Kenya yapata idhini ya kufanya majaribio ya chanjo ya Corona kwa binadamu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,859
2,000
35855744a72a5fdcf873dc688ba51b81

WANASAYANSI nchini Kenya wameungana na wenzao wa Kimataifa katika juhudi za kutafuta chanjo ya ugonjwa wa Covid-19, kwa kufanyia majaribio dawa tatu. Majaribio ya chanjo itafanyiwa binadamu ili kubaini ikiwa dawa hizo zinaweza kutibu ugonjwa huo.

Lakini Je dawa hizo ni zipi?

Watafiti wamekuwa mbioni kupata idhini ya kufanyia majaribio ya dawa aina tatu ikiwa ni pamoja na:
  • Remdesivir, ambayo iliidhinishwa na Marekani kama dawa ya dharura ya kutibu Covid-19.
  • Dawa ya kutibu malaria ya hydroxychloroquine.
  • Lopinavir/ritonavir, ambayo pia inatumiwa na wagonjwa wa HIV.
Kwa mujibu wa Gazeti la Nation nchini Kenya mtafiti mkuu katika uchunguzi huo Dkt Loice Achieng Ombajo, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Kuambukiza katika Hospitali ya kitaifa ya Kenyatta amesema kwamba kufikia sasa hakuna tiba ya Covid-19 inayopewa mgonjwa.

Badala yake ,wagonjwa wanasadiwa kukabiliana na dalili zinazoonekana kama vile kuwa na homa kali na kuumwa na videnda vya koo.
35855744a72a5fdcf873dc688ba51b81-1

Kenya imefika wapi katika majaribio hayo?
”Tuko katika awamu amabapo hatuwezi kubaini moja kwa moja nini kinafanya kazi,” alisema Dkt Loice Achieng Ombajo. Aliongeza kuwa katika majaribio ya tiba wagonjwa wengi wanashirikishwa bila mpangilio maalu lakini wote wanapewa dawa tofauti na wenzao.

”Kuna uwezekano wa dawa moja ikafanya kazi lakini wataalamu wanatakiwa kufuatilia kwa makini mienendo ya mgonjwa,” alisema katika mahojiano na gazeti la Nation.

Kufikia sasa Dkt Ombajo, na wenzake wamepata idhini kutoka kwa kamati ya maadili ya Chuo Kikuu cha Nairobi na mapendekezo yao kuchunguzwa na bodi ya dawa nchini Kenya.

Watafiti hao kwa sasa wanasubiri tamko la mwisho kutoka kwa bodi hiyo na Baraza la kitaifa la Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (NACOSTI).

Hatua nyingine muhimu kwa mujibu wa watalamu hao, ni kuhamasisha umma kuhusu majaribio hayo ya tiba kabla ya watu ”kufanya maamuzi” ikiwa wanataka kushiriki katika zoezi.

Dkt Ombaja anasema kabla ya mtu kushiriki katika majaribio ya tiba wale wanaoendesha shughuli hiyo lazima watoe maelezo kwa muhusika.

”Kwanza anaambiwa huu ndio utafiti tunaofanya, hizi ndizo dawa tunazofanyia majaribio, Hii ndio sababu tunazifanyia majaribio, na hivi ndivyo tutakavyokulinda. Ukiwa mgonjwa tuna bima ambayo itakuhudumia.

Je unakubali kusiriki? Na endapo mhusika atakubali anapewa fomu ya kutoa idhini. Kisha tunafanya tunafanya majaribio. Ni mchakato mrefu,” alisema Dkt Ombajo.

Wiki moja iliyopita Watafiti kutoka nchini Uingereza walisema wanafikiria kufanyia majaribio chanjo ya virusi vya corona nchini Kenya. Tangazo hilo lilizua ghadhabu miongoni mwa Wakenya ambao walitumia mitandao ya kijamii kupinga hatua hiyo.

Shirika la Afya duniani pi ailiwahi kuyaonya mataifa ya Ulaya kwamba bara la Afrika sio uwanja wa majaribio ya chanjo.

Mkuu wa Shirika hilo Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus alilaani kauli alizoziita za “kibaguzi” kutoka kwa madaktari wawili wa Ufaransa ambao walitaka chanjo ya virusi vya corona kufanyiwa majaribio barani Afrika.

“Afrika sio na haitakuwa uwanja wa majaribio ya chanjo yoyote,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus.
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,443
2,000
Hizi sasa ndio taarifa ambazo mchawi Geza Ulole kwa uelewa wake finyu amezigeuza zikawa eti vaccine za mabeberu, kama wanakwaya wa Lumumba wanavopenda kuwaita, zimeanza kufanyiwa majaribio nchini Kenya. Tafsiri umeletewa kwa kiswahili mzee, ili upunguze hizi aibu ndogo ndogo.

WHO Kenya: coronavirus vaccine trials ongoing in the country - JamiiForums Wanasayansi wote wanaoijielewa duniani wameungana kwenye hizi Solidarity Trials za WHO.

Tusipangiane tafadhali, nyie endeleeni na usanii wenu wa kupima sampuli kutoka kwa mbuzi na mapapai.
 
Babu Kingo

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
431
250

AISEE WE DOGO, HEBU KUWA MSTAARABU NA TUMA POSTS ZENYE MAANA TAFADHALI. KAMA HAUNA KITU CHA KUTUMA SIO LAZIMA KUTUMA BORA UKAE KIMYA TU.
 
PAGAN

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
10,211
2,000
Mimi bado sijaelewa hapo kwenye kupata idhini, kwani Marekani na Uingereza wanavyofanya majaribio walipewa idhini?
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,443
2,000
AISEE WE DOGO, HEBU KUWA MSTAARABU NA TUMA POSTS ZENYE MAANA TAFADHALI. KAMA HAUNA KITU CHA KUTUMA SIO LAZIMA KUTUMA BORA UKAE KIMYA TU.
Babu ungefata ushauri wako na ubaki kimya tu ingependendeza zaidi. Maanake kando na ku'tuma' CAPS kinachosalia kwenye hii comment yako ni utumbo.
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
6,562
2,000
Hizi sasa ndio taarifa ambazo mchawi Geza Ulole kwa uelewa wake finyu amezigeuza zikawa eti vaccine za mabeberu, kama wanakwaya wa Lumumba wanavopenda kuwaita, zimeanza kufanyiwa majaribio nchini Kenya. Tafsiri umeletewa kwa kiswahili mzee, ili upunguze hizi aibu ndogo ndogo.

WHO Kenya: coronavirus vaccine trials ongoing in the country - JamiiForums Wanasayansi wote wanaoijielewa duniani wameungana kwenye hizi Solidarity Trials za WHO.

Tusipangiane tafadhali, nyie endeleeni na usanii wenu wa kupima sampuli kutoka kwa mbuzi na mapapai.
Bado hamjakoma tuu, mara ya mwisho michanjo ya uzazi wa mpango iliuwa kizazi cha wanawake wenyu.
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,323
2,000
Kwahiyo Africa ndio tumekubali kuwa uwanja wa utafiti wa chanjo?kwa jinsi hii hawa wazungu sio watu wa kuwaendekeza kabisa.Hii inamaana kama itakuwa na madhara kwa binadamu wao wanakuwa wamebaki salama...
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
6,562
2,000
halafu wananchi hawalipwi kitu wanaambiwa ati ni volunteer exercice wakati politicians hujukua hizo fedha!
Mwalimu hakukosea aliposema, man eating man society, hawa jamaa ni mafia hasa.
Kwahiyo Africa ndio tumekubali kuwa uwanja wa utafiti wa chanjo?kwa jinsi hii hawa wazungu sio watu wa kuwaendekeza kabisa.Hii inamaana kama itakuwa na madhara kwa binadamu wao wanakuwa wamebaki salama...
Ni dharau za wazi lakini wao wanakubali.
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,443
2,000
Bado hamjakoma tuu, mara ya mwicho michanjo ya uzazi wa mpango iliuwa kizazi cha wanawake wenyu.
Umeamua kubadilisha mada kwa kuzungumzia ile chanjo ambayo nchi zote ukanda huu, Tz ikiwemo, ziliipokea bila pingamizi? Nchi ya Kenya tu na wataalamu kutoka Kenya ndio waliibuka na uchunguzi ambao ulionyesha kwamba baadhi ya chanjo hizo zilikuwa na 'traces' za dawa za kupanga uzazi. Sijui wataalamu wenu wa kupima mapapai na mbuzi walikuwa wapi enzi hizo.
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
6,562
2,000
Umeamua kubadilisha mada kwa kuzungumzia ile chanjo ambayo nchi zote ukanda huu, Tz ikiwemo, ziliipokea bila pingamizi? Nchi ya Kenya tu na wataalamu kutoka Kenya ndio waliibuka na uchunguzi ambao ulionyesha kwamba baadhi ya chanjo hizo zilikuwa na 'traces' za dawa za kupanga uzazi. Sijui wataalamu wenu wa kupima mapapai na mbuzi walikuwa wapi enzi hizo.
Ni lini tulipokea chanjo hizo, sisi huwa tunayakataa machanjo chanjo ya ajabu. Hata juzi juzi tuu hapa tulikataa ma GMO ya Billy. Tz ni nchi makini sana ndiyo maana hata al shaban hawaigusi.
 
Mbekenga

JF-Expert Member
Jun 14, 2010
1,748
2,000
Watu walifikiri ndege imenyofolewa viti kupeleka zawadi ya maua kumbe ilienda kubeba mzigo wa Bill Gate. Hivi hamkujiuliza Trump alivyompigia simu Prezda wenu?
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,443
2,000
Mwalimu hakukosea aliposema, man eating man society, hawa jamaa ni mafia hasa. Ni dharau za wazi lakini wao wanakubali.
Aisee, hapo awali nilidhani tatizo ni lugha ila baada ya kuletewa tafsiri kwa kiswahili mnaendelea kudhihirisha kwamba mna uelewa finyu kupindukia. Wanasayansi wa Kenya ndio wamepata idhini ya WHO(Solidarity Trials), ya kufanya majaribio ya tiba na chanjo ya COVID-19 kwa binadamu nchini Kenya. KEMRI, KAVI-ICR na wanasayansi kutoka Kenya ndio watafanya majaribio hayo. Sio wale 'mabeberu' wenu. Tiba zinazofanyiwa majaribio sio dawa au chanjo yoyote kutoka kwa 'mabeberu'. Dawa hizo tatu zimekuwepo tangia zamani, Remdesevir ni 'anti-viral' ambayo huwa inatumiwa kuzuia maambukizi ya virusi, sanasana kwa wahudumu wa afya. Hydroxychloroquine ni ya kutibu malaria na Lopinavir/Ritonavir kwa HIV Covid-19: Kenya set to begin clinical trial for three possible
 
Bantugbro

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
4,441
2,000
Hawa humu ndani unadhani wataelewa kitu..
Watu walifikiri ndege imenyofolewa viti kupeleka zawadi ya maua kumbe ilienda kubeba mzigo wa Bill Gate. Hivi hamkujiuliza Trump alivyompigia simu Prezda wenu?
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,443
2,000
Ni lini tulipokea chanjo hizo, sisi huwa tunayakataa machanjo chanjo ya ajabu. Hata juzi juzi tuu hapa tulikataa ma GMO ya Billy. Tz ni nchi makini sana ndiyo maana hata al shaban hawaigusi.
Hebu nipe orodha ya chanjo ambazo zimetengenezewa Tz, utaalamu huo hamna, viwanda navyo vya madawa hamna. Hata pain killer tu mnanunua kutoka Kenya. Chanjo zote za tetenus ambazo zilikuwa zimesambazwa ukanda huu wote zilikuwa na viini vya dawa za kupanga uzazi. Nchi ya Kenya ndio iliumbua njama yao hiyo baada ya kuzifanyia utafiti. Nchi za LDC hapa Afrika kama Tz huwa mnapewa misaada ya chanjo hizo kwasababu bajeti zenu za sekta ya afya huwa hazitoshi mboga. Ndio maana wataalamu wenu wa kupima mapapai hawakuwa na ufahamu wala ubavu wa kuuliza maswali. Kwa taarifa yako Kenya pia hatujakubali GMO.
 
Ramthods

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
515
250
Title ya hii thread ni misleading. Hizo sio chanjo, hizo ni dawa za kuboresha "recovery time" kwa wagonjwa wa Covid-19.
  • Remdesivir, ni dawa ambayo ilitengnezwa kwa ajili ya ugonjwa wa Ebola, na pia ilishafanyia majaribio kwa ugonjwa wa SARS/MERS
  • Hydroxychloroquine ni dawa kwa ajili ya tiba ya malaria
  • Combination ya Lopinavir na ritonavir inatumika kwa ajili ya kupunguza makali ya HIV
Kuziita hizi "chanjo" ni aidha kupotosha watu kwa makusudi, au inaonekana mtoa mada huwezi tofautisha kati ya chanjo na tiba.

Titile yako ingetakiwa kuwa: Kenya yapata idhini ya kufanya majaribio ya dawa ya Corona kwa binadamu

Kupata idhini ni lazima, sababu dawa kama Remdesivir ni serikali ya marekani ndio inaamua iende wapi na nani apate. Bila idhini yao, huwezi kupewa. Ni dawa inayotengenezwa na kampuni ya marekani inayoitwa Gilead Sciences, na imepewa kibali cha dharura na mamlaka ya dawa ya marekani kwa ajili ya tiba ya Covid-19 kwa wagonjwa walio na hali mbaya.
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
6,562
2,000
Hebu nipe orodha ya chanjo ambazo zimetengenezewa Tz, utaalamu huo hamna, viwanda navyo vya madawa hamna. Hata pain killer tu mnanunua kutoka Kenya. Chanjo zote za tetenus ambazo zilikuwa zimesambazwa ukanda huu wote zilikuwa na viini vya dawa za kupanga uzazi. Nchi ya Kenya ndio iliumbua njama yao hiyo baada ya kuzifanyia utafiti. Nchi za LDC hapa Afrika kama Tz huwa mnapewa misaada ya chanjo hizo kwasababu bajeti zenu za sekta ya afya huwa hazitoshi mboga. Ndio maana wataalamu wenu wa kupima mapapai hawakuwa na ufahamu wala ubavu wa kuuliza maswali. Kwa taarifa yako Kenya pia hatujakubali GMO.
Tanzania hatuna matatizo ya uzazi, fertility rate yetu ni zaidi ya 5% nyinyi ni 3%.
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
21,945
2,000
Fomu za kusajiri kwa ajili ya haya majaribio ziko wapi, nipo tayari kwa usaili, naomba kuelekezwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom