Kazi kwenye miradi mbalimbali huwa wanapataje?

Mmanyanigho

Senior Member
May 18, 2018
186
326
Wakuu mwema.

Kuna miradi mingi inaendelea hapa mjini Dar es salaam. Kuna mwendokasi maeneo mbalimbali wanatengeza.
Kuna barabara za mitaa zinajengwa maeneo mbalimbali, lakini yote hii huwa naona watu wakishiriki ujenzi huo (vibarua).

Sasa huwa najiuliza huwa wanapataje hizo nafasi, kuna matangazo huwa wanatoa? Wanayatoa kupitia wapi, kuna wale wanaochimbaga mitaro kwenye hiyo miradi wanapataje hizo nafasi??

Kwa anaejua huwa wanapataje hizo kazi atujuze wakuu.

Nimefika mjini hali si hali.
 
Dar ukiona vijana wamebeba vibegi mgongoni usidhani wote wanafanya kazi kwenye viyoyozi. Wengine ni fundi wajenzi wanazunguka kusaka kazi kwenye site mbalimbali. Anachotakiwa kujua ni wapi kuna site mpya ya ujenzi, anajihimu anawahi kuongea na fundi mkuu kabla kazi hazijaanza. Akiambiwa timu imekamilika anasogea mbele. Hali inakuwa hivyo had I siku atakapopata gap. Hivyo vibegi vinakuwa vimebeba viyendea kazi, akipewa kazi hatakiwi kusema naomba mwiko au pimamaji.

Wewe ni fundi wa nini?
 
Saidia fundi mkuu
 
Nitaelezea namna ya kupata kazi kwenye kampuni za ujenzi hasa za wachina kama ifuatavyo:-
1. Kamlete: Hawa mara nyingi wanandugu serikalini hasa Tanroad mara nyingi hawa wanapita kwa project manager wa mradi moja kwa Moja hata kama nafasi hakuna lazima atafukuzwa mtu ili jamaa apate nafasi. Nafasi hizi ni za madereva, engineer hasa fresh graduate na kazi za ofisini.
2. Mchina Wangu: Hili kundi la pili unakuta walishafanya kazi na Mchina Foreman so huwa wanapigiana simu kama kuna mradi sehemu so wanaenda kupiga kazi. Hapa kwenye hili kundi kuna foreman mbongo huyu anamniwa na Boss( Foreman Mchina) Huyu Mbongo akisema wewe si Sawa hapo kazi hakuna Foreman Mbongo mara nyingi wanauza kazi inategemea na kiasi gani unacho kinaanzia 30k to 50K.
3. Wasoteaji: Hawa huwa wanashinda getini kwenye Kamp ya mradi husika hapa watu wanakaa hata miezi 3 nje ya camp wakisubiri kupata kazi hapa ni bahati yako mfano kama Kuna mchina katoka China na sio mwenyeji Basi anatoka nje ya geti na kuchagua watu kwa ajili ya test then kazini.
4. Madereva: Hawa kama hauna konection sahau kazi lazima uwe na mtu anayekujua ili mchina akupe kazi hasa hizi Howo kuhusu Gari ndogo hizo sahau kwani zinakuwa na wakongwe kwenye kampuni
5. Ofisini: hapa unapeleka Cv yako kwenye kila kampuni ya wachina ya ujenzi kuna HR wawili mmoja Mchina ambaye ndo kila kitu na Mbongo huyu Hana NGUVU la kuamua lolote. Ila kama Kuna nafasi ya kitaalamu hapa HR mbongo atakuombea kazi kwa HR mchina ili upate hiyo kazi.
NB: Kufukuzwa kazi kwenye hizi kampuni zetu ni kitu cha kawaida unaweza kufanya kazi siku mbili ukaambiwa wewe sio Sawa.
 
Wakuu mwema.

Kuna miradi mingi inaendelea hapa mjini Dar es salaam. Kuna mwendokasi maeneo mbalimbali wanatengeza.
Kuna barabara za mitaa zinajengwa maeneo mbalimbali, lakini yote hii huwa naona watu wakishiriki ujenzi huo (vibarua).

Sasa huwa najiuliza huwa wanapataje hizo nafasi, kuna matangazo huwa wanatoa? Wanayatoa kupitia wapi, kuna wale wanaochimbaga mitaro kwenye hiyo miradi wanapataje hizo nafasi??

Kwa anaejua huwa wanapataje hizo kazi atujuze wakuu.

Nimefika mjini hali si hali.
Dah!kuna jamaa wanajenga hapa karibu na mtaani kwangu goba ni bonge la fensi krbia heka1 mitofali kama yote...ukijiwah utapata kazi ila ile mikazi migumu sana km hujazoea.
Ni goba kwa awadhi nyuma y fensi ya marehem bi lwakatare
Ila mimi naonaga bora ujitoe ufaham tafuta elf20 funga karanga anza kuuza kilo3 tu zunguk kwenye mikusanyiko Ya vijiwe vya vijana na wazee mimi
 
Wakuu mwema.

Kuna miradi mingi inaendelea hapa mjini Dar es salaam. Kuna mwendokasi maeneo mbalimbali wanatengeza.
Kuna barabara za mitaa zinajengwa maeneo mbalimbali, lakini yote hii huwa naona watu wakishiriki ujenzi huo (vibarua).

Sasa huwa najiuliza huwa wanapataje hizo nafasi, kuna matangazo huwa wanatoa? Wanayatoa kupitia wapi, kuna wale wanaochimbaga mitaro kwenye hiyo miradi wanapataje hizo nafasi??

Kwa anaejua huwa wanapataje hizo kazi atujuze wakuu.

Nimefika mjini hali si hali.
Connection tu mkuu
 
Back
Top Bottom