Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea?

Nataka Kumuongelea Taji. Naamini mpaka ukubwa wake huu, anafahamu ndani nje ya suala hili. Pongezi kwake kwani hajaruhusu suala hili liwe kizingiti katika maisha yake, the way I see it! Ni ngumu, chungu and you do not wish for that! Pole Taji.

Mimi leo ndiyo naona thread hii. Miaka kama mitano iliyopita niliwahi kumsoma Taji Liundi kwenye gazeti moja akieleza kidogo ilivyotokea.

Yeye anasema walipewa soda na kilichomuokoa Taji ni kwamba Taji sik hiyo alikuwa anacheza na wenzake. Alipoitwa kuja kunywa soda akaona soda itampotezea muda kwani anaweza kunyimwa namba na wenzake atakaokuta wanacheza.

Hivyo akaona dawa ni kujifanya ameimaliza na kuimwaga nyingi pembeni bila mama yake kujua.

Lakini Taji alieleza kwamba hata hiyo kidogo aliyoonja alipoenda kucheza alizimia huko na alipozinduka akajikuta yuko Hospitali.

Mnaosema Taji sijui afanye nini. Yeye mwenyewe nimimsoma akisema kwamba iko siku atamuuliza mama yake kwa nini alitaka kuwaua!
 
Thanks Mtambuzi!kesi hii ni moja ya kesi zilizowahi kutikisa jiji la Dar,kamakesi ilivyofuata kwenye miaka ya 80 mwanzoni kesi iliyomuhusu Dr huyu huyu kwenye kesi hii.Jambo kubwa hapa,kesi zote zilihusisha mambo ya mapenzi,tena kwa vijana wasomi wa kipindi hicho!na zote zilipelekea mauaji ya kutisha!!!Jamo moja kubwa la kujifunza hapa kwetu sote,pamoja na madhaifu yetu kama binadamu,hakuna jambo linaloweza kuumiza nafsi ya mwenzio kama usaliti wa mapenzi.Na basi tunapoamua kuingia katika ndoa ni lazima uamuzi huo uwe umefanyika kwa dhati!!Leo mzee Liundi pamoja na heshima yake katika jamii nadhani ni jambo linalomuumiza mpaka siku mauti yatakampomkuta!!!TUPENDANE KWA DHATI!!!!NDOA SIO MAIGIZO AU MAKARATASI YA MAKANISANI,MSIKITINI AU KWA MKUU WA WILAYA!!

na amefariki
 
Very touching...RIP Mama Liundi,Mwenyezi Mungu akupunguzie adhabu akupe pumziko lenye heri,inasikitisha sana.
 
Mimi leo ndiyo naona thread hii. Miaka kama mitano iliyopita niliwahi kumsoma Taji Liundi kwenye gazeti moja akieleza kidogo ilivyotokea.

Yeye anasema walipewa soda na kilichomuokoa Taji ni kwamba Taji sik hiyo alikuwa anacheza na wenzake. Alipoitwa kuja kunywa soda akaona soda itampotezea muda kwani anaweza kunyimwa namba na wenzake atakaokuta wanacheza.

Hivyo akaona dawa ni kujifanya ameimaliza na kuimwaga nyingi pembeni bila mama yake kujua.

Lakini Taji alieleza kwamba hata hiyo kidogo aliyoonja alipoenda kucheza alizimia huko na alipozinduka akajikuta yuko Hospitali.

Mnaosema Taji sijui afanye nini. Yeye mwenyewe nimimsoma akisema kwamba iko siku atamuuliza mama yake kwa nini alitaka kuwaua!
Huyo mama amefariki juzi, na jumanne wanamzika.

Unaweza fuatilia updates khtoka kwenye akaunti ya insta ya tajiliundi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom