Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 21,854
- 26,091
Nimeitoa huko kwa mdadisi na aliyekuwa mshiriki wa ujenzi wa katiba ya kenya,
::::::::::::::::::::::::::::::
KENYA INATEKETEA KISA KATIBA MPYA: NI FURSA NA SOMO KWA TANZANIA
Ni dhahiri polisi wa kawaida wamezidiwa. Sasa jeshi limelazimika kuingia kupambana na wanaojiita GenZ.
Bahati niliteuliwa kama mshauri Kwa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Cha Kenya (COTU -K) anachoongoza Brother Francis Atwoli. Ni wakati wa mchakato wa kutunga kilichoitwa katiba mpya. Wafanyakazi walishirikishwa vya kutosha. Hivyo ITUC na ILO wakanipa kibarua Cha kushauri. Vikao vingi tulifanya pale Mombasa.
Nilipopitia rasimu nilistaajabu kuona mambo ya hovyo ndani ya rasimu. Nitapitia machache:
1. Pendekezo kwamba kima cha chini cha mshahara (minimum living wage) kitamkwe kwenye katiba. Wenyewe wakidhani ni jambo zuri mno mshahara wa kima cha chini kulindwa kikatiba. Niliwaeleza huu ni ujinga. Mshahara ni suala la "econometrics". Sio a political issue.
2. Majaji wasailiwe na wananchi kabla ya kuajiriwa kupitia runinga. Wao wakiamini kuwa itazuia majaji kula rushwa au kuendelea serikali. Niliwaeleza upumbavu uliopo. Kwanza jaji hapimwi Kwa kigezo kimoja tu. Pili itawezekana vipi raia ambaye hata kuhesabu mpaka 5 hawezi amsaili jaji? Je baada ya kumsaili nani ataamua huyu aajiriwe yule ailsiajiriwe? n.k.
3. Uhuru wa kuandamana na kukusanyika usio na masharti. Niliwaeleza Nini kitatokea uhuru aina hii ukitolewa na katiba. Ndicho kinatokea Sasa.
4. Kuwe na wabunge wanaowakilisha wafanyakazi. Hili niliwarejesha Kwa Uganda, Tanzania, Cameroon na Cote D'Ivoire. Wafanyakazi huko walikuwa wanadai ubunge huo ufutwe hauwasaidii. Tanzania tulifanikiaa kujiondoa kwenye jumuia za chama na ndio JUWATA ikafa ikaja TFTU, baadae OTTU na Sasa TUCTA. Wafanyakazi walikuja kugundua wawakilishi wao walijali matumbo Yao. Pia ukitoka uamuzi unaowaumiza wanashindwa kupinga Kwa kuwa wawakilishi wao walishiriki kutoa uamuzi.
5. Kuruhusu maofisa na watendaji kushitakiwa binafsi hata wanapofanya kosa wakati wanatekeleza majukumu waliyopewa na katiba. Niliwaambia hii itafanya watumishi wa serikali haswa wa vyombo vya Dola kuzembea. Ndio maana Sasa unaona kisichana kinatikisa makalio mbele ya askari mwenye rungu na bunduki. Watumishi aina hii wanatakiwa waadhibiwe na mahakama ya kijeshi tu.
Nimetaja mifano michache lakini kusema kweli katiba ya Kenya ni mbovu mno na ndio chanzo cha haya machafuko . Wanatuambia ni katiba nzuri tuiige hawajui wasemalo. Nao Wana mawazo na matendo ya kina Shakira, Boniface Mwangi, Martha Karua, Kalonzo na Odinga.
Kuvurugika nchi ndio wanapata maslahi Yao
Tukatae. Tusiichezee katiba. Tusifanye reforms kwa mashinikizo.
Mwisho: nyumba ya jirani ikungua wee Jenga nyingi. Wapangaji wapo. Hakuna mtalii ataenda Kenya sasa. Wawekezaji wanaanza kuhama. Huu ndio muda wetu kuchangamka.
Halafu tuimarishe ulinzi mpakani. Wakimbizi wako njiani wanakuja.
Mwishoooo: tuendelee kudhibiti wakorofi wetu kwa nguvu na ari mpya. Bora walie sasa kuliko kuacha waanze kuchoma majengo na mali za watu
Nakazia tuwachape viboko tu,wanaojibidisha kutupeleka katika majanga ya aina hii,si kila jambo nilakuiga.
Nilisema, na narudia maneno ya wazee: "huwezi kuzuia kuhara kwa kidole kimoja". Hii ndio Kenya, wanaiteketeza huku wakihisi wapo sahihi na ni wasomi wa grade 1. Fikiria hii ni Magunas Supermarket (ipo Makutano, Meru). Vijana wanabomoa, wanachukua/kuiba na kuchoma mali za wafanyabiashara au serikali moto. Wasipodhibitiwa, mzigo wa shida unasambaa Afrika ya Mashariki, hasa hasa sisi majirani wa pande nyingi. Leo Kenya isipotawalika, hata sisi tunaumia kwa kiasi kikubwa sana.
#wanachimba highways yao iliyojengwa Kwa mabilioni ya Dollar