Kesi ya Lema: Lissu amkaanga Profesa Shivji

Kesi ya Lema: Lissu amkaanga Profesa Shivji

Kwa jinsi mtu anavyozidi kuzeeka ubongo unakuwa 'senile' lakini wa mtoto unazidi kukua. Kwa hiyo mwanafunzi anaweza kumzidi mwalimu wake kiakili na maarifa.
 

1. “Lissu katika maelezo yake alisema uamuzi wa mahakama katika kesi ya Lema umejenga upya msingi bora wa matumizi ya vyombo vya uamuzi, kwani kesi nyingi za kupinga matokeo ya ubunge, zimekuwa zikifunguliwa na watu ambao wamekuwa wakitumwa na vigogo wa kisiasa na watu wenye fedha.” GAZETI LA MWANANCHI – 28 DEC 2012

2.“Kwa mtazamo huo huo, tunathibitisha pasipo shaka kuwa Kesi ya Mgonja ilihukumiwa kinyume, ilitoa tafsiri potofu ya ‘hoja yamsingi ya uwepo wa kesi ya kujibu. Tunasema hivyo kwa kuwa hatufikirii kwamba Mahakama iliruhusu kila mpiga kura yeyote bila kuzingatia mahali alipojindikisha na kupiga kura anaweza kupinga matokeo yauchaguzi wowote, wa jimbo lolote mahakamani katika nchi hii. Utakuwa ni ujinga.”
Sehemu ya hukumu kama ilivyotolewa Dar es Salaam, tarehe 19, Decemba, 2012. Mbele ya Jaji, N.P Kimaro, B.M Luanda na S.A. MASATTI.
2. Hapa chini pia naweka CV ya mtu aliyetajwa kuwahi kuhukumiwa kinyume kwa sheria hiyo ambayo leo mahakama ya rufaa imeiweka in its right perspective. Mgonja aliwahi kuwa Waziri kamili akiwa kijana mbichi wa umri wa miaka 31….Naamini hata Lema ni mmoja wa wabunge vijana shupavu na ndio maana anapigwa vita nyingi ya kijinga kwa kutumia ofisi na pesa za matajiri na umma. Kwa nini tusijifunze kuheshimu maamuzi ya wapiga kura? …tunawaangamiza vijana shupavu wa ki Tanzania sababu ya chuki, pesa na madaraka….tutachuma laana….

Chedieli Yohane Mgonja.

kuzaliwa 31 December 1934, Vudee Same-Magharibi.

shule ya msingi Vudee, sekondari Ilboru na Tabora.

1959 ---Chuo Kikuu Makerere.

1960 ---Bwana Shauri Tanga.

1961 --- miongoni mwa Watanganyika sita waliotunukiwa zawadi kwa kushiriki ktk shindano la utenzi wa wimbo wa taifa wa Tanganyika.

1961 --- 62 Chuo Kikuu Cambridge UK -- kozi ya utawala na Diplomasia.
wengine katika kozi hiyo ni walioapata kuwa mabalozi George Nhigula,John Malecela, Bernard Mulokozi, Raphael Lukindo, Akili Daniel.

1962 --- Ubalozi wa Tanganyika New York.

1964 --- kuomba kurudi nyumbani kwa nia ya kugombea Ubunge.

1965 --- kupigania ubunge wilaya ya Pare vs Naibu Waziri na katibu mwenezi wa Tanu Elias *******.

1965 --- 67 Mbunge wilaya ya Pare, Waziri wa Maendeleo na Utamaduni. rekodi ya kuwa waziri kijana kuliko wote Tanzania.

1967 -- 68 Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi ( Mambo ya Nje ). waziri wa kwanza kujiunga na mafunzo ya JKT. baadaye kuendelea na mafunzo ya mgambo. waziri aliyetoa tamko la serikali ya Tanzania kuitambua Jamhuri ya watu wa Biafra.

1968 -- 72 Waziri wa Elimu. mabadiliko makubwa ktk mfumo wetu wa elimu yalifanyika kipindi cha uongozi wake.

1972 -- 75 Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Chama Mtwara. ni uteuzi pekee ambao Mwalimu alimjulisha kabla haujatangazwa. ilikuwa ni kipindi cha madaraka mikoani na vita ya ukombozi ya Msumbiji. mkoa wa mtwara kushika nafasi ya pili, ukifuatia dsm, ktk kuchangia vita vya ukombozi.

1977 -- Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Chama Tabora.

1977 -- 1980 Waziri wa Utamaduni, Vijana, na Michezo. Tanzania kukataa shinikizo la Marekani kususia michezo ya olympic Moscow. Ujumbe wa Marekani uliletwa na Mohamed Ali.

1980 -- 1982 kushinda Ubunge. Kushinda kesi dhidi yake mahakama Kuu Arusha. Kuvuliwa Ubunge na mahakama ya Rufaa Tanzania.

1984 -- kuteuliwa na Raisi Mkuu wa Mkoa Shinyanga.

1985 -- 95 Mbunge Wilaya ya Same: vs Jonas Manento(85) vs.Dr.Kivurunya Mtera(90).

Chedieli Yohane Mgonja, mbunge wa mwisho wilaya ya Pare(mwanga + same), na mbunge wa mwisho wilaya Same( same mashariki + magharibi )

 
Kweli Siasa Mchezo Mchafu..Juzi tu Profesa alikuwa ni Shujaa mwenye kuheshimiwa ...leo Amezeeka
Kesho akisema la kutufurahisha tutasahau uzee wake na kumwita Kamanda
 
Nimefurahishwa na kitendo cha Shivji na Rais wa TLS kutoa mawazo yao juu ya hukumu ya rufaa ya Lema hivi ndivyo wasomi wanavyotakiwa kufanya kutoa mchango wao pale wanapoona mambo yanaharibika lakini mbona hatujawasikia wakati lilipoibuliwa swala la majaji wasio na sifa huyo Rais wa TLS alilizungumzia kidogo wakati ile ndio ilikuwa nafasi yake kuonyesha namna gani wanasimamia sheria nchini kwa kifupi aache unafiki akijifanya ana uchungu wakati anaacha mambo mazito yanapita bila kuhoji

Hivi ndivyo wasomi wetu wanavyoumbuka. Hii inaonyesha wazi kuwa sisi watanzania baada ya kupata elimu hatuitumii zaidi kwa maendeleo ya Taifa bali ubinafsi zaidi. Yaani katika sehemu ambazo wananchi wengi hupoteza haki zao nadhani katika maswala ya sheria na haswa mahakamani ni namba moja. Leo hii mtu hata hajawahi sikika anaongea kisa mbunge wa upinzani kashinda kesi. Wakati huo huo Raisi huyu wa TLS alitakiwa kuwa neutral zaidi. Kinyume chake kavua koti kubakia na shati ya kijani. Hafai kabisa kuwa Raisi wa hicho chama, I am sorry! Huo ni mtazamo wangu tu. Pia ninaamini kuwa hata Mh. Lissu kwa sasa haitakuwa sahihi tena kwake kuwa raisi wa hiyo TLS.
 
Inapaswa wajue kuwa sheria nimsumeno ifikie mahali sheria ifanye kaziyake, sheria haitambui ccm, wala cdm.
 


1. “Lissu katika maelezo yake alisema uamuzi wa mahakama katika kesi ya Lema umejenga upya msingi bora wa matumizi ya vyombo vya uamuzi, kwani kesi nyingi za kupinga matokeo ya ubunge, zimekuwa zikifunguliwa na watu ambao wamekuwa wakitumwa na vigogo wa kisiasa na watu wenye fedha.” GAZETI LA MWANANCHI – 28 DECEMBER 2012
2.“Kwa mtazamo huo huo, tunathibitisha pasipo shaka kuwa Kesi ya Mgonja ilihukumiwa kinyume, ilitoa tafsiri potofu ya ‘hoja yamsingi ya uwepo wa kesi ya kujibu. Tunasema hivyo kwa kuwa hatufikirii kwamba Mahakama iliruhusu kila mpiga kura yeyote bila kuzingatia mahalialipojindikisha na kupiga kura anaweza kupinga matokeo yauchaguzi wowote, wa jimbo lolote mahakamani katika nchi hii.Utakuwa ni ujinga.”
Sehemu ya hukumu kama ilivyotolewa Dar es Salaam, tarehe 19, Decemba, 2012. Mbele ya Jaji, N.P Kimaro, B.M Luanda na S.A. MASATTI.

3.KESI YA UBUNGE YA GWIJI LA SIASA ZA UPARE “EARLY 60’S – EARLY 80’S MAREHEMU CHEDIEL YOHANA MGONJA, KAMA ILIVYOFUNGULIWA DHIDI YAKE NA WAPIGA KURA ATHINIELI AHIYA NA WILLIAM BAKARI, HUKU MGONJA AKISHINDA MAHAKAMA KUU ARUSHA NA BAADAYE KUTENGULIWA NA MAHAKAMA YA RUFAA DAR-ES-SALAAM NDICHO WAKILI MAKINI MNO HON. TUNDU LISSU ANACHOMAANISHA HAPO NO 1 JUU - UNDERLINED. KWA WALE “PLAYERS” KATIKA KESI YA MGONJA AMBAO BADO WAKO HAI NA WAKWELI, LEO MAHAKAMA YA RUFAA TANZANIA IMEMPA HAKI YA UBUNGE LATE HON.CHEDIEL MGONJA AKIWA KABURINI , LAKINI PIA KIJANA HON. GODBLESS LEMA. HAKI YA MTU HAIPOTEI NA MWENYEZI MUNGU KAITOA MBELE YA WATESI WA MGONJA AMBAO BADO WANAISHI. KWA KUMBUKUMBU ZANGU NA RECORD HAPA, WALIOKUWA NYUMA YA WAPIGA KURA WAWILI HAWA KUMPINGA MGONJA WALIKUWA NI AKINA CLEOPA MSUYA, MGAYA WA ELEPHANT MOTEL ENZI ZAKE, MAREHEMU JUDGE NASORO MZAVAS, MAREHEMU SAMMY MDEE, PETER KISUMO,NICODEMUS BANDUKA NA BAADHI YA WAPARE MATAJIRI NA TATIZO LENYEWE LILIKUWA “UWAZIRI MKUU WA TANZANIA” AMBAO ILIKUWA AWE AIDHA MGONJA AU CLEOPA MSUYA. KWA WANAOKUMBUKA HATA KUNA WATU WALIPOTEZA MAISHA INGAWA MLENGWA ALIKUWA MGONJA. MWL. NYERERE ALIGUNDUA TOO LATE HILA HIZO, NA NDIO MAANA CLEOPA HAKUDUMU KATIKA UWAZIRI MKUU WAKE. BAADAYE MGONJA ALIPEWA UKUU WA MKOA SHINYANGA AMBAPO MAHAKAMA TENA WALIMGOMEA MWL KWA MADAI KWAMBA MGONJA ANARUDISHWA BUNGENI TENA KWA KUPITIA MLANGO WA NYUMA. ANYWAY KATIKA ILE DHULUMA KUU DHIDI YA MGONJA, LENGO LILIKUWA KUMUUA NYOTA YAKE KATIKA SIASA NA HATA KUMKATISHA MAISHA ILIBIDI NA KWA KWELI WALIFANIKIWA KWA KIWANGO KIKUBWA. KAMA WALIOMFANYIA WANA RAHA HILO NAWAACHIA KINA CLEOPA, BANDUKA, KISUMO, MGAYA NA WENZAO AMBAO BADO WAKO HAI. MGONJA ALIKUWA CHAPA KAZI , MWANASIASA MAHIRI TANGU UJANA. UKIPENDA CHUKUA HUPENDI WAACHIE WENYEWE WAPIME.

RIP Chadiel Mgonja. Nadhani hukumu ya Godbless Lema imesababisha ujigeuze huko kaburini kwa furaha!
 
Malafyale,
Maelezo ya Lissu ndio yanathibitisha kabisa kwamba kilichofanyika sio tafsiri ya sheria bali kutengeneza sheria mpya.

Kama wangeona sheria ya mwaka 1985 ina makosa au inakiuka katiba basi wangelisema hivyo. Ila kusema sheria inakuwa abused kwahiyo tunaifuta au tunaiwekea ukomo sio kazi ya mahakama, hiyo ni kazi ya bunge.

Mtanzania

Mahakama ya rufaa imesisitiza kuwa ili ufungue kesi lzm uonyeshe ni kwa vipi haki zako za msingi kama mpiga kura zimekiukwa na cordially Am here to endorse the ruling!

Wapiga kura kama Mussa Mkanga aliyefungua kesi Arusha na wenzake SIJAONA SEHEMU TOKA KESI HII IANZE WALIPOONYESHA KUWA HAKI ZAO ZA MSINGI ZILIKIKUWA!

Hawa wanatumiwa tu toka kuambiwa wafungue kesi hadi kulipiwa gharama za mawakili;Mahakama ya rufaa HAJATUNGA SHERIA MPYA bali imeweka msisitizo kwa ALIYEATHIRIKA NA MATOKEO YA UCHAGUZI DIRECTLY NDIYE MWENYE HAKI YA KUFUNGUA KESI;hawa hawakuathirika na lolote kwenye uchaguzi huo ulio mpa ushindi MB Lema!
 
......Mwalimu na mwanafunzi.......inapendeza....

Halafu wanatokea wapuuzi wengine wanamlinganisha Kamanda Lissu na AG! Lissu saizi yake ni zaidi ya maprofessa wala hafananishwi na gamba lolote hata lingeelimika kwa kiwango gani!
 
nimefurahishwa na kitendo cha shivji na rais wa tls kutoa mawazo yao juu ya hukumu ya rufaa ya lema hivi ndivyo wasomi wanavyotakiwa kufanya kutoa mchango wao pale wanapoona mambo yanaharibika lakini mbona hatujawasikia wakati lilipoibuliwa swala la majaji wasio na sifa huyo rais wa tls alilizungumzia kidogo wakati ile ndio ilikuwa nafasi yake kuonyesha namna gani wanasimamia sheria nchini kwa kifupi aache unafiki akijifanya ana uchungu wakati anaacha mambo mazito yanapita bila kuhoji


Si ndio waanza kuibua mijadala kama hii ili kuchanganua nani ni yupi anafanya nini kwa namna gani na kwa manufaa ya nani.Hii ni nzuri sana kwa afya ya sheria nchini,kikubwa tu tusiichukulie kama ni kujipendekeza sijui nani ili sijui apate ukuu fulani.Kiukweli huu ni mpambano wenye tija kwa wenye weredi husika na kwa taifa kwa ujumla ili siku ingine pasiwepo malalamiko yanayohusu tasnia nyeti kama hiyo.
 
Mi nadhani kutokujua kitu sio dhambi. Hivyo basi, kwa wenzangu na mimi ambao kidogo sheria imetukaa kando bora tuwe wasomaji tu na kulike kama ukiguswa kuliko kuleta ushabiki uchwara kwenye mambo ya kitaaluma.
Mnakera sana.
 
Mimi naamini Prof. Shivji ameisoma hukumu na hajanukuliwa vibaya. Huo ndio msimamo wake (maoni yake) juu ya hukumu hiyo.
Kwa gwiji wa sheria kama yeye sidhani kama anaweza kutoa comment nzito kiasi hicho kabla ya kujiridhisha kwa kuisoma hukumu husika.

Mkuu usimpe Pro. Shivji Umungu, kwanini isiwezekane kuwa huakuisoma.
 
Mkuu nakuona unachungulia hapa tafadhali tunaomba comments zako kwenye hoja hii.
There are currently 150 users browsing this thread. (24 members and 126 guests)





 

Halafu wanatokea wapuuzi wengine wanamlinganisha Kamanda Lissu na AG! Lissu saizi yake ni zaidi ya maprofessa wala hafananishwi na gamba lolote
hata lingeelimika kwa kiwango gani!
Ni kweli kabisa mheshimiwa...jambo lolote la kitaalam linapoingiliwa na siasa basi huwa ni vigumu kulijadili.....utaalamu huwekwa kando...... mara nyingi hutegemea wangapi wanakusikiliza bila kujali unachoongea...
 
Back
Top Bottom