Kenya yapata idhini ya kufanya majaribio ya chanjo ya Corona kwa binadamu

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
779
1,000
35855744a72a5fdcf873dc688ba51b81


WANASAYANSI nchini Kenya wameungana na wenzao wa Kimataifa katika juhudi za kutafuta chanjo ya ugonjwa wa Covid-19, kwa kufanyia majaribio dawa tatu. Majaribio ya chanjo itafanyiwa binadamu ili kubaini ikiwa dawa hizo zinaweza kutibu ugonjwa huo.

Lakini Je dawa hizo ni zipi?

Watafiti wamekuwa mbioni kupata idhini ya kufanyia majaribio ya dawa aina tatu ikiwa ni pamoja na:
  • Remdesivir, ambayo iliidhinishwa na Marekani kama dawa ya dharura ya kutibu Covid-19.
  • Dawa ya kutibu malaria ya hydroxychloroquine.
  • Lopinavir/ritonavir, ambayo pia inatumiwa na wagonjwa wa HIV.
Kwa mujibu wa Gazeti la Nation nchini Kenya mtafiti mkuu katika uchunguzi huo Dkt Loice Achieng Ombajo, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Kuambukiza katika Hospitali ya kitaifa ya Kenyatta amesema kwamba kufikia sasa hakuna tiba ya Covid-19 inayopewa mgonjwa.

Badala yake ,wagonjwa wanasadiwa kukabiliana na dalili zinazoonekana kama vile kuwa na homa kali na kuumwa na videnda vya koo.
35855744a72a5fdcf873dc688ba51b81-1

Kenya imefika wapi katika majaribio hayo?
”Tuko katika awamu amabapo hatuwezi kubaini moja kwa moja nini kinafanya kazi,” alisema Dkt Loice Achieng Ombajo. Aliongeza kuwa katika majaribio ya tiba wagonjwa wengi wanashirikishwa bila mpangilio maalu lakini wote wanapewa dawa tofauti na wenzao.

”Kuna uwezekano wa dawa moja ikafanya kazi lakini wataalamu wanatakiwa kufuatilia kwa makini mienendo ya mgonjwa,” alisema katika mahojiano na gazeti la Nation.

Kufikia sasa Dkt Ombajo, na wenzake wamepata idhini kutoka kwa kamati ya maadili ya Chuo Kikuu cha Nairobi na mapendekezo yao kuchunguzwa na bodi ya dawa nchini Kenya.

Watafiti hao kwa sasa wanasubiri tamko la mwisho kutoka kwa bodi hiyo na Baraza la kitaifa la Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (NACOSTI).

Hatua nyingine muhimu kwa mujibu wa watalamu hao, ni kuhamasisha umma kuhusu majaribio hayo ya tiba kabla ya watu ”kufanya maamuzi” ikiwa wanataka kushiriki katika zoezi.

Dkt Ombaja anasema kabla ya mtu kushiriki katika majaribio ya tiba wale wanaoendesha shughuli hiyo lazima watoe maelezo kwa muhusika.

”Kwanza anaambiwa huu ndio utafiti tunaofanya, hizi ndizo dawa tunazofanyia majaribio, Hii ndio sababu tunazifanyia majaribio, na hivi ndivyo tutakavyokulinda. Ukiwa mgonjwa tuna bima ambayo itakuhudumia.

Je unakubali kusiriki? Na endapo mhusika atakubali anapewa fomu ya kutoa idhini. Kisha tunafanya tunafanya majaribio. Ni mchakato mrefu,” alisema Dkt Ombajo.

Wiki moja iliyopita Watafiti kutoka nchini Uingereza walisema wanafikiria kufanyia majaribio chanjo ya virusi vya corona nchini Kenya. Tangazo hilo lilizua ghadhabu miongoni mwa Wakenya ambao walitumia mitandao ya kijamii kupinga hatua hiyo.

Shirika la Afya duniani pi ailiwahi kuyaonya mataifa ya Ulaya kwamba bara la Afrika sio uwanja wa majaribio ya chanjo.

Mkuu wa Shirika hilo Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus alilaani kauli alizoziita za “kibaguzi” kutoka kwa madaktari wawili wa Ufaransa ambao walitaka chanjo ya virusi vya corona kufanyiwa majaribio barani Afrika.

“Afrika sio na haitakuwa uwanja wa majaribio ya chanjo yoyote,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus.
Hii habari ina walakini mkubwa.
Kichwa cha habari ni kuhusu chanjo pamoja na picha inaonyesha chanjo.
Lakini majaribio ni dawa/tiba za kawaida tuu wala sio chanjo.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,313
2,000
May 7, 2020
Dar es Tanzania

Ndege rasmi ya Rais yatua na mzigo wa msaada wa dawa toka serikali ya Madagascar na waziri wa Mambo ya Nje Mh. Prof. Palamagamba Aidan John Kabudi kuwa mmoja wa waTanzania wa mwanzo kugumia dawa hiyo adhimu ya kiAfrika ya kupambana na coronavirus wanaosababisha gonjwa la hatari la Covid-19
 

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,443
2,000
May 7, 2020
Dar es Tanzania
Ndege rasmi ya Rais yatua na mzigo wa msaada wa dawa toka serikali ya Madagascar na waziri wa Mambo ya Nje Mh. Prof. Palamagamba Aidan John Kabudi kuwa mmoja wa waTanzania wa mwanzo kugumia dawa hiyo adhimu ya kiAfrika ya kupambana na coronavirus wanaosababisha gonjwa la hatari la Covid-19
Mnapoteza muda wenu, hii dawa ya CVO kutoka Madagascar inatibu malaria tu, sio Corona. Nchi nyingi za Afrika zimeigomea baada ya utafiti kutoka kwa WHO na Africa CDC pia kuonesha kwamba
haiwezi ikatibu Corona. Nchi mbili tu Afrika ndio zimeikubali, Guinea na Tz. Jana kule magharibi ECOWAS(nchi 15) wameikana hadharani baada ya nchi ya Guinea kuiagiza. ECOWAS 'rejects' COVID-Organics, Madagascar's untested virus cure | Africanews
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom