Keissy alianzisha tena bungeni

Keissy alianzisha tena bungeni

Kama huyu mzanzibar mmoja anasema eti Zanzibar ipongezwe kwa kukabidhi kiti chake UN mikononi mwa Tanzania Bara. Ivi hili ni jambo la kifahari? MZanzibar kweli anaongea jambo hili na kuona ni sifa? mi nadhan huyu ndiyo kwenda kupimwa akili
ngoja kwanza mr.London, zanzibar haikukabithi kiti chake tg ila ilikirudisha na kuhamia kiti ch tg. au ww ulitaka tg ihamie kiti cha znz. baada ya muungano kiti un lazima kingekua kimoja.au wewe ndio wale wanaojidai kukubali muungano lakini znz iwe na kiti un!
 
Nchi ngumu hii hasa kwa sisi wanaume wa tanganyika,kipata cha laki mbli hapo inabidi kuhudumia wazanzibar na familia yako tutafika kweli..!!?
 
Tanganyika buzi la zanzibar....,hatutaki kuchunwa tena.......... Hatutaki,rudini kwenuuuuuuuuuuuuuuuuuu nyie wazanzibar .tanganyika sio shamba la bibi..ipo siku mtarudi kwenu,ipo siku mtarudi mende msipende .nyie watu waugunja mnapenda sana vya bure mnachuna tuuuuuuu

Wewe una kwenu?elimu huna umetoka kwenye broken family
 
Hivi Kenya wanadai Pemba yao kutoka wapi? Tanzania au Zanzibar? Kessy kaongea kweli hata huku kitaa watu wanahoji hayo hayo.
 
Jana ndipo nimekuja kugundua kodi zetu tunazokatwa huku tunalisha familia nzima ya mbunge wa Zanzibar ndio maana wakija huku wanakuwa wanaufyata ila wakiwa kwao wanakuwa wakali balaa.
 
Dah!!!! mimi bado nashangaa kama account ya pamoja imeanzishwa halafu hakuna lilifonyika wakati Tanganyika ndio wanatakiwa pia waifanyie kazi wakati wazanzibar washakamilisha halafu anatokea ----- eti tunawabeba wazanzibar kubeba my ass.
Pia kama anahisi tunabebwa peleka hoja bungeni kwamba muungano basi sisi tulishaukataa na tunataka muungano washirikisho ambao tutashirikiana baadhi ya mambo tuu na mipaka lakini hamna mtanganyika anothubutu kuifufua tanganyika.

Na zaidi amsikilize mheshmiwa Tundu Lissu kwenye hoja ya wanzanzibar alivyochambua rejea mikutano ya ukawa pemba na zanzibar na vilevile bungeni wakati anawasilisha hoja halafu utajua kwamba tunabebwa ama tunabeba.In essence,hapo ndo utajua tofauti ya WAJINGA NA WASOMI.
 
Kweli Tz tumelogwa. Wabunge wa Zanzibar wanalipwa na Tanganyika
 
Kesi yuko sahihi sana. Wazanzibar wamezoea vya bure toka tanganyika! Watanganyika tuamke sasa!
 
Tatizo la Ccm hampendi kuelezwa ukweli. Mnataka kuishi kiujanjaujanja tu. Keissy alieleza ukweli na ndio ukweli ulivyo. Hata kumwambia ao be radhi haisaidii maana ameshasema. Maneno hayafutwi kwa mfuto. Na ukweli utamuweka Mh Keissy huru. Ameingia kwenye vitabu vya historia-
 
ali-keissy1-533x272.jpg


Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mh Ali Keissy (CCM)



Posted by Edson Kamukara 16/09/2014


Wajumbe wamjadili Mbowe, Jaji Warioba

Mrema amkashifu Mbatia, aomba msaada CCM


MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM), ‘amechafua hali ya hewa’ bungeni, akisema bila muundo thabiti wa Muungano wa Serikali tatu, Zanzibar itaendelea kuinyonya Tanganyika.
Kauli hiyo ambayo ni kinyume na msimamo wa CCM, inayopigania muundo wa serikali mbili, jana ililitikisa Bunge Maalum la Katiba, ambako wajumbe kutoka Zanzibar walichachamaa wakimvurumishia maneno ya kejeri na kutaka kumpiga, hatua iliyosababisha atolewe ukumbini chini ya ulinzi mkali hadi nje ya eneo la Bunge ili kumnusuru.


Sambamba na tukio hilo, pia wajumbe wengi walipoteza muda mwingi wa mjadala kumshambulia Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakisema kuwa hotuba yake ya kutaka kuitisha maandamano ya kupinga Bunge la Katiba ni uchochezi na hivyo kuomba uongozi wa Bunge utoe kauli.


Kama vile sinema, Mbunge wa Mbinga Mashariki, Kapteni mstaafu John Komba (CCM), alisahau kauli yake kwamba atakwenda msituni kupindua Serikali ikiwa muundo wa Serikali tatu utapita, badala yake akamshambulia Mbowe kwamba kauli yake ya kutangaza maandamano na migomo ni kuingilia jukumu la Amiri Jeshi Mkuu kwa kutangaza vita, halafu serikali inakaa kimya.


Licha ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kuwabeba dhahiri baadhi ya wajumbe waliyokuwa wakimshambulia Mbowe kwa kuwaacha wazungumze hata baada ya dakika kumi zao kuisha, tukio la Keissy lilionekana kumkera na kuingilia kati kuwapa nafasi baadhi ya makada wa CCM kusafisha hali ya hewa.


ALIVYOANZA KEISSY
Mjumbe huyo ambaye msimamo wake uko wazi kwa kutokubaliana na serikali mbili zinazopigiwa chapuo na chama chake, alianza kwa kumsifu Mwenyekiti wake wa kamati namba moja, Ummy Mwalimu, akisema ni mwanamke jasiri anayefaa kugombea hata urais kwa jinsi alivyowaongoza vizuri.


Hata hivyo, wakati wajumbe wanawake wakimshangilia kwa makofi, Keissy aligeuka na kugusia muundo wa muungano, akisema kwamba huwezi kuzungumza katiba bila kujadili msingi wa muungano ili kuweka bayana ukweli.
“Ukweli lazima uwekwe wazi ili vizazi vijue na kila mtu abebe mzigo wake. Tanganyika imekuwa ikibebeshwa gharama za Zanzibar, tuna wabunge 83 wa Bunge la Jamhuri wanagharamiwa kila kitu wao, wake zao, waume zao familia zao na Serikali ya Tanganyika,” alisema.


Keissy aliongeza kwamba, jambo baya zaidi ni kwa serikali ya Zanzibar kutoweza kuchangia hata senti katika mfuko wa fedha wa pamoja na hivyo kusisitiza kwamba, muungano lazima uwekwe wazi kila mtu agharamie kadiri anavyotumia.
“Hili la Wazanzibari kutochangia gharama za muungano katuambia Gavana Beno Ndullu alipokuja kwenye kamati yetu, sasa tuache kujenga nyumba juu badala ya kuimarisha msingi, huu ni mfumo wa vyama vingi sio kama wakati ule wa chama kimoja wakati wa Nyerere,” alisema.


Alihoji kwamba, hata katika muundo wa serikali mbili unaopendekezwa na CCM, ni vigumu Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa kwanza wa Rais atakayekaimu nafasi endapo rais hayupo, kwani hakuchaguliwa na Watanzania wote.
Hata hivyo, wakati Keissy akiendelea kujenga hoja zake, wajumbe wengi kutoka Zanzibar waliinuka na kuomba kumpa taarifa huku wengine wakiomba mwongozo wa kiti, wakidai mjumbe huyo anapotosha na kuwatusi kwa kauli za kibaguzi.


Keissy alipangua hoja zao hata kabla ya kiti kutoa mwongozo, akiwataka watulie wasubiri amalize huku akisema kwamba, hata
Bunge hili la Katiba Zanzibar haijachangia, kauli iliyozidisha jazbawa Wazanzibari wakimwita ‘chizi’ na wengine kudai akapimwe.

“Mimi sio chizi bali machizi ni nyie mnaokubali kubebwa tu bilakuchangia,” alisema Keissy, kauli ambayo ilimfanya mjumbe mmoja kusimama na kumpa taarifa kwamba muungano umedumisha umoja na kwamba licha ya mbunge huyo kuwa na asili ya Kiarabu ya Pemba bado habaguliwi.


Kabla hata mjumbe huyo kumaliza taarifa yake, Keissy aliendelea tena na kumjibu akisema, asimtukane kwani naye asili yake ni Kongo. Kauli hiyo ilimwinua mjumbe mwingine aliyesema lugha yake inaudhi, inakera na kwamba anapaswa kupimwa akili.


MAKINDA, WASSIRA, HAMAD WAINGILIA
Baada ya hali kuzidi kuwa tete, Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda, aliomba nafasi kusema neno na kuwataka wajumbe wa Bunge hilo watambue kwamba wamefanya kazi kubwa hadi sasa, hivyo wapuuze yanayojitokeza na kusonga mbele.


Pia, Sitta aliwapa nafasi wajumbe Mohammed Thabit Kombo, Hamad Rashid Mohamed na Waziri Stephen Wassira, ambao walieleza historia ndefu ya muungano, wakisema umeweza kudumu kwa sababu ni wa damu baina ya watu wa pande hizo mbili.


Wassira, alisema kuwa usalama, amani na utulivu ni matunda ya umoja wa watu ambao thamani yake haiwezi kupatikana kwa fedha na hivyo kumshauri Keissy kuchunga kauli zake, akisema ulimi mara zote ndio huzaa matatizo.
Naye Sitta, alisema kuwa ni vigumu kwake kujua mjumbe atazungumza nini, hivyo akawataka kuzingatia kanuni inayolinda majadiliano na kisha akamtaka Keissy kufuta kauli yake kwamba Wazanzibari wanabebwa na Tanganyika.


Katika kuepusha rabsha, muda mfupi baada ya Bunge kuahirishwa kwa ajili ya mapumziko ya mchana, wapambe wa Bunge walimfuata Keissy na kumuondoa ukumbini kijanja, wakimpitisha mlango wa Spika na kumsindikiza hadi nje ya eneo la Bunge.


Hatua hiyo, iliokoa jahazi kwani wajumbe wengi kutoka Zanzibarwalionekana nje ya ukumbi wa Bunge wakimsubiri kwa hamu bila mafanikio, pasipokujua kwamba alikuwa ametoka nje tayari.


WARIOBA, MBOWE GUMZO
Katika hatua nyingine, hotuba ya Mbowe juzi katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa CHADEMA, ya kutaka wafuasi wa vyama vinavyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kuandamana kupinga Bunge hilo kuendelea, imewaumiza wajumbe wengi.


Wajumbe wengi waliochangia wakiwemo Fahami Dovutwa (UPDP), Abdallah Bulembo, Said Nkumba, Boniface Simbachawene, Amos Makalla, Prof. Mark Mwandosya na John Komba (wote CCM), na Maresia Power (201), walisema Mbowe anachochea vurugu.


Wakati Makala akiwaita UKAWA kuwa ni sawa na mtoto deko, Dovutwa alisema kuwa hao hao walimpigia kura Sitta wakidai ni tegemeo la kulinda masilahi yao katika mchakato huo, lakini alivyokataa kufanya hivyo sasa wamemgeuza aduai yao.


Komba alirejea kauli yake ya zamani katika Bunge hilo kwamba,vurugu zote zinaletwa na Jaji Warioba ambaye anawatuhumu wajumbe wa Bunge hilo kwamba wanakula fedha za wananchi bure wakati tume yake nayo ilikula fedha nyingi.


“Bunge hili litoe tamko kwamba ‘Warioba ni shida’…ni sawa na mtu aliyefufuka kijijini, watu wote wanamkimbia. Alipokuwa ananyolewa…sisi tulikaa kimya, na sisi tunaponyolewa naye akae kimya,” alisema.
Komba alikwenda mbali zaidi na kulishambulia Kanisa Katoliki,akiwatuhumu maaskofu kwamba wamebadili salamu ya imani ya dhehebu hilo ya ‘Kristu Tumaini letu’ na kwamba wanaagiza waumini waseme; “UKAWA Tumaini letu”.


Augustine Mrema wa TLP, alitumia dakika zake kumi, kuomba CCM wahamie Vunjo ili kumsaidia UKAWA wasimnyang’anye jimbo, na kumtusi Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kuwa aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete wakati havai sketi.


Chanzo Tanzania Daima
 
He is My favorite MP. Hana unafiki wala kuuma maneno zaidi ya kusimamia kila anachokiamini.
ccm watake wasitake serikali 3 haziepukiki nchi hii.
 
Sasa na izi pesa za TRA zinazosafirishwa kuletwa bara inakuaje? Hiyo misaada inayokuja kwa jins la TANZANIA inaishia wapi? Ile chenji ya Radar imeishia wapi na ilisemwa kuwa ni hela ya muungano? Hebu nielewesheni, izi pesa za Muungano mnazotubebea zinatumika wapi? Wakati barabara zanzibar zinajengwa na SMZ au msaada kutoka nje? Airport inajengwa na SMZ, bandari SMZ, hio hela mnayotubeba iko wapi? Inatumika kulipia mishahara ya Zanzibar kama mnavojidai? Kuwalipa walimu mnapata shida kisha mulipe wafanyi kazi wa SMZ? Labda muwalipe kwa kuwafanya wanyamaze! Nyinyi kama Tanganyika mmeifanyia nini Zanzibar hasa hata mseme mnatubeba wakati nyie wenyewe hamjiwezi!miji yenyewe mnajengewa na wazanzibari na ajira mnapewa na wazanzibari. Eti anatoka mtu uko anasema wazanzibari wanapenda vya bure kumbe choyo tu akiona wazanzibari wakiweka majengo katika nchi ambayo watu hata kujenga chumba hawajui..... Kama Keissy kidume atangaze kuwa Muungano basi na wala huo wa mkataba usiwepo, atakuwa katusaidia sana tena tutamshukuru sana. Asikae akazungumza mambo asoyajua, analalamika jimboni kwake hakuna maji, ni mbunge saivi miaka mingapi? Kishapokea kiasi gani? Kama anauchungu na watu wake angewafikishia maji zamani tu..... Au ata kisima huwezi kuchimba uko unapoishi?
 
Kama tukipata video huu uzi utanoga sana! Kessy yupo sahii hatuwezi kuilisha mijibaba mizima huku ikipiga kelele!,,,,,,,,Tanganyika sio buzi la kuchuna, wamezoea dezo na vya kunyonga!.....wsmekutana na maccm ambayo hayataki kusikia ukweli!
 
Safi sana Keissy wewe ni mbunge halisi wa watu wako. Ulichowwambia ni ukweli na hoja kuwa ati wamepoteza utambulisho UN sisi tumepoteza si UN tu bali hata ndani hakuna mtanganyika kisheria bali wazanzibari wapo. Huu ukoloni wa kutawaliwa na watumwa wa unguja ningependa ukome mara moja. Kosa letu ni kuwasaidia mapinduzi sasa wametupindua na sisi. Wazanzibari wanapenda vya bure sana. Bora tuitishe kura ya maoni ya kuamua kujitenga kama Scotland tu.
 
Ndugu Zangu ,sifa walizo mwagiwa wabunge kutoka Zanzibari na Ndgugu A Keissy sio matusi au kashifa kama inavyo ongelewa ndani na nje ya bunge ,kabla sijalizungumzia hili nitapenda kutowa mifano hai ya familia nyingi za kizanzibari ambazo jamaa zao wapo hasa warabuni wamekuwa wakiishi katika maisha kama aliyoyaeleza Ndugu Keissy katika bunge ni kweli tupu maisha ya jamii kubwa kule zenj wamekuwa wakiishi hivyo kupokea pesa au vitu muhimu kutoka kwa familia zao zilizopo nje utamaduni wao wa kuzaliwa nao ,sasa inapokuja aliyoyasema Ndugu Keissy zile zilikuwa ni sifa kwa wabunge wa kizanzibari na wengi wao hujisifia hilo kwa wake zao na familia zao kuwa wanakwenda bara kuchota mtaji sio aibu kwao mwanamume anahudumiwa yeye na mkewe na watoto kama tunavyo wahudumia wabunge wao na ndio hilo lilizo elezwa ndani ya bunge ,hao watu ni watu wa mtelezo jamii imekulia katika hali hiyo usitegemee wabunge wao wabadilike na ndio leo hii tunashuhudia wamekuwa mstari wa mbele kukwamisha maendeleo, uvivi wa akili zao imepelekea hao waitwao wabunge kutoka zanzibar kuwa na akili za kuchangiwa , jana leo hii ndugu Ali Keissyi ameliweka bayana lakini hao viumbe wameweka pamba za masikio as long mrabo kutoka Tanganyika unaingia katika mikono yao binafsi.
 
Back
Top Bottom