Kawambwa Amechakachua matokeo ya Darasa la 7 2012

Kawambwa Amechakachua matokeo ya Darasa la 7 2012

Mpamo

Member
Joined
Dec 8, 2012
Posts
94
Reaction score
17
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ameundaganya umma kuwa kiwango cha ufaulu kimeongezeka huku kukiw na habari za uhakika kutoka kwa Maafisa Elimu wa Mikoa kuwa baada ya kukamilisha zoezi la usajili walitakiwa wachague upya wanafunzi baada ya kuona hali ilikuwa mbaya sana. Waliagizwa kuchagua wanafunzi hadi waliopata alama 70/250.

Sasa kama mwaka 2011 walichagua hadi aliyepata alama 100/250, je Waziri wa Elimu yuko sahihi kudai kuwa idadi ya waliofaulu imeongezeka bila kuwaambia watanzania ukweli kuwa ufaulu wa mwaka huu ni kupata 28% badala ya 40% ya miaka yote?

Je hawa maafisa elimu wameamua kumsingizia Waziri kwa malengo yapi eti walipewa maelekezo? Wadau toeni ufafanuzi nimeshindwa kuelewa kilichotangazwa leo kuhusu matokeo ya darasa la 7
 
Nashangaa wamemwacha aharibu elimu kwa muda mrefu namna hiyo. Huyu jamaa hamna kitu kabisa na ndiyo maana alikuwa anahamishwa hamishwa wizara katika kipindi cha miaka mitano alihamishwa mara nne sasa kumwacha hapo muda mrefu matokeo yake ndiyo hayo tumeona alivyotangaza matokeo na huo ni mwanzo tu hadi elimu ife kabisa. Tusubiri idadi a wataaobainika kutojua kusoma na kuandika. Ama kweli maskini hana chae!
 
Nasikia hadi waliopata 60% nao wamechaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari,tatizo watoto wao hawasomi hapa.
 
Hivi Kawambwa anafanya hivyo kwa maslahi ya nani. Hawezi kumwogopa Mungu hata kidogo? ni kweli watoto wao hawasomi kwenye hiZo shule ambazo wameamua kupeleka hata wasiojua kusoma
 
Serikali isichokijua ni umuhimu wa walimu,wataendelea kuchakachua hadi wachoke.Walimu wanataabika mitaani kwa mazingira magumu,mishahara kidogo,madeni yao sugu,ukosefu wa nyumba n.k nani atafundisha kwa moyo na hii serikali ilivyo ya ajabu hata xmass hawatalipa mshahara.Seriksali isitafute mchawi wa elimu ni yenyewe,iongeze
 
Yaani Katika mawaziri wasiowajali walimu Kawambwa ni nambari one. Wakati wa mgomo wa walimu alikuwa anatoa kauli za majigambo na vitisho kwa walimu. Sasa mbona ameshindwa kutangaza kazi halisi ya walimu waliyomfanyia kutokana na ujira anaowalipa?
 
kufeli kwa wanafunzi kunaonekana kwao hukuna tatizo na hawajui wapi waanzie maana hawataki kuwashirikisha wadau wa elimu yaani waziri ni kila kitu na anajua kila kitu
 
Kama kuna ushahidi kuwa amedanganya umma katika jambo ambalo ndiyo hasa msingi wa maendeleo, hivi kwa nini asitakiwe kujiuzulu? Yeye ndiye aliyeagiza maafisa elimu warudi kambini ili wachague hata wasiojua kusoma wapelekwe sekondari ili mradi kujaza tu madarasa. Na ni yeye mwenyewe ametangazia umma bila hata aibu kuwa wanafunzi waliofanya mtihani mwaka huu wamefaulu zaidi kuliko wa mwaka 2011, eti ongezeko la asilimia 8, sasa hapa si kuna ushahidi wa moja kwa moja ukilinganisha na Dr. Cyril Chami ambaye ameondolewa kwenye uwaziri kwa makosa ya Ekelege, Maige alikuwa na kosa gani la moja kwa moja? Au huyu jamaa anafanya hivyo kwa sababu ni ndugu yake na JK?
 
Hivi Kawambwa anafanya hivyo kwa maslahi ya nani. Hawezi kumwogopa Mungu hata kidogo? ni kweli watoto wao hawasomi kwenye hiZo shule ambazo wameamua kupeleka hata wasiojua kusoma

mwanawe alikuwa anasoma Mzizima
 
Hivi Kawambwa anafanya hivyo kwa maslahi ya nani.

ni kwa maslahi yake binafsi. angetangaza kiwango kimeshuka kila mtu angehoji utendaji wake ila kwa sasa bado ni wachache wanaoelewa uhalisia.
 
Jamani mnanionea buuuure mimi Kawambwa,mwenzenu nimeagizwa na mkulu ili kukinusuru chama chetu(ccm)
 
Tanzania haina mwenyewe. Kodo unakamuliwa mpaka basi. Kwa akili yako ndogo unadhani unjenga kumbe unawasaidia viongozi kwenda kubembea majuu na wake zao, kulipia watoto wao ada Uingereza, Marekani, Ujerumani, Urusi, na kwingineko ambako shule zimesimama. Kodi yetu ndiyo ya kwenda kupima afya na kujitibu India, Marekani, Ujerumani na kwingineko. Kwetu tunabaki na kina kawambwa wakitutangazia matokeo feki na shule ambazo zimebaki historia. Je wanawezaje kutuambia chakula ni kizuri na wameandaa vyema wakati wao hawali? Watanzania tuache ujinga. Hawa viongozi si wa kuzomewa pekee na ccm yao, bali ni wa kupiga mawe. Hii nchi ni yetu na sii yao. Wao wanaweza hamia Uswiz walikokusanya na kuficha asilimia kubwa ya kodi zetu. Sisi tunabaki hapa hapa tukiteseka na kufa bila sababu. Angalieni maadili yanavyomomonyoka kwa kasi. Angalieni walikofika polisi. Angalieni uhalisia wa mashule, mahospitali, barabara, umeme, nk. Vyote ni ubabaishaji tu. Je ni kwa nini? Ukosefu wa elimu. Tuamke na mawe sasa inatosha!
 
Well kama zamanii kupasi ilikuwa ni kupata zaidi ya asilimia 70 na watu wachache wanafikia basi wenye ugenius wao badala ya kuongeza kiwango cha ubora wa elimu ili wanapunguza alama. Sasa kama alama ya 50 inafikiwa na wengi well utawalaumu. NI sawasawa na badala ya kukimbia mita 100 unaona watu hawafikii inabidi uweke mita 50... na wengi wanaifikia unajisia unawakimbiaji wa mita 100!

Hili linahitaji kuulizwa Bungeni kama viwango vya alama za kupasi vimebadilishwa na kama ndio ni vipi na kwanini?
 
Elimu ya tz kwa ujumla ni janga kuu la taifa.
 
Nadhani tatizi sio Kawambwa, ni serikali mzima, hawezi kufanya lolote bila kuwasiliana na siri-kali kuuuuuu
 
Viwango vya kuchaguliwa vinaendana na uwepo wa nafasi katika shule za sekondari. Acheni umbumbumbu, shule za msingi hakuna neno kufaulu isipokuwa kuchaguliwa.
 
Mmkjj. NIna mashaka kama tuna ALAMA ya kupass mtihani kwa Tanzania. Otherwise jiulize maswali yafuatayo.
  1. Ni nani anaweka standard za kupass (labda baraza la mitihani) kwa kuzingatia mambo mengi
  2. NI nina mwenye mamlaka ya kubadilisha alama kuiongeza ama kuipunguza? Vitu gani vya kuzingatia isije kuwa mtu anapunguza alama kwa kuwa tu mtoto wa dadake amepata alama za chini?
  3. Madhara ya kupunguza alama ni nini? - hasa kwa walimu wa sekondari, vyuo vikuu wanaokuja kuwapokea watoto walioshindwa mitihani?
  4. Labda tujiulize (je mitihani ni njia sahihi kuwapima watoto kiwango cha uelewa wao pasipo kuwakaririsha? Kama ndo njia pekee iliyopo ama kuna namna nyingine je kwa vipi wizara husika zimejenga mifumo ya kuwapokea hao failures na kuwaingiza kwenye mfumo rasimi wa inputs (mafunzo) outputs ufaulu mitihani

Well kama zamanii kupasi ilikuwa ni kupata zaidi ya asilimia 70 na watu wachache wanafikia basi wenye ugenius wao badala ya kuongeza kiwango cha ubora wa elimu ili wanapunguza alama. Sasa kama alama ya 50 inafikiwa na wengi well utawalaumu. NI sawasawa na badala ya kukimbia mita 100 unaona watu hawafikii inabidi uweke mita 50... na wengi wanaifikia unajisia unawakimbiaji wa mita 100!

Hili linahitaji kuulizwa Bungeni kama viwango vya alama za kupasi vimebadilishwa na kama ndio ni vipi na kwanini?
 
Back
Top Bottom