaidi ya shule na mimi naongezea "Sheria haikaririwi" kama mtu anavyoweza kukariri kanuni nyingine za Kisayansi, Prof. Shivji na huyo Stola wametokota.

Ingependeza kama Dada yetu Batilda ndo angefungua kesi ya kudhalilishwa na naamini ingekuwa ni kesi ya madai tu aitake Mahakama imwamuru Lema amwombe radhi au amplipe fidia ambayo angeisi ingetibu majeraha ya lungu isiyofaa aliyotolewa (kama ipo na ingedhibitika hivyo pasi kuacha shaka) ukizingatia ushahidi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye kesi hii hii ya Lema. Kama ni kuvunja katiba, basi hao waliotunga sheria ya uchaguzi ya mwaka 1995 na kuruhusu lugha zisizofaa ndo walivunja hiyo katiba ibara ya 26(2) kwa kuhalilisha uvunjaji wa sheria. Nina wasiwasi sana na moni ya Prof. Shivji wa siku hizi
 
Hapana mkuu nimefurahi walivyofuatilia habari hii kwa kina na naamini hawataishia hapo!

Kama wangekuwa na muendelezo huu kwenye habari nyeti kama ufisadi pengine yangekuwepo mabadiliko makubwa.

Kuhusu Prof Shivji naamini hajaisoma hukumu na hakuelewa mazingira ya kesi ndio maana amedhani haki ya mpiga kura imekiukwa!

kufikiri kuwa profesa shivji anaweza kutoa maoni bila kupitia kwanza hoja husika kunatia mashaka umakini wa wasomi wetu katika masuala nyeti yanayogusa maslahi ya wananchi moja kwa moja. ikiwa ni kweli kuwa hivyo ndivyo ilivyotokea basi ninamuomba yeye pamoja na wasomi wenzake na watu wengine mashuhuri wawe wepesi wa kusikia lakini wasiwe wepesi wa kusema au kujibu kabla hawajaelewa vema wanachotakiwa kusema au kujibu. ni kwa manufaa ya wengi.
 
Tukumbuke ubongo pia unazeeka tusitoe maoni kwa JAZBA:A S angry:
 
Nchi hii ina wasomi na wasomi uchwala. huwezi kumwita mtu msomi wakati ni mwepesi wa kulopoka kuliko kufikili
 
2+2=4. inakuwaje katika sheria mwingine anasema ni 3 na mwingine 5. na je cc tusiowanasheria tutapata hak zet kwel mahakaman?
 
Huu ndio uzuri wa sheria, sio kama maths 3 + 3 = 6. Kila mara kutokeapo matatizo, wanasheria hubishana kwa hoja based on tafsiri. Naona hii ni changamoto kwa katiba mpya kuweka mipaka ya mpiga kura
 
Shivji hajasoma hukumu. Aibu hii imempata coz amekurupuka. Kama si kukurupuka basi anatumika na magambaya au hajasoma hukumu husika.”[/SIZE][/FONT]

Jana Wakili wa Lema, Tundu Lissu, alimkosoa Profesa Shivji pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Francis Stolla akisema wanasheria hao wamepotoka katika matamshi yao ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Rufani.

Matamshi ya Shivji pia yaliiteka mijadala katika mitandao ya kijamii ya Jamii Forums, Mabadiliko na Facebook ambako wachangiaji walikuwa wakivutana huku baadhi yao wakisema wazi kwamba msomi huyo amekosea huku wengine wakimtetea kwamba yuko sahihi.

Akizungumza na gazeti hili jana kutoka Songea mkoani Ruvuma, Lissu alipinga vikali hoja zilizotolewa na Profesa Shivji pamoja na Stolla, akisema kuwa hazina mashiko na zinaweza kutolewa tu na mtu ambaye hakufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.

Juzi Profesa Shivji na Stolla walinukuliwa wakiikosoa hukumu ya Mahakama ya Rufani, iliyomrejesha bungeni Lema wakisema hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu Salum Massati, Bernard Luanda na kiongozi wao Nathalia Kimaro, inapingana na sheria.

Lissu katika maelezo yake alisema uamuzi wa mahakama katika kesi ya Lema umejenga upya msingi bora wa matumizi ya vyombo vya uamuzi, kwani kesi nyingi za kupinga matokeo ya ubunge, zimekuwa zikifunguliwa na watu ambao wamekuwa wakitumwa na vigogo wa kisiasa na watu wenye fedha.

Akizungumza na Mwananchi, Lissu alisema hoja hizo hazina mashiko na kuwa ile iliyotolewa na Profesa Shivji inatokana na msomi huyo kuzungumza kitaalamu bila kuangalia mazingira halisi ya siasa za Kitanzania.

Lissu alisema mahakama ya rufani haikupiga marufuku wapiga kura kufungua kesi za kupinga ila iliwataka tu kufanya hivyo pale haki zao zinapokiukwa.

“Kwanza siyo kweli kwamba mahakama imepiga marufuku wapiga kura kufungua kesi, ilisema watafanya hivyo pale ambapo haki zao zimevunjwa, haki zenyewe ni kupiga kura, kura zao kutohesabiwa ama suala jingine litakalomnyima kupiga kura, hizo ndiyo haki za mpiga kura,” alisema na kuongeza:

“Sasa mwalimu wangu, Profesa Shivji yeye anatazama tu kwa jicho la kitaalamu na kusema haki za binadamu zimekiukwa, kwa muda wanasiasa, matajiri na CCM wamekuwa wakiwatumia wananchi kuwapinga wabunge wa upinzani.”

Uchambuzi wa Lissu
Alitoa mfano akisema katika uchaguzi wa 1995, Dk Willibrod Slaa alishinda ubunge na watu wanaojiita wananchi walifungua kesi kupinga ushindi huo, mwaka 2000 wakampinga tena na hata 2005.

Alisema 1995 Makongoro Nyerere aliposhinda ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini kupitia NCCR- Mageuzi, watu wanaojiita wananchi walifungua kesi ambayo matokeo yake yalikuwa mbunge huyo kupoteza kiti chake.

Lissu alisema 2005 aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Marehemu Chacha Wangwe alifunguliwa kesi na watu waliojiita wananchi ambao mwisho wake walishindwa.

“Hawa wananchi ambao wanafungua kesi zenye mawakili wanaolipwa mamilioni ya fedha ni watu ambao hata fedha za kununua viatu hawana, hawa waliokuwa wakimpinga Marehemu Wangwe nikiwa mahakamani niliwauliza kama wanawajua mawakili waliokuwa wanawatetea, walikuwa hawawajui.

Nikawauliza kama wamewahi kufika Dar es Salaam wakasema hapana, sasa sijui waliwapataje wale mawakili,” alisema na kuongeza:

“Wote hawa wanakuwa ni watu wanaotumiwa. Mwaka huu kati ya wabunge wote 25 Chadema tulioshinda, 14 tulifunguliwa kesi na kati ya hizi 12 zimefunguliwa na watu wanaojiita wananchi, hii ni kutumiwa,” alisema.

Alisema mara baada ya uchaguzi mwaka 2010 aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, aliandika waraka kuwataka makatibu wa chama hicho kufungua kesi kwa majimbo yote ambayo chama hicho kiliangushwa jambo alilosema ndilo liliwasukuma kuwatumia wananchi.

Kuhusu hoja kuwa mahakama hiyo ya rufani imeingilia kazi ya kutunga sheria badala ya kuzitafsiri na kuwa imepingana na sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Chediel Mgonja ya mwaka 1980, Lissu alisema hazina mashiko.

“Hiyo ni hoja ya kipuuzi. Hiyo sheria ya kuwa mwananchi yeyote ana haki ya kufungua kesi kuwa imetenguliwa na Mahakama ya Rufani, hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria ukimuuliza atakwambia kuwa, amri ya Mahakama Kuu wala ya Mahakama ya Rufani yenyewe haiwezi kuizuia mahakama hiyo ya juu kabisa nchini kufanya uamuzi wake,” alisema.

Akizungumzia hoja ya Stolla kwamba mahakama iliibua jambo jipya la kuhoji kama wajibu rufani walikuwa wapiga kura ama la, alisema Rais wake huyo hana hoja, kwani wakili wa walalamikaji aliibua hoja kama hiyo na alipoulizwa na mmoja wa majaji kuwa “Hata sisi hatuwezi kulizungumzia suala hili, alishindwa kujibu akawa anajikanyaga tu,” alisema.


Aliongeza: “Kwenye rufaa ya kwanza mahakama inaruhusiwa kuibua chochote, sasa hizo ni hoja zinazotolewa na watu ambao marafiki zao wa CCM wameshindwa sasa wanavaa joho la utaalamu kutoa hoja kama hizi zisizo na mashiko.”

Shivji na Stolla

Profesa Shivji kwa upande wake alieleza kushangazwa na maelezo ya Mahakama ya Rufani kuwa mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na kusema hiyo ni sawa na kutunga sheria mpya na si kutafsiri zilizopo.

“Sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja (Chediel ya mwaka 1980), vinampa haki mpiga kura kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Sijaona hoja nzito ya Mahakama ya kufuta haki hiyo ya mpiga kura,” alisema Profesa Shivji.

Kwa upande wake, Stolla alisema: “Nimesikiliza hata maoni ya wanasheria mbalimbali wakizungumzia kutopendezwa na tafsiri ya Mahakama ya Rufani kuhusu haki ya mpiga kura ‘ku-challenge’ (kupinga) matokeo ya uchaguzi mahakamani.

Aliongeza: “Katika uamuzi wa kisheria, inaonekana Mahakama imetunga sheria mpya na wengi tunajiuliza kama siyo, ni sababu gani nyingine inampa haki mpiga kura kupinga matokeo?”

Stolla alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi ya tangu mwaka 1985, ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, kabla ya kutungwa upya mwaka 2005, inampa haki mpiga kura kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

Kesi ya Lema
Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, mwaka huu kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake.

Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake alikuwa akitumia lugha ya matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa wadhifa huo kwa tiketi ya CCM, Dk Batilda Buriani.

Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila ilimtia hatiani kwa kutumia lugha ya matusi na kutengua matokeo yaliyompa ushindi.

Hata hivyo, alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupitia kwa mawakili wake, Method Kimomogoro na Tundu Lissu ambayo Desemba 21, mwaka huu ilimrejesha tena bungeni baada ya kukubali rufaa yake.

Katika uamuzi wake, Mahakama hiyo ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni masilahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba na kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au masilahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.

CHANZO: Gazeti la Mwananchi | Dec 29, 2012[/QUOTE]
 
Prof Shivji amekosea. Mhakama ya Rufaa haijatunga sheria mpya. Mngoja na Lema siyo sheria, bali ni rulings. Rulings zinaset prescedents ambazo zinaweza kuwa invoked katika litigation zinazofuata.

Kwa sasa, Lema imeistaafisha Mgonja hadi hapo mahakama ya juu zaidi ya ile ya Rufaa (EA au Commonwealth).
 


1. “Lissu katika maelezo yake alisema uamuzi wa mahakama katika kesi ya Lema umejenga upya msingi bora wa matumizi ya vyombo vya uamuzi, kwani kesi nyingi za kupinga matokeo ya ubunge, zimekuwa zikifunguliwa na watu ambao wamekuwa wakitumwa na vigogo wa kisiasa na watu wenye fedha.” GAZETI LA MWANANCHI – 28 DECEMBER 2012
2.“Kwa mtazamo huo huo, tunathibitisha pasipo shaka kuwa Kesi ya Mgonja ilihukumiwa kinyume, ilitoa tafsiri potofu ya ‘hoja yamsingi ya uwepo wa kesi ya kujibu. Tunasema hivyo kwa kuwa hatufikirii kwamba Mahakama iliruhusu kila mpiga kura yeyote bila kuzingatia mahalialipojindikisha na kupiga kura anaweza kupinga matokeo yauchaguzi wowote, wa jimbo lolote mahakamani katika nchi hii.Utakuwa ni ujinga.”
Sehemu ya hukumu kama ilivyotolewa Dar es Salaam, tarehe 19, Decemba, 2012. Mbele ya Jaji, N.P Kimaro, B.M Luanda na S.A. MASATTI.

3.KESI YA UBUNGE YA GWIJI LA SIASA ZA UPARE “EARLY 60’S – EARLY 80’S MAREHEMU CHEDIEL YOHANA MGONJA, KAMA ILIVYOFUNGULIWA DHIDI YAKE NA WAPIGA KURA ATHINIELI AHIYA NA WILLIAM BAKARI, HUKU MGONJA AKISHINDA MAHAKAMA KUU ARUSHA NA BAADAYE KUTENGULIWA NA MAHAKAMA YA RUFAA DAR-ES-SALAAM NDICHO WAKILI MAKINI MNO HON. TUNDU LISSU ANACHOMAANISHA HAPO NO 1 JUU - UNDERLINED. KWA WALE “PLAYERS” KATIKA KESI YA MGONJA AMBAO BADO WAKO HAI NA WAKWELI, LEO MAHAKAMA YA RUFAA TANZANIA IMEMPA HAKI YA UBUNGE LATE HON.CHEDIEL MGONJA AKIWA KABURINI , LAKINI PIA KIJANA HON. GODBLESS LEMA. HAKI YA MTU HAIPOTEI NA MWENYEZI MUNGU KAITOA MBELE YA WATESI WA MGONJA AMBAO BADO WANAISHI. KWA KUMBUKUMBU ZANGU NA RECORD HAPA, WALIOKUWA NYUMA YA WAPIGA KURA WAWILI HAWA KUMPINGA MGONJA WALIKUWA NI AKINA CLEOPA MSUYA, MGAYA WA ELEPHANT MOTEL ENZI ZAKE, MAREHEMU JUDGE NASORO MZAVAS, MAREHEMU SAMMY MDEE, PETER KISUMO,NICODEMUS BANDUKA NA BAADHI YA WAPARE MATAJIRI NA TATIZO LENYEWE LILIKUWA “UWAZIRI MKUU WA TANZANIA” AMBAO ILIKUWA AWE AIDHA MGONJA AU CLEOPA MSUYA. KWA WANAOKUMBUKA HATA KUNA WATU WALIPOTEZA MAISHA INGAWA MLENGWA ALIKUWA MGONJA. MWL. NYERERE ALIGUNDUA TOO LATE HILA HIZO, NA NDIO MAANA CLEOPA HAKUDUMU KATIKA UWAZIRI MKUU WAKE. BAADAYE MGONJA ALIPEWA UKUU WA MKOA SHINYANGA AMBAPO MAHAKAMA TENA WALIMGOMEA MWL KWA MADAI KWAMBA MGONJA ANARUDISHWA BUNGENI TENA KWA KUPITIA MLANGO WA NYUMA. ANYWAY KATIKA ILE DHULUMA KUU DHIDI YA MGONJA, LENGO LILIKUWA KUMUUA NYOTA YAKE KATIKA SIASA NA HATA KUMKATISHA MAISHA ILIBIDI NA KWA KWELI WALIFANIKIWA KWA KIWANGO KIKUBWA. KAMA WALIOMFANYIA WANA RAHA HILO NAWAACHIA KINA CLEOPA, BANDUKA, KISUMO, MGAYA NA WENZAO AMBAO BADO WAKO HAI. MGONJA ALIKUWA CHAPA KAZI , MWANASIASA MAHIRI TANGU UJANA. UKIPENDA CHUKUA HUPENDI WAACHIE WENYEWE WAPIME.
 
mbobevu wa sheria lisu anasema hoja ya prof shivji inazingatia zaid taaluma inavyotaka na haizingatii mazngira ya siasa za bongo. kwamba kwa mambo yanavyoenda bongo taaluma iwekwe pemben isizingatiwe? ajabu

La Hasha Mkuu, hapo ana maanisha kuwa hata sheria inahitaji matumizi kwa vitendo siyo nadharia peke yake. Aonekanvyo Mh. Lisu yeye anaitumia elimu yake ya sheria vilivyo kwa vitendo zaidi. Anaitumia "practically" kuendeleza jamii!. Prof. anafundishia zaidi.

Sasa wewe fikiria anayeshtaki anaulizwa maswali rahisi pale mahakamani anashindwa kujibu. Anayeshtaki hamfahamu wakili wake? Na majaji wengine hawaoni hata haja ya kuweka kumbukumbu sawa kuwa wanoshtaki ni kweli ni wapiga kura? Ina maana anaweza toka mtalii mmoja huko akafungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na kesi hiyo mahakamani? Nina hakika kabisa kwamba inapotokea mwananchi anafungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi na wala si mhusika aliyeshindwa, huyo mwananchi anakuwa ametumiwa. Pili kwa standard zetu waafrika na haswa nchi yetu, kwa mwanamke kuamua kutumia fedha zake kuendesha kesi kama hiyo si jambo la kawaida hata kidogo. Tena kwa taarifa yako hata wa Ulaya isingekuwa rahisi kuchukua uamuzi huo. Wakinamama ni watu makini sana katika maswala ya uchumi binafsi. Atashiriki kufanya hivyo kama tu ametumwa (kuwa hatatumia fedha zake binafsi) na anaona kuna maslahi. Upelelezi makini ukifanyika itagundulika kuwa wale wamama wawili walitumiwa kupinga ushindi wa Lema. Hata kwa kuchunguza mwenendo wa akaunti zao tu ingetosha kubaini ukweli.
 
Hapana mkuu nimefurahi walivyofuatilia habari hii kwa kina na naamini hawataishia hapo!

Kama wangekuwa na muendelezo huu kwenye habari nyeti kama ufisadi pengine yangekuwepo mabadiliko makubwa.

Kuhusu Prof Shivji naamini hajaisoma hukumu na hakuelewa mazingira ya kesi ndio maana amedhani haki ya mpiga kura imekiukwa!

Mkuu, hapo kwenye RED, UMENIKUNA KUMOYO!! Hawazifanyii mwendelezo kesi za ufisadi au zinazowahusu vigogo kwa sababu ya BAHASHA!!!
 
Back
Top Bottom