Kawambwa Amechakachua matokeo ya Darasa la 7 2012

Kawambwa Amechakachua matokeo ya Darasa la 7 2012

Viwango vya kuchaguliwa vinaendana na uwepo wa nafasi katika shule za sekondari. Acheni umbumbumbu, shule za msingi hakuna neno kufaulu isipokuwa kuchaguliwa.

We kibaraka wa Nape, Ufaulu upo ndio maana wanafanya mtihani. Kuna viwango vya kufaulu ili uchaguliwe kwenda kidato cha kwanza. Si lazima utetee kila kitu, hata kama unalipwa mida mingine tumia busara.
 
Nadnahi waziri kivuli wa Elimu afatilie hii habari kama ni kweli basi amuombe Kamanda Lema wakae wasaidiane kuandika hotuba yenye manaeno ya kuchoma kama ile ya mambo ya ndani!
 
Nimesoma gazeti la MWananchi wameandika kuwa MATOKEO YA DARASA LA SABA AIBU.
Waliopata Daraja D ano wachaguliwa kuendelea na Sekondari .
Hali ya ufaulu ni kama ifuatavyo
Daraja A (alama 201 - 250) - 0.34%
Daraja B ( alama 151 - 200) - 4.54%
Daraja C ( alama 101 - 150) - 24.82
Daraja D ( alama 51 -100) - 58.82%
Daraja E ( Alama 0-50) - 8.18%

Waziri wa Elimu Kivuli Kamanda wetu Susan Lyimo ameshaanza kuyafanyia kazi amesema anasubiri apate taarifa rasmi za kitaaluma za matokeo ili kambi ya upinzani iweze kutoa tamko rasmi. Kwa hiyo wale wenye taarifa za kuaminika wawasiliane naye ili aweze kufanyia kazi mara moja.
Simu yake ni 0715 582 414.

Source: Gazeti la Mwananchi 21/12/2012
 
Taifa linaangamia kwa sababu za baadhi ya kuogopa kelele za wananchi,siasa.Mara nyingi ukweli Serikali haipendi kuukubali.
kiwango cha elimu kimeshuka,na hakuna hatua iliyochukuliwa ya kunusuru mfumo wa elimu unaobadilishwa kila kukicha.

Kizazi kijacho kitakuwa na wakati mgumu sana;wajinga watakuwa wengi.!
 
basi kama ukweli ndio huo kawambwa ni janga la kitaifa na anatuchimbia watanzania kaburi kwa sababu kwa sasa tumebaki kuangalia quantity ya elimu yaani mirundikano ya wanafunzi kuanzia sekondari hadi mavyuo vikuu bila kujali ubora wa elimu inayotolewa na abado kwa sababu kuna hili lingine la matokeo ya form four kwani shule nyingi zinazoongoza kufeli ni shule za kata ambazo zipo kwa ajili ya watoto wa maskini kujichimbia kaburi wenyewe.
 
katika mawaziri ambao JK alibugi ni huyu Kawambwa, anadidimiza Elimu na serikali umeridhika na kusahau kabisa hii wizara ambayo ndiyo mhimili wa taifa.
 
basi kama ukweli ndio huo kawambwa ni janga la kitaifa na anatuchimbia watanzania kaburi kwa sababu kwa sasa tumebaki kuangalia quantity ya elimu yaani mirundikano ya wanafunzi kuanzia sekondari hadi mavyuo vikuu bila kujali ubora wa elimu inayotolewa na abado kwa sababu kuna hili lingine la matokeo ya form four kwani shule nyingi zinazoongoza kufeli ni shule za kata ambazo zipo kwa ajili ya watoto wa maskini kujichimbia kaburi wenyewe.

nikweli serikali inafurahia mlundikano wa wanafunzi darasani pasipo kufutailia ubora wa elimu inayo tolewa na mazingira kwa ujumla.
 
kawambwa mwogope mungu wako. taifa unalipeleka wapi hili? kwanini usikubali matokeo na kukiri mapungufu? wapeni walimu stahiki zao taifa linakufa
 
Amini usiamini maafisa elimu walirudishwa kufanya uteuzi upya na kuongeza wanafunzi kwakuwa shule nyingi zilikosa wanafunzi kwa kiwango cha ufaulu busara wangeacha matokeo yaleyale ili tujue sasa wamesema watatoa mtihani ili kuwaondoa wasiojua kusoma je wote wakifeli tena itakuwaje?
 
Ni vizuri sana kuweka yaliyo mabaya na yanayowakwaza watanzania kuendelea kuwekwa wazi
 
Viwango vya kuchaguliwa vinaendana na uwepo wa nafasi katika shule za sekondari. Acheni umbumbumbu, shule za msingi hakuna neno kufaulu isipokuwa kuchaguliwa.

Wewe ndio una tatizo kwani hoja iliyotolewa ni ya kweli wewe unapotosha ila unaonekana sio mdau wa elimu kabisa ok soma tena hii news then edit yako okey?
 
Nimesoma gazeti la MWananchi wameandika kuwa MATOKEO YA DARASA LA SABA AIBU.
Waliopata Daraja D ano wachaguliwa kuendelea na Sekondari .
Hali ya ufaulu ni kama ifuatavyo
Daraja A (alama 201 - 250) - 0.34%
Daraja B ( alama 151 - 200) - 4.54%
Daraja C ( alama 101 - 150) - 24.82
Daraja D ( alama 51 -100) - 58.82%
Daraja E ( Alama 0-50) - 8.18%

Waziri wa Elimu Kivuli Kamanda wetu Susan Lyimo ameshaanza kuyafanyia kazi amesema anasubiri apate taarifa rasmi za kitaaluma za matokeo ili kambi ya upinzani iweze kutoa tamko rasmi. Kwa hiyo wale wenye taarifa za kuaminika wawasiliane naye ili aweze kufanyia kazi mara moja.
Simu yake ni 0715 582 414.

Source: Gazeti la Mwananchi 21/12/2012

Duuuh, sasa kama hali ndiyo hiyo wakifanya mtihani wa kuwachuja sekondari si itakuwa hatari?
 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ameundaganya umma kuwa kiwango cha ufaulu kimeongezeka huku kukiw na habari za uhakika kutoka kwa Maafisa Elimu wa Mikoa kuwa baada ya kukamilisha zoezi la usajili walitakiwa wachague upya wanafunzi baada ya kuona hali ilikuwa mbaya sana. Waliagizwa kuchagua wanafunzi hadi waliopata alama 70/250.

Sasa kama mwaka 2011 walichagua hadi aliyepata alama 100/250, je Waziri wa Elimu yuko sahihi kudai kuwa idadi ya waliofaulu imeongezeka bila kuwaambia watanzania ukweli kuwa ufaulu wa mwaka huu ni kupata 28% badala ya 40% ya miaka yote?

Je hawa maafisa elimu wameamua kumsingizia Waziri kwa malengo yapi eti walipewa maelekezo? Wadau toeni ufafanuzi nimeshindwa kuelewa kilichotangazwa leo kuhusu matokeo ya darasa la 7

Maana ya kufaulu ni kupata maksi ambazo ni PASS na si maksi za kuchaguliwa. Mnaweza kumaliza kumaliza form four wote mwaka wenu mkapata division one, lakini kwa vile nafsi ni chache maksi za kuchaguliwa zikawekwa na wengine wenye division one wakaachwa.
Mwaka unaofuata wengi wao wakapata division three na wote wakachaguliwa. tofautisha maksi za ku pass na mstari unaochorwa kwa waliopass kwa ajiri ya kuchaguliwa.
 
Back
Top Bottom