Keissy alianzisha tena bungeni

Keissy alianzisha tena bungeni

sijakuelewa hapa. unataka tena muendelee kubebwa hata kwa baraza lenu la mawaziri lije huku bara kula posho? hivi hamtosheki na hawa akina nahodha vuai, dr.hatib, dr. mwinyi, dr. bilal na wengineo wengi wanaokula ruzuku za wabara bila ya kuzitolea jasho? maajabu haya.
masikini tanganyika yangu.

Hao ndo wanao kula rasilimali zenu, na sio wazanzibari kwa ujumla, wanao kula ni wachache ambao hujifungia hapo dodoma.
 
Duuh!! Kessy..Huyu kwa CCM hakuna wa kumsogelea..Anasimamia anacho Amini..Siyo maigizo ya Mwingulu kuvaa matambara shingoni ndiyo Uzalendo
Huyu Kesissy ni mpuuzi tu hata posho wanazopeana huko bungeni nani kawapa ruksa angeanza kwanza kupambana nazo kama ana uchungu na Tanganyika.
 
Mawazo kama ya KESSY hamuwezi kuyamaliza kwa kupigana naye nje ya Bunge yeye ndivyo anavyoamini hata upande mwingine mwa shilingi wanasema Tanganyika imevaa koti la muungano.Rasmu ya katiba ya Mzee Warioba iliweka misigi mizuri ya kumaliza dukuduku kama hizo.Mambo yote ni serikali tatu kama ilivyoainishwa na kamati ya Mzee Warioba hata ukisoma kitabu cha Dr Mwakyembe kinafafanua vizuri dukuduku za akina Kessy na Duni suala ni serikali tatu.Mwl OLUOCHI amewambia hata katiba yetu ikipinda haitashi zaidi ya miaka 10.Tunahitaji Zanzibar na Tanganyika zenye serikali kamili si ujaja ujanja wa akina LUKUVI na WASIRA.Malikia miaka mingi alikuwa na mawazo mgando lakini kabla mwezi huu haujaisha tegemea kupata SCOTLAND huru.SITTA,LUKUVI,WASIRA mpo hapo
Well said..tunamshukuru Mhe Keissy kwa haya maono. Huyu ni mmoja wa wateule wachache waliobaki mjengoni kwa ajili ya kuikomboa Tanganyika huru
 
Wabunge wa Zanzibar wanachangia hoja zaidi ya hao wa Bara ambao kila kukicha wanaonekana wamelala tena wengine wakisha weka saini ya mahudhurio wanarudi mahotelini kujirusha na mabinti. Huyu Mjumbe Kessy ni jinga la wajinga kwa sababu bunge letu ni bunge la JMT sio bunge la Tanganyika. Hao wajumbe 83 wanawakilisha majimbo yao sawa kabisa na wabunge 300 wetu ambao kwa upumbavu wetu wameenda pale kuchuma na kugombea nafasi za kuingia mabaraza ya Bunge kuvuta Posho. Kama kuna mambo ya Tanganyika ambayo wabunge wa Zanzibar hawatakiwi kujadili basi na uiundwe Congress yenye wajumbe wake toka pande mbili ili kupitia yale ya Muungano, kisha hilo bunge la Tanganyika libakie na magarasha wake.

Akumbuke tu kwamba Katiba inayojadiliwa ni ya Tanzania hivyo kila kinachpitishwa na bunge hilo ni kwa ajili ya Tanzania sio Tanganyika, Sheria za Tanganyika ndizo hutumika kama sheria mama. hivyo ni wao Wazanzibar wamefungwa na matakwa ya Tanganyika kuingia moja kwa moja kuwa sheria mama na ndio maana wanaitaka serikali 3 (ya Tanganyika) ili sheria mama ya JMT iwe tofauti na ile ya Tanganyika.

Ama kweli ni taabu kubwa sana akili ndogo kuongoza akili kubwa.
Ama kweli ukistaajabu ya musa!
Leo ni wewe unawaunga mkono S3!! Masaa machache kwenye ule uzi wa Pasco umesema S2. Leo unashauri bunge la tatu kama Warioba, mkuu ukweli ukitimia... Ahsante Keissy unatoa majoka mapangoni.

Mkandara, kwanini hawana kazi na maana yoyote katika bunge kama anavyosema Keissy!

1. Hawana mchango katika wa fedha(siyo hadithi za Mkuu wa majeshi) katik posho na mishara yao.
Pesa hizo zinatoka hazina Dar ambako wao, kwa mujibu wa Ndulu majuzi tu hawana mchango hata senti tano.

Wanachukua milioni 15 kwa mwezi, wanaenda kutibiwa na kila mafao ikiwa ni pesa za Tanganyika kwa jina la Tanzania.
Jumla ya mishahara yao ni Bilioni 126. I mean watu 84 wasio na kazi wanalipwa kiasi hicho! Real

2. Wamekuja kutetea masilahi ya znz. Ndio maana wana 2/3. Hivyo wanapaswa kulipwa na SMZ.
Hawapaswi kulipwa na JMT kwasababu tunajua wazi hawana mchango katika hazina wala TRA.
TRA inakusanya znz na kuacha huko, hizi wanazobeba na kupora ni za TRA Tanganyika, ambayo kwa uhuni na wizi wanaita TRA Tanzania.

3. Hawana la kusema kwasababu hizi
a) Tukiongelea NECTA, wao wameondoa wana baraza lao. Hapo Dodoma hawana haki ya kuongelea mambo yetu ya elimu
b) TBS, wameondoa katika muungano, iliyobaki ni yetu wanazungumzia nini kama si umbea tu unaowasumbua
c) Mafuta na gesi walikimbia kuondoa, leo wamegundua hata pipa moja halitoshi wanakuja kuongelea isiyo wahusu
d) Waliondoa bandari ili iwe huru huko znz, leo inapokea meli 31/2 na kwa mwezi. Dodoma wanajadili bandari zetu ili iweje

Orodha ni ndefu sana na inatia kinyaa jinsi wazanzibar wanavyopora Tanganyika kwa jina la Tanzania.


Mbunge Keissy ana uchungu, maana Bilioni 126 za mishahara tu ya hao watalii wanaokuja Dodoma inatosha kumaliza tatizo la barabara na maji mkoani Sumbawanga.

Leo wananchi wa Nkasi wanalipa kodi kwenda kulipa mishahara ya watu 84 wanokuja kutetea nchi yao.

Hawa wanapaswa walipwe na SMZ ili wakija kucheza drafti wawajibike huko kwao, si kuja kulala na kuongelea mambo yasiyowahusu. Umbea tu halafu wanalipwa milioni 15/mwezi, wizi mkubwa huu.

Ngoja niwape maudhi zaidi ya hawa watalii wa Unguja na Pemba pale Dodoma.

Nchi yao ina watu 1.2M sawa na idadi ya watu wa jimbo la Ubungo au Ilala.

Wabunge wao wanawakilisha hadi watu 5,000 sawa na kata ya makurumla hapa Dar.

Mfuko wa jimbo, mbunge wa Kinodnoni, Kawe, Mpanda, Mgumu na Muheza wenye idadi ya watu si chini ya 500,000( laki tano) wanapewa pesa za mfuko wa jimbo sawa na mbunge wa znz mwenye watu (5,000) elfu tano.

Yaani mbunge wa Temeke anapewa milioni 30 sawa na wa makunduchi ambaye watu wake ni 3,000-5,000.

Kwa wale msioelewa, chuko kikuu cha Dar es salaam kina watu wengi kulliko jimbo moja la mtalii wa znz

Hizo pesa za jimbo zinatoka kodi za Watanganyika. Wao wamekataa TRA iisilete pesa bara.
Hizo zinazokusanywa bara ndizo zinaenda hazina kuwalipa hawa watalii.

Yaani chao kibaki huko, chetu ndicho tugawane kwa jina la Tanzania.
Ndio maana hawataki kusikia Tanganyika, maana Tanganyika haitatoa nafasi za wizi wa mchana namna hii. Uporaji tu

Tazama, ndani ya Baraza la wawakilishi, wao wana wajumbe 50 kwasababu hawana pesa za kulipa zaidi ya hapo.

Watalii waokuja Dodoma ni 84 kwasababu SMZ haina shida ya kuwalipa, hilo ni zigo la Watanganyika, na tunawalipa.

Huu wizi Watanganyika na hasa wabunge wa CCM wanaufumbia macho.

Kw uhalisia wabunge( watalii kwa maana halisi) wanapaswa kuja Dodoma si kwa zaidi ya siku 5.

Wasikilize bajeti ya ulinzi na usalama, mambo ya ndani na nje, naa baada ya hapo waondoke maana mengine yote wameshayakataa yasiwe ya muungano, wameyaondoa.

Hata kusikiliza ni favor maana hawajui bajeti ya wizara hizo. ZNZ haina mchango hata senti tano kumbuka.



cc Mkandara Bongolander Pasco MJINI CHAI Alinda Mchambuzi
 
Last edited by a moderator:
Kessy yupo sahihi. Tena anatakiwa apongezwe kwa kuwasemea watanganyika ambao siku zote wanashindwa kuongea ukweli kuhusu utata wa muungano. Mwenye busara yeyote lazima ajiulize,hivi zanzbar wanachangia sh ngapi kwenye gharama za muungano. Jibukeshatoa Benno Ndulu gavana kwamba hawachangii kitu!. Kingine pia tujiulize,tunapomufanya rais wa zanzbar kuwa makamu wa kwanza wa rais,hivi tuna akili kweli? Ikitokea rais wa Tanzania bahati mbaya kafa,huyo makamu wa kwanza ndiye atakua rais. Sasa kichekesho ni kwamba huyo makamu kachaguliwa na watu laki kadhaa wa Zanzbar tu,watanganyika wote milioni 44 hawajamchagua wala hawajashirikishwa kumpata! Haya ni maajabu na mbunge Kessy ana ujasiri wa kuyaelezea haya na tumemuelewa.
Kwa kuongezea hapo ikitokea CUF wamechukua nchi Zanzibar na CCM bara. Kwa hiyo lazima wawe na coalition government? na unavyosema ikatokea Rais wa Bara amekufa automatic CUF ndio itakuwa inaongoza nchi.. Hawa jamaa sijui kama wana akili aisee
 
Huyu Kesissy ni mpuuzi tu hata posho wanazopeana huko bungeni nani kawapa ruksa angeanza kwanza kupambana nazo kama ana uchungu na Tanganyika.

Miezi 6 posho sio mchezo, eti leo ananguruma, unafiki tu.
 
kwenye mada kama hizi mtu kama Ritz yupo radhi siku hiyo asipate buku7
 
Last edited by a moderator:
Eti wazenji walimsubiri Keissy nje ya ukumbi ili wambonyeze kizenji? Wanatafuta balaa hao. Wajue kuwa Keissy anawakilisha kwa kiasi kikubwa mtazamo wa watanganyika walio wengi.
 
Miezi 6 posho sio mchezo, eti leo ananguruma, unafiki tu.
Cha kuchekesha huyu Keissy, kawashikia akili watu na kumuona ana uchungu na taifa lakini yeye na wenzake wanakula kodi zetu huku wanagonga meza na kukoroma bungeni huku kwenye akanti zao wanawekewa pesa.
 
Eti wazenji walimsubiri Keissy nje ya ukumbi ili wambonyeze kizenji? Wanatafuta balaa hao. Wajue kuwa Keissy anawakilisha kwa kiasi kikubwa mtazamo wa watanganyika walio wengi.

Kessy ni kigeugeu siyo mtu wa kumwamini kirahisi,ndiyo maana alipotishwa na Wassira akatubu,kwanini asinge simamia msimamo wake.
 
Kwa kweli watanganyika ni watu wa maajabu sana,hivi aliyeificha tanganyika ni nani kama sie nyerere?zanzibar inahusika vipi na upotevu wa tanganyika?tokea nyerere alipo uasisi muungano huu ni waznzibar ndio waliokuwa wanaupinga muungano huu?wazanzibar wangapi wameteswa,wameuliwa,wamewekwa kizuizini(uamsho)na wengine kupotea hadi leo hawajulikani walipo kisa tu wamehoji muungano huu je ni haki kuwalaumu wazanzibar kwenye muungano huu?ifike mahali watanganyika muache unafiki wa kuwalaumu wazanzbar,inafika muda rais wa zanzibar mnamteua kutoka dodoma ili aje zanzibar kusimamia maslahi ya tanganyika na kuleta vifaru na majeshi kuhakikisha ukoloni wa nyerere unatawala zanzibar bila ya ridhaa ya wazanzbar,kama kweli huyo keissy sie mnafiki atueleze ni kwanini ccm hawataki serekali 3 zilizopendekezwa na rasimu ya warioba?zanzbar kwanza.
 
Cha kuchekesha huyu Keissy, kawashikia akili watu na kumuona ana uchungu na taifa lakini yeye na wenzake wanakula kodi zetu huku wanagonga meza na kukoroma bungeni huku kwenye akanti zao wanawekewa pesa.

kumbe shetani akizeeka anakuwa malaika! AU WAMEIBA ACCOUNT YAKO?
 
Bora hata kessy anaropoka uozo na upuuzi wa Ccm nyoko zao!!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Keissy ni mnafiki tu,atueleze ni kwanini ccm hawataki mfumo wa serekali 3?atueleze zanzibar inahusika vipi na upotevu wa tanganyika?ni nani alieificha tanganyika kwenye muungano?kwa nn siku za uchaguzi hupelekwa jeshi na vifaru zanzibar, kwa nini waziri mkuu wa tanzania hafiki zanzibar kukagua miradi ya maendeleo?wazanzibar ndio waliouliwa,kuteswa,kuwekwa kizuizini(uamsho),kupotezwa na wengine vilema hadi leo kisa wamehoji muungano je kwa upande wa tanganyika ni nani yaliyo mfika hayo?haturudi nyuma wazanzibar kudai haki zetu kwenye muungano huu hadi hapo tanganyika itakapofufuka,zanzibar kwanza.
 
miaka 50 ya kudanganyana ifike mahali tuwe wakweli ccm wamezoea vya dhuluma hawawezi kuishi ktk ukweli ..huyu mzee Nkasi namuunga mkono hatuwezi kubeba mzigo uliobebeka tena kila mtu ababe mzigo wake hawa wanzazibar tunalisha kwa pesa zetu hawana faida yoyote kwetu... back tanganyika

Wewe na tanganyika yako!
 
Back
Top Bottom