Updates ya miradi mbalimbali iliyokwama kumalizika

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Uzi huu utakuwa maalumu kwa kupeana taarifa za miradi mbalimbali inayosuasua au iliyokwama kumalizika ujenzi wake ili kusaidia kuiamsha serikali iweze kutupia jicho kwenye hiyo miradi iweze kuisha na kuwa msaada mkubwa kwa watanzania.

1.Niko mkoa wa Simiyu wilaya ya Maswa. kijiji cha Mwabayanda kuna bonge la zahanati lakini umaliziwaji wake unasuasua na inadaiwa na wenyeji wa hapa kuwa kandarasi haonekani site kwa muda mrefu sasa.

3.Pia kule jimbo la Mtama mkoa wa Lindi madiwani wamelalamikia ujenzi wa hospitali ya wilaya umekwama kuisha licha ya pesa zote zaidi ya millioni 500 kupelekwa!.

4.Licha ya serikali kupitia naibu waziri wa ujenzi mh Mwita Waitara kukanusha kuwa ujenzi wa barabara ya njia 8 kutoka Kimara hadi Kibaha haujakwama kukamilika lakini wakazi wa pembeni mwa barabara hiyo wamesema hawajawahi kumuona kandarasi anayejenga barabara hiyo kwa miezi 2 sasa!!
==
Lindi. Madiwani wa halmashauri Mtama mkoani Lindi wamekerwa na kitendo cha Sh500 milioni kutotosha katika ujenzi wa wodi tatu za hospitali ya wilaya.

Kutotosha kwa fedha hizo kumeelezwa na mhandisi idara ya ujenzi, Abruhan Juma kutoa taarifa ya kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa wodi ya uzazi, wanaume na wanawake kwamba umekwama kwa sababu kiasi hicho cha fedha kuisha na kuhitajika nyingine Sh198 milioni.

"Mradi umesimama baada ya ongezeko la mahitaji ya vifaa ikiwemo mbao na silingi bodi," amesema Juma.

Madiwani Halmashauri ya mtama mkoani Lindi
Akizungumza kwa niaba ya madiwani, diwani wa Nahukahuka, Hamza Nguachi amesema wanatambua Serikali imepeleka Sh500 milioni lakini cha kushangaza hazikutosha," fedha hizi zimepelekwa kila wilaya kwa maelekezo lakini kwingine zmemaliza ujenzi ila Mtama zimeshindwa kukamilisha ujenzi na kunahitajika nyingine kama Sh200 milioni," amesema Nguachi

Diwani mwingine, Hawa Nameta amesema uadilifu kwa watendaji umekuwa mdogo kwani wamekuwa wakijali maslahi yao binafsi kuliko halmashaur hali ambayo isipo zibitiwa itaendelea kudidimiza maendeleo ya halmashauri.

"Siku mmoja nilitamani kulia nliipoambiwa kuna vifaa vya ujenzi vinatakiwa kununuliwa nje ya halmashauri ya Mtama wakati vinapatikana kila mahali hapa tena kwa bei ya kupatana," amesema Nameta

Rashidi Mega, mwenyekiti wa kijiji cha Kiwalala amesema kitendo cha madiwani kuhoji na kutokubaliana kuongeza fedha za kumalizia mradi wa ujenzi wa wodi tatu ni sahihi kwani miradi ya Serikali inaletwa kwa bajeti na maelekezo.

"Kwanza niwapongeze madiwani wangu kwa kuwa na msimamo wa namna hiyo wakiendelea na tabia hiyo watarudisha uaminifu, uwajibikaji na uadilifu kwa watendaji," amesema Mega.

Mkurungezi mtendaji wa halmashauri hiyo, George Mbilinyi amesema wana changamoto nyingi ikiwemo matumizi ya fedha bila kufuata utaratibu, miradi kutokamilika kwa wakati.

"Ndugu zangu hii halmashauri inakosa usimamizi kila mtumishi alikuwa anafanya kazi kivyake na kimazoea kulikuwa hakuna wa kusimamia hayo, nimewaomba madiwani kunipa muda kurudisha nidhamu kazi, uadilifu na mahusiano," amesema Mbilinyi.
 
Uzi huu utakuwa maalumu kwa kupeana taarifa za miradi mbalimbali inayosuasua au iliyokwama kumalizika ujenzi wake ili kusaidia kuiamsha serikali iweze kutupia jicho kwenye hiyo miradi iweze kuisha na kuwa msaada mkubwa kwa watanzania.

1.Niko mkoa wa Simiyu wilaya ya Maswa. kijiji cha Mwabayanda kuna bonge la zahanati lakini umaliziwaji wake unasuasua na inadaiwa na wenyeji wa hapa kuwa kandarasi haonekani site kwa muda mrefu sasa.

3.Pia kule jimbo la Mtama mkoa wa Lindi madiwani wamelalamikia ujenzi wa hospitali ya wilaya umekwama kuisha licha ya pesa zote zaidi ya millioni 500 kupelekwa!.

4.Licha ya serikali kupitia naibu waziri wa ujenzi mh Mwita Waitara kukanusha kuwa ujenzi wa barabara ya njia 8 kutoka Kimara hadi Kibaha haujakwama kukamilika lakini wakazi wa pembeni mwa barabara hiyo wamesema hawajawahi kumuona kandarasi anayejenga barabara hiyo kwa miezi 2 sasa!!

Tuletee kwanza updates ya ile iliyokamilika ndio utuletee na isiyokamilika🤔
 
Kuna kichaaa kaicost nchi pakubwa sana akilala akiamka anaanzishwa mradi🙏🙏 nashukur Mungu alituliza bahari
 
Tuletee kwanza updates ya ile iliyokamilika ndio utuletee na isiyokamilika

Unafikiri huyu mchawi analo jema basi?! Yupo hapa kuharibu tuu na mwandiko ni wa yohana mbatizaji wa jei efu.
 
Barabara ya Tanga - Pangani naona imesimama...walioko jikoni tujuzeni nini shida?
 
Tukimaliza na huu uzi tufungue mwingine
UPDATES YA MIRADI ILIYOKAMILIKA LAKINI IPO CHINI YA KIWANGO RUSHWA NA UFISADI ULIVYOSHAMIRI KWENYE HIYO MIRADI.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom