Kesi ndogo ya Freeman Mbowe: Shahidi akamilisha ushahidi wake, Shahidi mwingine kuendelea tarehe 12/11/2021

hii kitu hachomoki walahi!!! Kama timu kibatala imeanza kuishiwa pumzi Basi jamaa hachomoki kwa hii kitu!!
 
Huyu afande Jumanne Malangahe kweli ni MWONGO sana...

Yaani mji wa Moshi ambao hauna foleni za magari kutoka KCMC kwenda Rau Madukani walitumia dakika 45...!!!!!?????

Duuh, ama kweli njia ya mwongo ni fupi sana...

Kwa wasioifahamu Moshi Manispaa, umbali wa kutoka KCMC hadi Rau Madukani, kwa DSM tunaweza kulinganisha na umbali wa kama kutoka Buguruni kwenda Shule ya Uhuru....!!

Sasa hapo kwa gari na tena ni sehemu isiyo na msongamano unaweza kutumia dkk 45 kweli?? Labda uwe unasukuma gari kwa mikono...!!!

Yaani huu ni uthibitisho tosha kuwa hii kesi in UONGO uliotengenezwa na watu tu waliokuwa wamekaa ofisini kwa kusukumwa na NIA OVU nyuma yake...
 
Jaji ameingia..

Kesi inatajwa...

Quorum zipo vile vile...

Mtobesya: Shahidi Wakati Mnamkamata Ling'wenya ni taarifa zipi Mlikuwa nazo tayari?

Shahidi: Taarifa tulizokuwa nazo alikuwa ni Miongoni Mwa Kundi ambalo lina fanya Njama Kwa Kufanya Vitendo Vya Kigaidi ambavyo ni
Kushiriki katika Kulipua Vituo Vya kuuzia Mafuta

Kukata Miti na Kuweka Barabarani, Kulipua maeneo yenye Mkusanyiko wa watu na Kuhamasisha Maaandamano ya siyo na Kikomo.
Mtobesya: Ni hizo Taarifa tu au Mlikuwa na Zingine?

Shahidi: Kimyaaa

Mtobesya: Ni nani aliwasaidia Kuwapa Taarifa Mpaka Mkajua Eneo alilokuwa Ling'wenya?

Shahidi: Nilikuwa na Mkuu wangu Afande Kingai yeye Ndiye alikuwa anajua aliyekuwa nampa taarifa
Mtobesya: Nitakuwa sahihi Kwamba Mpelelezi yoyote kabla hajafanya Upelelezi anakuwa na dhana Kichwani unapoenda Field Unaenda kuthibitisha Kama ni Chanya au Hasi ni sahihi?

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji Kwenye Shauri hili Dhana yako ilikuwa ni nini
Shahidi: nilikuwa naenda Field Kuthibitisha tuhuma kama Mtuhumiwa huyo anahusika

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji ilichukua muda gani, tangu unatengeneza Dhana hiyo Mpaka Mnamkamata Ling'wenya

Kimyaaaaaaaaaa kinatawala kwa sekunde kadhaa hapa... Namna gani!
Jaji: anamuuliza Shahidi kama ameelewa Swali

Shahidi anapata kigugumizi kidogo anashindwa kuongea hapa..

Lakini anafanikiwa kuendelea..

Shahidi: Ni palepale nilipopata Taarifa na Kuanza Kutafakari na haikuchukua Muda Mrefu

Mtobesya: Mueleze Jaji Taarifa hizo ulizipata lini
Shahidi: Siku ya Tarehe 04 August 2020

MTOBESYA: na Ling'wenya Mlimkamata tarehe ngapi?

Shahidi: Naomba nirejee Nyuma ya Swali Lako ulilokuwa Umeniuliza

MTOBESYA: enheeeeeeee!
Shahidi: UMENIULIZA Iinachukua Muda gani Kuniwezesha Kwenda Field

Mtobesya: Sijakuuliza Swali hilo

Shahidi: Dhana ni Kama Kitu ambacho huna a Uhakika nacho

Mtobesya: Hapana namaanisha HYPOTHESIS, Mpelelezi Yoyote lazima awe na Hypothesis

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Mtobesya: Nakurudisha Kwenye Swali Sasa, Je Mlimkamata lini Ling'wenya

Shahidi: Tarehe 05 August 2020

Mtobesya: Maelezo Ya Ling'wenya uliyaandika lini

Shahidi: Tarehe 07 August 2020

Mtobesya: Kwa hiyo nitakuwa Sasa Kwamba Wakati Unamuhoji ulikuwa na Taarifa

Shahidi: Hapana Sikuwa na Taarifa

Mtobesya: Siwezi Kukunyonga kwa Majibu yako. Haya Umesema Ling'wenya alikiri Kujihusisha Kufanya Vitendo hivyo ni Vipi

Shahidi: Kwamba kweli alijihusisha na Vitendo Vya kupanga Njama
Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema Mpelelezi asiandike Maelezo ya Mtuhumiwa, Kwa sababu Mpelelezi anataarifa Nyingi Wakati anampeleleza?

Shahidi Hapana Siyo Sahihi

Mtobesya: Kwa hiyo pale ambapo Kuna Askari Mwingine na Mpelelezi Yupo Hairuhusiwi Askari Mwingine Kuchukua Maelezo
Kwamba Hamkuwezesha Kukutana na Ndugu..

Shahidi: Sahihi Sikusema
Mtobesya: Kwa hiyo tunakubaliana kwamba Nitakuwa sahihi nikisema Kwamba Mtu pekee anayejua kama Mtuhumiwa alikamatwa ni Nyie Mlimkamata, Yeye aliyekamatwa na Mtu aliyekamatwa Wakiwa Pamoja

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Unaelea nini Kuhusu Maelezo ya Onyo
Shahid: Ni yale yanayo chukuliwa Kuhusu Mtuhumiwa anahusishwa na Kutenda aina fulani ya Kosa

Mtobesya: Ni hivyo tu?

Shahidi: INATOSHA

Mtobesya: Nitakuwa Sahihi nikisema Maelezo ya Onyo Yanatakiwa Kuonyesha Mtuhumiwa Kosa analo tuhumiwa nalo

Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya: Nitakuwa Sahihi Kwamba Kosa Unalomuonya Nalo ni lazima liwe limetamwaka Kwenye Sheria

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Nitakuwa Sahihi Kwamba Maelezo ya Onyo Yanatakiwa kuwa Sheria na inatakiwa Kuonyesha Kifungu Unachomuonya nacho

Shahidi: Siyo Kweli, unaweza Kumwambia Kwa Maneno tu

Mtobesya: Kwa hiyo siyo Muhimu Kumtajia Kifungu unacho Muonya nacho?

Shahidi: Ni Muhimu kwa Minajiri ya Kumuonya mshtakiwa Mwenyewe

Mtobesya: Kwa hiyo kwako wewe Siyo Muhimu

Shahidi: Nilisahau lakini nilikuwa nishamwambia

Mtobesya: Nitakuwa sahihi Kwamba ni Matakwa ya Kisheria, Baada ya zoezi la Kuonya Kuisha Tarehe, Mwaka na Muda lazima viwe katika fomu unayotumia Kumuonya

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: na wewe Uliweka hivyo

Shahidi: Ndiyo Niliweka

Mtobesya: Tutaona baadae kama Uliweka
Mtobesya: na nitakuwa Sahihi Muda wa Kuonya Siyo Muda wa Kuchukua Maelezo, Unamuonya kwanza kisha Unamchukua Maelezo

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Kwa hiyo ni sahihi Kwamba muda wa Kuonya ni Tofauti na muda wa Kuchukua Maelezo

Shahidi: Ni sahihi
Mtobesya Twende kwenye Hitimisho la Kuandika Maelezo pale unapotakiwa Kuthibitisha

Nitakuwa Sahihi nikisema Ufungaji wa Maelezo ya onyo una namna Mbili au Tatu kwanza wa Mtu anaye Jua Kusoma na Kuandika na ameridhia Kwa anaye andika, ambaye ajui Kusoma na Kuandika au amekataa na Mwisho Mtu ambaye amekataa

Shahidi: Siyo Sahihi

Mtobesya: Haya tueleze Wewe Wa kwanza anathibitisha vipi

Shahidi: Yeye Mwenyewe anaandika Kwamba nimeyasoma na Kuyaelewa

Mtobesya: na hiyo inaonekana katika Statement uliyoiandika

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Mtobesya Twende kwenye Hitimisho la Kuandika Maelezo pale unapotakiwa Kuthibitisha Nitakuwa Sahihi nikisema Ufungaji wa Maelezo ya onyo una namna Mbili au Tatu kwanza wa Mtu anaye Jua Kusoma na Kuandika na ameridhia Kwa anaye andika, ambaye ajui Kusoma na Kuandika au amekataa na Mwisho Mtu ambaye amekataa Shahidi: Siyo Sahihi Mtobesya: Haya tueleze Wewe Wa kwanza anathibitisha vipi Shahidi: Yeye Mwenyewe anaandika Kwamba nimeyasoma na Kuyaelewa Mtobesya: na hiyo inaonekana katika Statement uliyoiandika Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Mtobesya: na wewe Mwenyewe Unaandika Je Mwishoni

Shahidi: Unathibitisha Kuandika Maelezo ya Mtuhumiwa huyo

Mtobesya: huyo ambaye amesoma na kuandika, anathibitisha Vipi..? KWA signature na Dole Gumba Maana havitumiki kwa Pamoja

Shahidi: Alisaini Pamoja na Dole Gumba

Mtobesya: Kule Chini Mnapoweka Ithibati Kuna Vifungu Mnaviandika

Shahidi: sahihi

Mtobesya: Mueleze Jaji kwenye Maelezo yenu Mlitumia Vifungu gani

Shahidi: Ilikuwa Imeshaandikwa Kwenye Karatasi, niliona hakuna haja ya Kuweka hiko Kifungu
Mtobesya: Kitaje Kifungu

Shahidi: Kilikuwa Kifungu Cha 57(3)

Mtobesya: Umekitaja Maana Yake unakifahamu Mueleze Mheshimiwa Jaji kama hicho Kifungu aya zake

Shahidi: Sikumbuki Kama Zipo hizo aya

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe ID 1

Mahakama inampatia Mtobesya ID1

Mtobesya: Na Kuonyesha Kielelezo Cha Mahakama Nikuulize Maswali Machache, Iambie Mahakama Kama Baada Onyo Uliweka Muda

Shahidi anakuwa mbishiiiii hapa, Mbishi, lakini Mwishoni anasema HAKUNA MUDA..
Mtobesya: tuonyeshe uthibitisho amesoma na Kuyaelewa Sehemu gani

Shahidi: Mtuhumiwa amesaini na Kuweka Dole Gumba

Mtobesya: na Kifungu cha Sheria

Shahidi: Ndiyo nimesema Kwamba Karatasi ilikuwa Tight sikupata nafasi ya kuweka
Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji Pale ambapo Maelezo ya Mtuhumiwa anathibitisha Kuna Kifungu cha Sheria au Hakipo

Shahidi: Hakipo Kifungu cha Sheria
Mh,kazi kwelikweli,kesi hii itaingia kwenye rekodi za Karne hii Kama kesi ya kubambika aliyoandaliwa kizembe na watu wasio kuwa na ueledi wa kutosha kubambikia watu kesi😆😆😆 tuanzishe kozi maalumu watu wasome 😜😜
 
Huyu afande Jumanne Malangahe kweli ni MWONGO sana...

Yaani mji wa Moshi ambao hauna foleni za magari kutoka KCMC kwenda Rau Madukani walitumia dakika 45...!!!!!?????

Duuh, ama kweli njia ya mwongo ni fupi sana...

Maana kutoka KCMC hadi Rau Madukani ni umbali wa kama kutoka Mnazimoja [DSM] hadi Stesheni au Central Police DSM..

Sasa hapo kwa gari na sehemu isiyo na msongamano unaweza kutumia dkk 45 kweli?? Labda uwe unasukuma gari kwa mikono...!!!
Police wanaajiriwa kwa mbio na urefu ndiyo kipimo cha interviews
 
Huyu afande Jumanne Malangahe kweli ni MWONGO sana...

Yaani mji wa Moshi ambao hauna foleni za magari kutoka KCMC kwenda Rau Madukani walitumia dakika 45...!!!!!?????

Duuh, ama kweli njia ya mwongo ni fupi sana...

Maana kutoka KCMC hadi Rau Madukani ni umbali wa kama kutoka Mnazimoja [DSM] hadi Stesheni au Central Police DSM..

Sasa hapo kwa gari na sehemu isiyo na msongamano unaweza kutumia dkk 45 kweli?? Labda uwe unasukuma gari kwa mikono...!!!
Alijitahidi sana kukwepa kutaja muda sababu alijua atajichanganya na wale wenzake walishakwisha kutoa ushahidi.
Ushahidi wa kuchonga ni lazima wotw muwe makini saana msiende nje ya script..
 
Yaani wafuasi wa Mbowe wao wanacho taka kuona mara zote kuwa Jaji anaamua jinsi wao wanavyo taka, kinyume cha hapo, wataanzisha matusi na kejeli.

Hiii inathibitisha wazi jinsi walivyo funzwa na kiongozi wao tabia za kihalifu na wamekomaa.
Kichwa maji
 
hii kitu hachomoki walahi!!! Kama timu kibatala imeanza kuishiwa pumzi Basi jamaa hachomoki kwa hii kitu!!
Wamesha create reasonable doubt, mshitakiwa hakupekekwa kwa mlinzi wa amani na hakuthibitisha kukiri kwa maandishi,,
Hivyo kukiri kwake ni irrelevant im material,
Huwezi kutumia bastora yenye risasi tatu kulipua visima vya mafuta across country,, at least unahitaji baruti.
Hamna kesi hapo
 
hii kitu hachomoki walahi!!! Kama timu kibatala imeanza kuishiwa pumzi Basi jamaa hachomoki kwa hii kitu!!
Mungu ni wetu sote.Huwezi Amini Kabla ya MBOWE kufungwa Kuna kitu kinaweza kukutokea.Magufuli alitamani sana TUNDU LISSU afe haraka.Magufuli alikuwa zaidi yako alitamani kuona MBOWE anafungwa Maisha.Ukweli huu Magufuli alifariki kabla hayo hayajatokea.Mungu Ni waajabu Sana.Nilimwambia hayo ndugu yako jingalao akapuuza sasa hivi mateso anayo yapitia Ni zaidi ya MBOWE..!MBOWE atafungwa na hii ndiyo furaha na ushindi wa CCM ,familia yako Utapata kinga ya magonjwa MBOWE akifungwa,Familia atachana na umasikini MBOWE akifungwa.Ndugu zako wote hatakufa tena MBOWE akifungwa.Furahi na Kushangilia Kwani MBOWE atafungwa soon
 
ubambikiaji wakati mzee mboe alikuwa anapanga mikakati ya kuvuruga amani ya nchi, kisa uchu wa madaraka, sasa ngoja akawe mnyampara.
Umekazana kuita mboe ndio nani huyo? Au unashindwa kuandika vizuri kutokana na kukosa elimu na kuwa na matamanio yako yaliyopitiliza?
Angalia utakalia mpini bwege we!
 
Judge ame beti kwenye hii kesi, maamuzi yake hata kwenye rulling iliopita yana ukakasi sana. Kibatala & Co Ltd wanaivua nguo serikali na mahakama kwa pamoja.

Hata mwanafunzi wa 1st year anaesoma LLB, hawezi kutoa rulling isio na mashiko kisheria kama yeye mwenye experience ya zaidi ya miaka 15 katika tasnia ya sheria. Aibu hii.

Yeye mwenyewe Judge analijua hilo, na roho inamsuta anavojaribu kuliokoa jahazi la wakina Jamhuri.

Tatizo mnajiona wote ni wanasheria kweli zuzu ni zuzu tu
 
Hii kesi nashauri Rais Samia aongee na mwana sheria wake aiondoe tu ili Serikali yake iendelee kuheshimiwa.
Sababu moja kuu
Rais Samia hii kesi kaikuta mezani.
Waliopanda asilimia kubwa hawapo ofisini au duniani.
Samia aitumie kesi kujijengea heshima mbele ya jamuia ya kimataifa.
 
Mungu ni wetu sote.Huwezi Amini Kabla ya MBOWE kufungwa Kuna kitu kinaweza kukutokea.Magufuli alitamani sana TUNDU LISSU afe haraka.Magufuli alikuwa zaidi yako alitamani kuona MBOWE anafungwa Maisha.Ukweli huu Magufuli alifariki kabla hayo hayajatokea.Mungu Ni waajabu Sana.Nilimwambia hayo ndugu yako jingalao akapuuza sasa hivi mateso anayo yapitia Ni zaidi ya MBOWE..!MBOWE atafungwa na hii ndiyo furaha na ushindi wa CCM ,familia yako Utapata kinga ya magonjwa MBOWE akifungwa,Familia atachana na umasikini MBOWE akifungwa.Ndugu zako wote hatakufa tena MBOWE akifungwa.Furahi na Kushangilia Kwani MBOWE atafungwa soon
Magu alipiga push ups kwa kumkejeli Lowassa. Alijiona ni mzima na mwenye kinga. Alimuona Lowassa ni mgonjwa na kifo kinamnyemelea. Aah wapi Mungu ni Mkubwa kuliko awae yote ktk dunia hii.
 
1636649809328.png
 
Yaani Askari Mzima Kwa Anakiri Kuwa Kesi Ya Ugaidi ni Kesi Kubwa, Lakini Anasema Hakuona Umuhimu wa kutumia Audio recording au video kumuhoji Mtuhumiwa Angeuwawa Huko Ndani? Hivi hawa Askari wetu Hata Movie Tuu hawaangalii?

Askari amefanya kazi Dar es Salaam lakini kuna vituo Vya Polisi Havijui?

Askari amehamisha Mahabusu kuepuka mchanganyiko na Taarifa kuvuja, lakini hajui kama watuhumiwa walikuwa Isolated au laaa, sasa ulihamisha Wa Nini?
 
leo mmefurahi eeeh...
sasa ikitokea siku nyingine mmekataliwa muwe na heshima na adbu.
acheni matusi, ukorofi na kejeli, hivyo hivito msaidia mzee wenu mboe.

Ndezi, hujajua madhara ya nyaraka kukataliwa mahakamani! Usichojua ni kuwa kazi ya utetezi sio kuonesha Mbowe na wenzie hawakufanya makosa wanayoshtakiwa nayo bali kuweka shaka katika mashitaka. Kama jaji ataamua kwa msingi wa “ushahidi usiokuwa na mashaka” basi washitakiwa wataachiwa huru!!

Mashaka yaliyowekwa sasa hivi ni namna nyaraka hii ilivopatikana wakati ilikuwa mahakamani! Je mahakama inawasiliana na waleta mashitaka against washitakiwa?? Usione jaji ni mjinga, wala usione ni ushindi kwa Chadema. Jaji kaamua kuikataa document ambayo mbeleni angeulizwa waleta mashtaka wameipataje bila maombi!!

Ndezi kama wewe mnaagaliaga mtu alipoangukia, badala ya kwanini ameanguka!
 
Hii kesi nashauri Rais Samia aongee na mwana sheria wake aiondoe tu ili Serikali yake iendelee kuheshimiwa.
Sababu moja kuu
Rais Samia hii kesi kaikuta mezani.
Waliopanda asilimia kubwa hawapo ofisini au duniani.
Samia aitumie kesi kujijengea heshima mbele ya jamuia ya kimataifa.
Kwani mmesahau kuwa Mh SSH alikuwepo kwenye Serikali ya mwendazake, na kwamba haya mambo yalisukwa miezi ya July/August cho2020?
Lakini mama aliingia kwa ahadi kuwa hataki kuona kesi kubambikia watu.
Kilichokuja kuvuruga haya masuala/kesi hii ni pale mkuu wa jeshi la polis IGP alipoongea na chombo kimoja cha habari cha Dakika 45 aliposema Mbowe ni mhalifu hata kabla mahakama haijamhukumu.
Mbaya zaidi tena pale Rais wetu alipoitangazia dunia kupitia chombo kimoja cha habari cha kimataifa kwamba Mbowe ana kesi ya kujibu (inawezekana Mh Rais wetu hakupewa taarifa sahihi kutoka kwa wasaidizi wake juu ya dual/kesi hii). Matamko ya viongozi hawa, kwa maoni yangu yanaathiri sana mwenendo wa kesi hii.
Kwa maoni yangu, DPP ndiye mtu sahihi anayeweza kuokoa jahazi kwa kuifuta/kuiondoa kesi hii mahakamani kwa MASLAHI mapana ya Taifa.
 
Yaani Askari Mzima Kwa Anakiri Kuwa Kesi Ya Ugaidi ni Kesi Kubwa, Lakini Anasema Hakuona Umuhimu wa kutumia Audio recording au video kumuhoji Mtuhumiwa Angeuwawa Huko Ndani? Hivi hawa Askari wetu Hata Movie Tuu hawaangalii?

Askari amefanya kazi Dar es Salaam lakini kuna vituo Vya Polisi Havijui?

Askari amehamisha Mahabusu kuepuka mchanganyiko na Taarifa kuvuja, lakini hajui kama watuhumiwa walikuwa Isolated au laaa, sasa ulihamisha Wa Nini?

Umeona udhaifu wa shahidi vizuri kabisa. Anaulizwa kwanini baada ya kukiri makosa yake hawakumpeleka kwa mlinzi wa amani. Anajibu: hatukutaka kupoteza muda tulikuwa tunataka kuhakikisha ugaidi hautokei. Anasahau hata shahidi mwenzake aliulizwa kama kuna taarifa zozote kwa wakuu wa polisi wa maeneo lengwa, jibu hakuna. Kama walengwa (Sabaya) walifahamishwa kuhusu kutafutwa kwao kutendwa ubaya, hapana. Kama walitoa taarifa kwa kamati za usalama za wilaya au mkoa, hapana. Sasa sijui ni hawa watu wanne tu walikuwa na jukumu la kuzuia ugaidi nchi nzima???

Tuna polisi wa ajabu sana. Na bahati mbaya huyu shahidi nae amesimamishwa kazi kwa kubambikizia mtu kesi!!
 
Back
Top Bottom