Rais Samia atangaza siku 5 za maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth aliyekuwa Mkuu wa Nchi ya Tanganyika

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Rais Samia atangaza siku tano za maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II kilichotokea tarehe 8 Septemba, 2022.

Maombolezo hayo yataanza tarehe 10 Septemba hadi tarehe 14 Septemba.

Katika kipindi hicho bendera za Tanzania zitapepea nusu mlingoti, ikiwa ni pamoja na kwenye balozi zetu.

Ni jambo la hekima kidiplomasia kuonyesha kama nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola kuwa umeguswa na msiba huo wa kiongozi huyo mkuu wa Uingereza. Baadhi ya nchi zilizoshusha bendera yao nusu mlingoti ni pamoja na Nigeria, Kenya na Ghana.

Tanzania ni kati ya nchi 19 za Afrika zilizopo ndani ya Jumuiya ya Madola ambazo ziliwahi kuwa sehemu ya Ufalme wa Uingereza na zilipata uhuru ndani ya Jumuiya hiyo.

Kwa hiyo, Malkia Elizabeth II alikuwa moja kwa moja mkuu wa nchi, aliyewakilishwa ndani ya nchi na Gavana Mkuu.

Nchi hizo ni


Tanganyika (Tanzania) , 9 Desemba 1961 kama Ufalme - ikawa Jamhuri ya Tanganyika tarehe 9 Desemba 1962, Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili 1964, na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 29 Oktoba 1964.


Botswana , 30 Septemba 1966 kama Jamhuri

Cameroon , 11 Novemba 1995 kama Jamhuri

Gambia , 18 Februari 1965 kama Ufalme - ikawa Jamhuri tarehe 24 Aprili 1970

Ghana , 6 Machi 1957 kama Ufalme - ikawa Jamhuri ya 1 Julai 1960

Kenya , 12 Desemba 1963 kama Nchi - ikawa Jamhuri tarehe 12 Desemba 1964

Lesotho , 4 Oktoba 1966 kama Ufalme

Malawi , 6 Julai 1964 kama Ufalme - ikawa Jamhuri ya 6 Julai 1966

Mauritius , 12 Machi 1968 kama eneo - ikawa Jamhuri ya 12 Machi 1992

Msumbiji , 12 Desemba 1995 kama Jamhuri

Namibia , 21 Machi 1990 kama jamhuri

Nigeria , 1 Oktoba 1960 kama Ufalme - ikawa Jamhuri mnamo 1 Oktoba 1963 - kusimamishwa kati ya 11 Novemba 1995 na Mei 29, 1999

Rwanda , Novemba 28, 2009 kama Jamhuri

Seychelles , 29 Juni 1976 kama Jamhuri

Sierra Leone , 27 Aprili 1961 kama Ufalme - ikawa Jamhuri 19 Aprili 1971

Afrika Kusini , 3 Desemba 1931 kama Ufalme - aliondoka kuwa Jamhuri tarehe 31 Mei 1961, alijiunga na 1 Juni 1994

Swaziland , 6 Septemba 1968 kama Ufalme

Uganda , 9 Oktoba 1962 kama Ufalme - ikawa Jamhuri tarehe 9 Oktoba 1963

Zambia , 24 Oktoba 1964 kama Jamhuri

Zimbabwe , 18 Aprili 1980 kama Jamhuri - kusimamishwa tarehe 19 Machi 2002, iliondoka tarehe 8 Desemba 2003

Taarifa kamili,

IMG_20220910_002700.jpg
 
Sasa hii ni shobo!

Sisi Rais wetu Magufuli alipofariki Waingereza walitangaza siku ngapi za maombolezo?.

Sisi tumeshafiwa na viongozi wetu wakubwa tu akiwemo Mzee Kawawa , hatujawahi kutangaza siku tano za maombolezo , Huyu Malkia kwetu ni nani haswa hadi tumpe siku zote hizo?

Huu ni utumwa wa Fikra!

Halafu hii serikali mbona inatoa taarifa kwa Umma usiku wa manane, imekuwa serikali ya kichawi?
 
Waafrika ndio walewale

======

Rais Samia atangaza siku tano za maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II kilichotokea tarehe 8 Septemba, 2022.

Maombolezo hayo yataanza tarehe 10 Septemba hadi tarehe 14 Septemba.

Katika kipindi hicho bendera za Tanzania zitapepea nusu mlingoti, ikiwa ni pamoja na kwenye balozi zetu.

20220910_001905.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Hayati Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, kilichotokea tarehe Sept. 8 2022

Maombolezo hayo yataanza Septemba 10, 2022 hadi tarehe Septemba 14, 2022.

Katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye balozi zake.

Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na Uingereza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa mtawala wao.View attachment 2351945
 
Sasa hii ni shobo!

Sisi Rais wetu Magufuli alipofariki Waingereza walitangaza siku ngapi za maombolezo?.

Sisi tumeshafiwa na viongozi wetu wakubwa tu akiwemo Benjamin Mkapa, Sokoine , hatujawahi kutangaza siku tano za maombolezo , Huyu Malkia kwetu ni nani haswa hadi tumpe siku zote hizo?

Huu ni utumwa wa Fikra!

Halafu hii serikali mbona inatoa taarifa kwa Umma usiku wa manane, imekuwa serikali ya kichawi?
Wana support bajeti yenu kiasi gan? Unaishi kwa kulishwa na una jeuri huna hata unga wa kukutosha mwezi bila mzungu kuweka jasho lake unahoji? Jitegemee then peleka jeuri baadaye!

Magu aliwaosha mind zenu mkajua hamna kitu mnamtegemea mzungu wkt bajeti yake zaidi ya nusu anaomba na anazuga mmelipa kodi!

Anyway hii ni taratibu ya kidoplomasia Tanzania ni nchi ndani ya Commonwealth Kama unajua maana yake haiwezi kujitenga kwa kuwe wewe unataka huko ikungulyabashashi.
 
Rais Samia atangaza siku tano za maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II kilichotokea tarehe 8 Septemba, 2022.

Maombolezo hayo yataanza tarehe 10 Septemba hadi tarehe 14 Septemba.

Katika kipindi hicho bendera za Tanzania zitapepea nusu mlingoti, ikiwa ni pamoja na kwenye balozi zetu.

Taarifa kamiliView attachment 2351886
Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Madola ambayo inaziunganisha nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza na nchi zilizokuwa makoloni yake.

Ni jambo la hekima kidiplomasia kuonyesha kama nchi mwanachama kuwa umeguswa na msiba huo wa kiongozi huyo mkuu wa Uingereza. Tanzania inapokea misaada mingi ya kifedha kutoka kwa nchi hii.

Kwa hiyo ni vyema kuwadhihirishia kuwa tupo pamoja nao katika kipindi wanapoomboleza kifo cha kiongozi mkuu wa taifa lao. Natambua si Tanzania tu ambayo itashusha bendera zake nusu mlingoti, bali mataifa yaliyo mengi ikiwemo nchi zote zilizo wanachama wa Jumuiya ya Madola.
 
Back
Top Bottom