Kenya mshahara wa rais uko wazi

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,252
113,647
Jana tume ya mishahara [ya watumishi wa umma] ya Kenya imetangaza viwango vipya vya mishahara ya viongozi wa umma.

Viwango hivyo vipya ni vidogo kidogo kulinganisha na viwango vya sasa.

Kwa hiyo, rais mpya ajaye baada ya uchaguzi wao wa mwezi ujao ataanza kupokea huo mshahara mpya.

Na kama Uhuru Kenyata akishinda basi ina maana mshahara ataopokea kuanzia mwezi Septemba utakuwa ni pungufu kuliko apatao sasa.

Tofauti na huku kwetu ambapo kuna wapumbavu ukiulizia mshahara wa rais wanakwambia 'mshahara wa mtu ni siri'.

 

Pendekeza na huku maana huku ndio tuna rais mzalendo kuliko Kenya. Huku ndio hilo wazo litapita kirahisi maana hii ni serekali inayojali wanyonge. Huenda ww ukasikilizwa maana sasa hivi huwa unawatetea sana, sisi tunapinga kila kitu hatutasikikizwa.
 
Kwani si mlishatajowa na muhusika mshahara mwenyewe mshahara wake enyi kizazi cha sanaa na makaratasi..au hamkuambia tena kabla hata ya kenyata??
 
Nchi ya kizungu?

Hapana.

Ni ya walau wanaojielewa.

Kujielewa hakuna cha uzungu.
Nyani, kumbuka kipindi kile yupo chato likizoni, alisema akija atataja mshahara wake, tulisha sikia tena? Na watu wanasema mshahara wa Rais Tz ni mkubwa sana. Nadhani kwa Afrika Tz ni ya tatu kwa mshahara mnono wa Marais. Ngoja tuendelee na uzalendo huu tuliouanzisha
 
Huku ile salary slip ya yule jamaa ilipotelea clouds 360 ambako aliwatumia wakati anatekeleza uongo wake

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom