Kesi dhidi ya JamiiForums zaelekea hatua mpya: Asanteni watanzania, asante wana JF!

Mungu yu pamoja nanyi. Police wetu ni tatizo. Utakuta hata wale wanaomtonyaga Magu aende bandarini "kukamata" magari yaliongizwa nchini kwa janjajanja, police wetu huwa wana hamu kubwa ya kuwajua ili wawatie ndani
BAHATI Mbaya wanakuwa ni watu WA idara ya mkuu na sio wao, Mbona wangekoma
 
Hii ni sebule yetu ya mtandaoni kwa Tanzania.

Mola awasimamie
Haya yote anayopitia Melo na JF ni kwasababu yenu nyinyi CCM na Mfalme mwenyewe! Kipindi cha JK tulikua tuna jimwayamwaya tu humu ila sasa hivi tumekua wanyonge mpaka kufunguliana kesi za kijinga.

Ni ajabu kujifanya unamuhurumia Max wakati bado uko upande wa watesi wake.
 
Poleni sana. Nawatakieni kila lenye heri.

Binafsi, bado nashangaa ni kwa vipi hizo kesi zote tatu zimekuwepo mpaka sasa. Zilipaswa kunguka mapema. Hazina mashiko. Zinapoteza muda wa mahakimu/majaji wetu kushughulikia kesi za ufisadi na nyinginezo zenye maslahi kwa taifa.
 
chief Maxence Melo pole sana na pia hongera sana kwa ujasiri wa kusimamia unachokiamini....nimepata kitu, Mungu azidi kukupigania na najua hata kuacha, natumai pia na ww hautatuacha na sisi wanaJF.

ila hizo kesi mimi kama sijazielewa hivi....kwann polisi wanawataka waanzilishi wa hizo mada tajwa..!? kwanza naomba kujua....walishakili kama ni kweli au si kweli kuhusu hizo tuhuma?
 
HAO POLISI BADALA YA KUCHUNGUZWA MKWEPA KODI WANAMCHUNGUZA MTOA TAARIFA ZA UHALIFU ZA NINI? HAPOHAPO WANASEMA ETI RAIA MSHRIKIANE NA JESH LA POLIS KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU? SASA KAMA MTOA TAARIFA ANAANDAMWA UHALIFU HAUWEZ KWISHA.
 
Nchi hii ina watu wenye akili za ajabu sana! Viongozi kujidai mungu mtu! Usisahau huku mafia pwani kuna mkurugenzi mmoja juha .bwana erick mapunda aliwaweka baadhi ya watu ndani (polisi) ati anawalalamikia kwa kumwandika ubadhirifu wake humu jamii forum. Mambo yaliyosemwa ni mengi sana na mkurugenzi huyu/kama ni kweli hana uwezo wa kukanusha hata moja hana.
 
Maxence, binafsi nimemuunga mkono JPM kuanzia kampeni hadi juhudi zake mbalimbali. Lakini hili la uhuru wa vyombo vya habari na hasa hizi kesi za JF ni moja ya doa kubwa na issue iliyoturudisha chini wengine.

Msingi wa hizi kesi hauna faida kwa Taifa zaidi ya kuwakatisha tamaa watoa taarifa.

Bila Jamii Forums sehemu kubwa ya ufisadi unaopigwa vita leo isingekuwa na nguvu iliyo nayo leo. JPM anayo fursa kubwa ya kuwa Rais wa kihistoria akibadili vitu vinavyomchafua kama uhuru wa kutoa maoni au taarifa bila kubughudhiwa kama umetumia lugha ya staha na umesema ukweli.

Lazima tujenge taifa la wasema ukweli bila uoga na kila anayesema uongo au kutoa hoja kwa lugha zisizo za staha achukuliwe hatua kali.

Kila lakheri Cde Maxence Melo ....Tunafatilia kwa karibu kila nukta ....
Kama ni nia tu kweli anaonekana anayo ........ probably tatizo ni means!!

Anyway, binafsi bado sijawa convinced na juhudi zake nyingi mpaka sasa maana sijaona matunda. Kila anachokifanya hakielekei kufikia mwisho (haraka). Labda la wafanyakazi hewa....!!

Kwa hili la kuwakaba koo social media kama JF ndiyo linanifanya nijiulize mara 10 kama kweli kuna nia ya kupambana na rushwa ukichukulia kuwa JF wamekuwa ni ka whistle blowsers .............!! Whistle blowers huwa wanakuwa protected unless ni swala la usalama wa taifa ...!

Ushindi wa JF utakuwa ni ushindi wetu wote!! Kama JF watashindwa basi jukwaa la siasa ni bora lifungwe mpaka mwenyewe atakapotoka madarakani!!
 
Max melo sijakusahau kwenye maombi ya leo asubuh,
kwanza niseme hv wana JF whetever kama Max yeye kama yeye na staff member wake wanaweza kutujua au la!, sijui sana maswala ya ID adress sijui service provider na mengneyo au kama tunavyotumia ID fake, Email or whatever na kuhisi hatujulikani, yote hayo hatuna uhakika wao ndo wanajua, ila tunachopaswa kuamin ni kwamba MELO ANASUMBULIWA MAHAKAMANI KWA KUTUTETEA SISI, sasa jiulize je anaweza kutujua au hawezi, mimi na wewe hatuna uhakika na majibu yetu.

Kesi zote zinazomkabili Maxence Melo ananguva ya kushinda na mimi nina imani atashnda kwa sababu ana sehemu ya kusimamia kisheria(either iwe kwa sheria za Jf au yeyote ile inayompa haki) hivyo basi yupo ndani ya sheria na sheria inamlinda. Hivyo bas mimi na wewe pale tunapoandka thread au comment yoyote Jf tufanye hvyo tukijiaminisha ya kua tupo ndan ya sheria za jf(hatukiuki sheria za jf) ili bas kunapotokea mapambano kama haya Maxence Melo awe na sehemu ya kutusimamia sio unatoka nje ya sheria makusud halaf unajiaminisha et sitajulikana au [HASHTAG]#Maxence[/HASHTAG] Melo atakutetea, ndia pengne atafanya hvyo ila sio kigezo cha wewe kumswekesha rumande au kumsumbua kwenye kesi ya kukutetea wewe kwa kukiuka sheria makusud.

Kama si mara ya kwanza bas ya pili leo kuandika comment ya serias Jf na weng wananijua kwa utani, ila hili limenigusa sana japo simjui Melo na yeye hanijui nakupa pole brother na tupo nyuma yako. Live long jf

WHERE WE DARE TO TALK OPENLY.
Call me reyzzap.
 
Back
Top Bottom