Kenya ilipigania uhuru wake. Tanzania ilipewa uhuru bure na Mbeberu

Tony254

JF-Expert Member
May 11, 2017
16,017
16,427
Watanzania huwa wana kiburi ya hali ya juu sana maana wanaamini kuwa wao ndio waliikomboa Afrika kutoka kwa Mabeberu. Ukiona waziri wao akifoka jinsi waliikomboa Afrika hadi mate inamtoka mdomoni na mishipa kuvimba kichwani ndio utajua kwamba hii propaganda ya CCM ni nzito sana.

Ukweli wa mambo ni kuwa nchi chache sana hapa Afrika zilipigania uhuru wao. Nchi zilizopigania uhuru kwa kumwaga damu hazijapita 12 hapa Afrika. Nitataja baadhi yao: Kenya, Guinea Bissau, Mozambique, Zimbabwe, South Africa, Angola, Algeria na zingine chache. Nchi nyingi za Afrika zilipewa uhuru wao bure bila vita. Tanzania ni mojawapo ya nchi zilizopewa uhuru bure kabisa na beberu bila Watanzania kuingia msituni kumenyana na Mzungu. Hamkumwaga damu ili kupigania uhuru wenu.

Kama nyie ni wakombozi wa Afrika mbona hamkuikomboa Kenya kutoka kwa mabeberu? Mabeberu waliua Wakenya karibia laki moja wakati wa state of emergency 1952 wakati wanapigana na Maumau. Wamama na watoto wakapelekwa kwenye concentration camp ambapo wengi walikufa kwa njaa. Wanaume walipelekwa gerezani na kuteswa na kuuawa.

Hata nchi ya Uingereza imeomba msamaha kwa ushetani waliotufanyia na kutoa pesa kama fidia. Mbona nyie hamkutusaidia? Mbona sisi tulijipigania uhuru wenyewe na kufa kwa wingi ili tupate uhuru wetu? Hakuna nchi yoyote ya Afrika iliyotusaidia kupata Uhuru. So nyamazeni. Hata hamkupigania uhuru wenu mlipewa bure. We don't owe you anything. Hatuna deni lenu maana nyie hamkutusaidia.
 
Mkuu historian umesoma wapi?
Kenya, Guinea Bissau, Mozambique, Zimbabwe, South Africa, Angola, Algeria ...huku more Tanzania ilipeleka vijana...haya hiyo maumau unayoongelea vijana wa TANU walikuja kuwasaidia.
Tanzania haikusaidia Kenya kupata uhuru.
 
Ukiwa mjinga unauliwa kama kuku wa kufugwa ila ukitumia akili na maarifa unabeba chochote bila kutumia nguvu za kimwili
Kenya was a settler economy. Mabeberu pamoja na familia zao walikuwa wanaishi Kenya kwa wingi lakini hawakuwa wanaishi Tanzania kwa wingi. Kwa hivyo beberu alikataa kuondoka Kenya bila vita maana alikuwa na shamba kubwa yenye rutuba hapa Kenya. Sasa alisema haondoki bila vita. Lakini beberu hakuwa na shamba wala kitu chochote cha maana hapo Tanzania so aliwapa uhuru maana Tanzania ilikuwa useless kwake.
 
Kenya was a settler economy. Beberu walikuwa wanaishi Kenya kwa wingi lakini hawakuwa wanaishi Tanzania kwa wingi. Kwa hivyo beberu alikataa kuondoka Kenya bila vita maana alikuwa na shamba kubwa yenye rutuba hapa Kenya. Sasa alisema haondoki bila vita. Lakini beberu hakuwa na shamba wala kitu chochote cha maana hapo Tanzania so aliwapa uhuru maana Tanzania ilikuwa useless kwake.
Hahaha imekuuma hadi umeifungulia thread. Nyie mlipewa uhuru wa karatasi ila bado wanawatawala hadi sasa hivi mzungu akikohoa tu mnaufyata bado hampo huru vibaraka wa mabeberu nyie.
 
Ni ukweli kabisa, kilichoipumbaza Tanzania ni uhuru wa kupewa bila kutumia nguvu

Kenya na nchi nyingine zilipigania uhuru kwa nguvu hata kama Tanzania ilienda kusaidia kijeshi lakini hakuna vita vya kidai uhuru Tanzania mwenye historia alete hapa.

Machifu ndio walikua wanapigana na sio Tanzania kwa ujumla, watz tuache ushabiki mandazi, ndio maana mpaka leo CCM inatuona mabumbunda na hatuna cha kuwafanya
 
Ni ukweli kabisa, kilichoipumbaza Tanzania ni uhuru wa kupewa bila kutumia nguvu

Kenya na nchi nyingine zilipigania uhuru kwa nguvu hata kama Tanzania ilienda kusaidia kijeshi lakini hakuna vita vya kidai uhuru Tanzania mwenye historia alete hapa.

Machifu ndio walikua wanapigana na sio Tanzania kwa ujumla, watz tuache ushabiki mandazi, ndio maana mpaka leo CCM inatuona mabumbunda na hatuna cha kuwafanya
Umeongea ukweli kabisa mzee. Wakati mwingine ni vizuri kusema ukweli.
 
Katika kupigania uhuru kila nchi ilipigana kama kenya kulikua na mau mau na sisi tulikua na maji maji war zote hizo zilikua ni mbinu za kupigania uhuru na mapambano hayo yalikua na uwanda mkubwa sana
Majimaji walipigana zamani sana tena walikuwa wanapigana dhidi ya Wajerumani. Mimi nasema Waingereza waliwapa uhuru wenu bure bila kumwaga damu. Unapinga hilo?
 
Ni ukweli kabisa, kilichoipumbaza Tanzania ni uhuru wa kupewa bila kutumia nguvu

Kenya na nchi nyingine zilipigania uhuru kwa nguvu hata kama Tanzania ilienda kusaidia kijeshi lakini hakuna vita vya kidai uhuru Tanzania mwenye historia alete hapa.

Machifu ndio walikua wanapigana na sio Tanzania kwa ujumla, watz tuache ushabiki mandazi, ndio maana mpaka leo CCM inatuona mabumbunda na hatuna cha kuwafanya

ushabiki maandazi ni kusema tz ilizisaidia nchi nyingine kupata uhuru!!!!

wewe ndio maandazi yenyewe sasa.
 
Nyie Wakenya ukiacha tambo zenu za kujifanya mnajua kila kitu huko shuleni sijui huwa mnasoma nini!! Ulitarajia Tananyika iwasaidie Manyang'au ya Kenya wakati wakati Tanganyika yenyewe ilikuwa bado chini ya Mkoloni?!

Yaani unatakiwa kurudishwa shule kujifunza kwamba, nchi nyingi Barani Afrika zilipata uhuru miaka ya 60, na nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda!

Hata hivyo, hadi kufika miaka ya 70 bado kulikuwa na nchi zingine especially Kusini mwa Afrika ambazo bado zilikuwa chini ya Wakoloni!!!

Walioenda shule wanapozungumzia role ya Tanzania kupigania uhuru wa nchi zingine wanazungumzia kuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa Waafrika wenzetu ambao bado walikuwa chini ya makucha ya Wakoloni!!

Wakati Tanzania wakifanya harakati hizo za kuhakikisha kila nchi Afrika inakuwa huru, Manyang'au ya Kenya yalikuwa yanashirikiana na Walowezi wa Kizungu kupora na kuhodhi ardhi ya Wakenya!!!

Achana na huyo Waziri, UNESCO wanaandika hapa chini kwamba:-
'Roads to lndependence in Africa: The African liberation Heritage' is a multi-country programme to be hosted by Tanzania in collaboration with African Union (AU) member countries and United Nations Educational, Scientific and Cultural organization (UNESCO).
Aidha UNESCO wanaendelea kutujuza kwamba:-
It is an acknowledgement of the importance of liberation movements to the process of decolonization of the continent as well as the role played by Tanzania in providing material and moral support to the liberation movements which led to the struggle for independence in Southern Africa.
Kisha wanamwelezea Jemadari wa Mapambano:-
Through Mwalimu Nyerere's leadership, Tanzania was the material, political, philosophical and spiritual base for many liberation movements, Tanzania ensured that a generation of Africa leaders was ready when the countries gained their independence. Through the "Dar School", intellectuals at the University of Dar es Salaam provided future African leaders with a philosophy of African unity (Pan - Africanism) which is still today the vision of the African Union (AU).
Hayo hapo juu yanapatikana kwenye andiko la UNESCO titled:- 'Roads to lndependence in Africa: The African liberation Heritage'. Humo vikaragosi vya Kizungu, a.k.a Kenya hawajatajw

Sio hivyo tu, hata gazeti lenu wenyewe, The Standard linaandika:-
After Mandela was released from detention in 1990, one of the immediate international engagements was a round African trip to thank leaders, particularly of the ‘Casablanca Group’ led by Libya and ‘Frontline’ states led by Tanzania that supported ANC against apartheid.
Na kumbukumbu zinaonesha kwamba, Nelson Mandela na Zuma walipita Jomo Kenyatta INternational Airport lakini waligoma hata kuteremka pamoja na SA Officials kuweka Red Carpet wakitarajia Mandela angeteremka wakati akiwa safarini kuelekea Libya!

Wapigania uhuru Afrika yote wanaiona Kenya ni Vibaraka tu wa Wakoloni kwa sababu you were bedding with the Boers and other Western Monsters!!
 
Majimaji walipigana zamani sana tena walikuwa wanapigana dhidi ya Wajerumani. Mimi nasema Waingereza waliwapa uhuru wenu bure bila kumwaga damu. Unapinga hilo?
Na hapo ndo uone tofauti kati ya Tanganyika na Kenya!!!

A moment colonists set their feet in Tanganyika, Mababu zetu waka-react!!

Mwaka 1891, miaka 6 tu baada ya Mkoloni Mjerumani kuanzisha utawala wake, Wahehe wakiongozwa na Mkwawa wakapigana na Mjerumani!!! Kumbukumbu zinaonesha, battalion ya kwanza ya Mkoloni Mjerumani ilifyekwa na wakalazimika kutimua mbio!!

Mwaka 1994 Wajerumani wakapeleka battalion nyingine... Wahehe wakapigana na mkoloni kwa miaka 4 hadi 1898.

Miaka 7 baadae, yaani mwaka 1905, Mkoloni wa KIjerumani akakumbana na mtiti mwingine sehemu ya Pwani ya Tanganyika kuelekea kusini!! Ingawaje Wazee wetu hawakuwa na zana zozote za maana za kivita, lakini mtiti uliendelea kwa miaka 2 hadi 1907!!

Unlike Kenya through Mau mau ambapo baada ya kukamatwa kwa kiongozi wake tu Wakenya wakaanza kufyata mkia, lakini kukamatwa mapema kwa Kinjektile Ngwale kiongozi wa Vita vya Maji Maji hakukufanya vita hivyo kuishia hapo kwa sababu ndo kwanza vita vikazidi kuenea kutokea Kilwa ilikoanzia hadi Morogoro na Ruvuma!!!

Kwahiyo ni kukosa maarifa kudhani Mau Mau Uprising ni tofauti na Maji Maji wakati vita vyote vilikuwa ni dhidi ya mkoloni!

Ni ukosefu wa Maarifa kui-rate Mau Mau kwa sababu tu ilichelewa kuanza wakati kimsingi uchelewaji huo inaonesha ni namna gani mlivyokuwa waoga kupambana na mkoloni!!

Yaani tangia 1885 mlikuwa kwenye usingizi wa pono hadi 1952 wakati Tanganyika kwa wakati huo tulikuwa tayari tumeshaonesha hatutaki ujinga miaka kadhaa iliyopita, kabla hata Wapiganaji wa Mau Mau hawajazaliwa!!!!

Na lau kama Mwingereza angeendeleza ubabe wa Kikoloni, bado Mababu ya Kitanganyika yangesimama against that colonist that was being entertianed in Kenya kwa zaidi ya miaka 60!!!!

That's TANGANYIKA, the father of TANZANIA... the same son who never bowed down even to the Boers you used to bed with!!!
 
Back
Top Bottom