Kesi ndogo ya Freeman Mbowe: Shahidi akamilisha ushahidi wake, Shahidi mwingine kuendelea tarehe 12/11/2021

haka kazee nako kanafiki kweli,Sasa si kakagombee uenyekiti wa chama,aachane na uaskofu tumkaribishe kwenye ulingo wa siasa!! hizo sare zinatumika vibaya sana!! au naye ni shahidi wa utetezi!!
Wewe kinachokuuma ni nini?
 
Umeona udhaifu wa shahidi vizuri kabisa. Anaulizwa kwanini baada ya kukiri makosa yake hawakumpeleka kwa mlinzi wa amani. Anajibu: hatukutaka kupoteza muda tulikuwa tunataka kuhakikisha ugaidi hautokei. Anasahau hata shahidi mwenzake aliulizwa kama kuna taarifa zozote kwa wakuu wa polisi wa maeneo lengwa, jibu hakuna. Kama walengwa (Sabaya) walifahamishwa kuhusu kutafutwa kwao kutendwa ubaya, hapana. Kama walitoa taarifa kwa kamati za usalama za wilaya au mkoa, hapana. Sasa sijui ni hawa watu wanne tu walikuwa na jukumu la kuzuia ugaidi nchi nzima???

Tuna polisi wa ajabu sana. Na bahati mbaya huyu shahidi nae amesimamishwa kazi kwa kubambikizia mtu kesi!!
Inaonyesha wazi hii ilikuwa ni timu maalum iliyokuwa imepewa jukumu la kummaliza Mbowe. Ni timu iliyokuwa inawajibika kwa mtu mmoja tu aliyeikabidhi kazi hiyo kwao.
Hii timu ilikuwa ipo nje ya taratibu zote za utendaji ndani ya jeshi la polisi, ndiyo maana hawa wengine wote hawakuhusishwa.

Ni yale yale ya Sabaya; kukabidhiwa kazi nje ya mkoa na wilaya anamofanyia kazi.
 
Ni kweli asingefuata sheria kwa hili legacy yake ingepotelea mbali.
Watu wanasoma vzr hii kesi huko mtaani na ingewashangaza km isinhekuwa.
Jaji anapaswa kujua kuwa yeye hayuko peke yake hapa duniani, ana familia mke na watoto. Ana ndugu zake na marafiki, jee haoni aibu anapo onekana mjinga na asiyetenda haki ana aibisha walio karibu naye mbele ya jamii?
Akiona patelea mbali basi ametawaliwa na ubinafsi kama yule jamaa wa Chato ambaye kaondoka na aibu kubwa aliyoiacha huku nyuma.
 
Siyo aoze mwenyewe peke yake, aoze na uzao wake upate ukoma.mabaya na mashimo anayo waombea wenzie yamrudie yy
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom