Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea?

ALIYEKUWA Msajili wa kwanza wa vyama vya siasa, Jaji George Liundi, amefariki dunia juzi mchana nyumbani kwake Keko Juu jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Tanzania Daima, mtoto wa marehemu, Taji Liundi, alisema baba yake alifariki dunia saa 7 mchana baada ya kuugua malaria, shinikizo la damu na maumivu ya mgongo.

Taji alisema taratibu za mazishi zinafanywa na familia nyumbani kwao Keko Juu, ambapo marehemu Liundi anatarajiwa kuzikwa Alhamisi katika makaburi ya Chang'ombe. Enzi za uhai wake marehemu Liundi alikuwa msajili wa kwanza wa vyama vya siasa, ameacha watoto watatu na wajukuu wanne.

Akiwa Jaji, Liundi alipitia hatua ngumu kwenye maisha yake, baada ya mkewe Agnes Doris Liundi kushitakiwa na Jamhuri mwaka 1979 kwa kosa la kuwaua watoto wake watatu kwa kuwanywesha sumu Februari 21,1978 nyumbani kwao jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo iliyokuwa mbele ya Jaji Lewis Makame, Agness aliyeolewa na Liundi mwaka 1967 alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Source:
Tanzania Daima – Jaji Liundi afariki dunia

CC: Mtambuzi,
[MENTION]JokaKuu[/MENTION], [MENTION]Joka Kuu[/MENTION], [MENTION]RR[/MENTION], NATA, ram, Asprin, Mwita Maranya, Pasco, Mentor, Mama Joe, magee, FirstLady1, The Boss, [MENTION]JS[/MENTION], Kidogo chetu, Lukolo, Bigbro, Mtumishi Wetu, Leftist, B'REAL, Kombo, kadoda11, kanga, GIUSEPE, BPM, MAHEPE, Kongosho, mkomatembo, ALEX PETER, webondo, Ronn M, Kijivo, sober saimoni
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mtambuzi nimesahau kuuliza, kwa hiyo hiyo hukumu ilishatekelezwa? Au mama bado yuko jela, au alifariki natural death? Na kama alifariki natural death alifia jela au wapi? Samahani, ni OP kidogo.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom