sijakuelewa hapa. unataka tena muendelee kubebwa hata kwa baraza lenu la mawaziri lije huku bara kula posho? hivi hamtosheki na hawa akina nahodha vuai, dr.hatib, dr. mwinyi, dr. bilal na wengineo wengi wanaokula ruzuku za wabara bila ya kuzitolea jasho? maajabu haya.
masikini tanganyika yangu.
masikini tanganyika yangu.
Tanganyika kwa namna fulani inaitumia Zanzibar kama koloni lake bila ya kuweka kila kitu wazi. Na hii ndiyo sababu ya kutokubali uwepo wa serikali tatu au moja. Ukiweka serikali tatu, Tanganyika haitakuwa na mamlaka makubwa juu ya Zanzibar kama ilivyo sasa. Kwa mfumo wa sasa, japo mawaziri wa Mwungano hawaendi Zanzibar lakini wana mamlaka makubwa sana juu ya Zanzibar.
Rais wa Jamhuri akiitisha Baraza la Mawaziri anawaita mawaziri wa Tanganyika, na kule Zanzibar anayetakiwa ahudhurie humo ni Rais wao tu ambaye hadhi yake haiwi tofauti na ile ya Mawaziri (siku hizi naambiwa huwa haji). Ni kwenye Baraza hili la Mawaziri ndiko masuala ya ulinzi wa Taifa, mambo ya nje, uchumi, Elimu ya juu, n.k. yanajadiliwa. Na uamuzi wake lazima uwaguse Wazanzibari. Kuna Mawaziri wachache kwenye Wizara fulani waliotoka Zanzibar lakini hawapo katika wizara hizi kama wawakilishi wa Wazanzibari.
Kutokana na ukweli huo ni kwamba kwa vile Tanganyika inaitumia Zanzibar kama koloni lake kwa mgongo wa Mwungano, ni lazima ibebe gharama fulani za kulihudumia koloni lake. Kule Afrika nadhani mnashuhudia kila mara Ufaransa inaenda kuzima maasi kwenye makoloni yake ya zamani. Kama Ufaransa inagharamia mpaka leo makoloni yake, hali inategemewa iwe vipi kwa Tanganyika ambayo mpaka leo inaitumia Zanzibar kama koloni lake kwa siri?
Ukweli unaweza kuwafanya wazanzibari wachukie lakini ukweli ni lazima usemwe, na ukweli huu uwe hamasa kwa Wazanzibari kupigania kuwa washirika wa Mwungano kuliko kuwa koloni kwa mgongo wa mwungano.