Kesi dhidi ya JamiiForums zaelekea hatua mpya: Asanteni watanzania, asante wana JF!

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,867
2,000
1786429C-5824-427E-8317-29DC67D1A7AC.jpeg


Ndugu, jamaa na marafiki...

Nachukua fursa hii kukushukuruni kwa support ambayo mmetupa tangu kuanza kwa kesi 3 zinazoendelea mahakamani Kisutu tangu Disemba 19, 2016 hadi leo.

Kuanzia kesho, Disemba 05 hadi Disemba 07 (siku 3 mfululizo) kesi mbili zimewekwa kwenye ‘session’ ili zifike tamati. Mwisho wowote wa kesi hizi bado utakuwa ndio mwisho wenyewe, uwe mbaya au mzuri kwa upande wetu.

Na mnamo Disemba 18-20 (siku 3 mfululizo) kesi ya 3 itaunguruma katika Mahakama ya Kisutu.

Tangu nakamatwa mnamo Disemba 13, 2016 hadi leo, nimepata salaam nyingi za kunitakia kila la heri pamoja na timu yangu na wengine ambao hata hawakunijua physically walijikuta wakisimama nami katika kutetea uhuru wetu wa kujieleza na faragha ya watoa taarifa wenye nia njema!

Kesi tatu zenyewe ni hizi:
1) Kampuni ya Oilcom ilidaiwa kukwepa kodi bandarini, Jeshi la Polisi linataka taarifa za aliyeanzisha mjadala huo; sisi tunaamini chanzo cha taarifa hii kilitakiwa kulindwa na si kukamatwa bali Polisi wangefanya uchunguzi.
2) Kampuni ya CUSNA Investment ilidaiwa kufoji nyaraka bandarini na kuwatesa wafanyakazi wazalendo na kupendelea wageni toka nje ya nchi; Polisi walitaka kumkamata mwanzisha mada lakini sisi tunaamini chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema, tulitarajia iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa mhusika na kuelezwa kosa lake.
3) Kuwa na Tovuti ambayo ni .COM. Hapa sitii neno...

Yeyote aliyetuunga mkono (kwa namna yoyote) hata bila kujua tunapigania nini nasema ASANTE. Karibuni tujumuike pamoja Kisutu tarehe hizi hadi hatma ya kesi hizi.

Asanteni sana watanzania!
 

Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
19,918
2,000
Tuko pamoja Mkurugenzi kwa sasa Jamii forum pekee ndio chombo ambacho watu wako huru kuzungumza maoni yao bila kuvunja sheria za nchi.

Nawatakia kila la kheri katika mchakato wa kesi hizo na InshaAllah Mwenyezi Mungu atakuwa Upande wa Haki.
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
35,463
2,000
Big up Melo kwa kuwa nasubira ya hali ya juu katika hili sakata.

Hongereni sote wana JF kwa kupanza sauti kwa namna moja au nyingine na hatimae tunashinda hivi vikwazo na kuendelea vyema na Media yetu huru.
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
16,064
2,000
Maxence, binafsi nimemuunga mkono JPM kuanzia kampeni hadi juhudi zake mbalimbali. Lakini hili la uhuru wa vyombo vya habari na hasa hizi kesi za JF ni moja ya doa kubwa na issue iliyoturudisha chini wengine.

Msingi wa hizi kesi hauna faida kwa Taifa zaidi ya kuwakatisha tamaa watoa taarifa.

Bila Jamii Forums sehemu kubwa ya ufisadi unaopigwa vita leo isingekuwa na nguvu iliyo nayo leo. JPM anayo fursa kubwa ya kuwa Rais wa kihistoria akibadili vitu vinavyomchafua kama uhuru wa kutoa maoni au taarifa bila kubughudhiwa kama umetumia lugha ya staha na umesema ukweli.

Lazima tujenge taifa la wasema ukweli bila uoga na kila anayesema uongo au kutoa hoja kwa lugha zisizo za staha achukuliwe hatua kali.

Kila lakheri Cde Maxence Melo ....Tunafatilia kwa karibu kila nukta ....
 

Jiwedogo

JF-Expert Member
May 23, 2017
2,820
2,000
Mkuu...
Kumbe bado haujalala.....
Basi asante kwa taarifa na Mungu atusimamie ili kesi iweze kukwisha salama....
 

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,152
2,000
Mungu yuko upande wetu Maxence Melo.

Naweza kusema tu hilo maana kwa ushallow walionao vyombo vyetu vya dola ilibidi hata wapunguzwe kazini na JF iwe sehemu kuu ya kupata taarifa badala ya sasa wanavyoitumia kutafuta promotion! Shame! Yatakwisha tu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom