Kenyatta aihutubia Kenya msiba wa Magufuli, atangaza siku saba za maombelezo na bendera nusu mlingoti

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,816
Leo Rais wa Kenya amelihutubia Taifa la Kenya juu ya kifo cha Rais Magufuli na kutoa pole kwa mama Janeth Magufuli na watanzania.

Amesema anakumbuka ziara ya Rais Magufuli nchini Kenya na kwa pamoja wakafungua barabara inayoitwa 'Seven Bypass' na kwake binafsi anaikumbuka heshma kubwa aliyopatiwa na Rais magufuli kwa kumtembelea mama yake, mama Ngina Kenyatta nyumbani kwake na kumualika yeye Rais Kenyatta kumtembelea Chato na kupata nafasi ya kumsalimia mama yake na kulala kwa Rais Magufuli.

Kenyatta amesema amepoteza rafiki, kiongozi mwenzake na nchi ya Kenya inasimama imara na Tanzania katika wakati mgumu.

Kenyatta ameongea na makamu wa Rais, Mama Samia Hassan na kumpa pole za wakenya
 
Ni wakati wa kuinyanyua glasi na kumuangalia bwa Ndafu akiiva Polepole huku majonzi yakitugubika japo kinafki.
 
Kenya inaungana na watanzania kwa siku saba za maombolezo kwa heshima ya Rais wa zamani wa Tanzania John Pombe Magufuli.

IMG_20210318_093936.png
 
Kenyatta ameonesha vile inatakiwa kumstiri marehemu hata kama akiwa na mapungufu yake, nakumbuka pale alipolihutubia bunge la Kenya na kuwaasa viongozi wenzie wa nchi jirani wakae vizuri na wanasiasa wa upinzani baada ya Lema kukimbilia Kenya akihofia usalama wake.
 
siipendi CCM.

Ila shame upon yourself.
Sio wote ambao tutagalagala kwa kilio na kusaga meno wengine tutaomboleza kikwetu kwa glasi ya cognag na Ndafu huku tukiangalia kilele cha Kibo na Mawenzi

Tumelilia rohoni kwa muda mrefu wakati Sabaya akitutesa na kutupora Mali na Fedha hakuna alietusaidia
 
Sio wote ambao tutagalagala kwa kilio wengine tutaomboleza kikwetu kwa glasi ya cognag na Ndafu huku tukiangalia kilele cha Kibo na Mawenzi

Tumelilia rohoni kwa muda mrefu wakati Sabaya akitutesa na kutupora Mali na Fedha hakuna alietusaidia
Uko sahihi ndugu, acha Mungu aka deal nae huko huko.

Lakini hatufurahii kifo.

Ile mipira ya maji aliyokupora Sabaya ilirudi?
 
Lakini hatufurahii kifo.
Ama kwa hakika kila mtu atakufa
Kama siku Ile Risasi ingepasua mshioa mkubwa wa Damu wa Lissu tusingeruhusiwa hata kulia wala kumuombea kuna watu tunawajua walikesha wakinywa na kuimba
 
Ama kwa hakika kila mtu atakufa
Kama siku Ile Risasi ingepasua mshioa mkubwa wa Damu wa Lissu tusingeruhusiwa hata kulia wala kumuombea kuna watu tunawajua walikesha wakinywa na kuimba
Aisee, basi hatari sana.

Hongera kwa furaha ulionayo muda huu.
 
Wakenya wanaomboleza kifo cha Rais Magufuli. Rais w nchi jirani. Vijana wengi Wakenya walimuenzi kiongozi huyo. Hata jina lake (Magufuli) ni maarufu kwa nicknames hapa Kenya. Mwenyewe najua vijana wanne wameadopt hilo jina lake kama nickname yao.


Sisi hatuchukii wenzetu wa East Africa, ingawa ushindani ni mkubwa kati yetu na Watanzania kwenye mtandao.
 
Back
Top Bottom