Kawambwa Amechakachua matokeo ya Darasa la 7 2012

Kawambwa Amechakachua matokeo ya Darasa la 7 2012

Mkuu hayo yote nayaelewa vizuri. Lakini kwa ini Waziri hakuyaweka wazi wakati wa kutangaza matokeo? Au dhana ya uwazi na ukweli imefutwa?
Ingekuwa vizuri akaweka wazi walipopigia mstari ili hata walimu wa selondari wajue wameletewa wanafunzi wa aina gani. Bado naona si sahihi kulingamisha kiwango cha ufaulu na mwaka uliopita wakati mstari wako umeshuka chini kwa alama 30 yaano 70 badala ya 100. Huo ni uchakachuaji!!!!!!
 
Tunakoelekea ni kupataTAIFA lenye wasomi MBUMBUMBU, ona sasa kwa hli, serikali/wizara iache Longolongo, Ukweli ni kwamba ufaulu wa wanafunzi hali c shwari.
 
Kuna mentality za kikoloni ndio zinatusumbua, hizi mentality tumeletewa ili tujibague wenyewe, mtu yoyote aliye pass kwa alama zozote zile anafaa kuendelea na masomo husika.

Kama ni vinginevyo shule za private wanafunzi wao wengi wote wangekuwa hawapasi mitihani yao, maana mara nyingi ni wale ambao hawakupata nafasi, serikalini, achana na watoto wachache wanaoenda special school kwa ukwasi wa wazazi wao.
Mbona waliopata div four wengi wanaenda private na kufaulu vizuri na kuwa acha mbali kwa wale waliopata div one? Hii ingekuwa issue kama walichaguliwa hawakufaulu mtihani.
 
..Tafadhali mwenye hiyo barua ya maagizo yanayosemwa kuhusu kurudia zoezi la kuchagua wanafunzi TAFADHALI auweke hapa. Kwa sababu hata mimi nilisikia kuwepo kwa waraka huo! nimeshindwa kupata nakala yake. Ninaamini kupatikana kwa nakala ya waraka au barua hiyo ya maagizo ndio itakuwa muafaka kuonesha watanzania kuwa, taarifa iliyotolewa na Waziri sio ya UKWELI kama wanavyotaka kutuaminisha.
 
Habari za uhakiki nilizozipatabtoka kwa ndugu yangu ambaye ni Afisa Elimu wa Wilaya anasema kuwa Waziri ametaka suala hilo la kushusha alama lifanyike kwa siri sana. Maelekezo yalitolewa kwa simu kuepuka kuwapo kwa ushahidi wa maandishi na maagizo hayo yaliambatana na vitisho kwa atakayetoa taarifa. Ushahidi utaonekana katika TSM 9 maana kila anayechaguliwa alama zake hujazwa
 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ameundaganya umma kuwa kiwango cha ufaulu kimeongezeka huku kukiw na habari za uhakika kutoka kwa Maafisa Elimu wa Mikoa kuwa baada ya kukamilisha zoezi la usajili walitakiwa wachague upya wanafunzi baada ya kuona hali ilikuwa mbaya sana. Waliagizwa kuchagua wanafunzi hadi waliopata alama 70/250.

Sasa kama mwaka 2011 walichagua hadi aliyepata alama 100/250, je Waziri wa Elimu yuko sahihi kudai kuwa idadi ya waliofaulu imeongezeka bila kuwaambia watanzania ukweli kuwa ufaulu wa mwaka huu ni kupata 28% badala ya 40% ya miaka yote?

Je hawa maafisa elimu wameamua kumsingizia Waziri kwa malengo yapi eti walipewa maelekezo? Wadau toeni ufafanuzi nimeshindwa kuelewa kilichotangazwa leo kuhusu matokeo ya darasa la 7

Serikali ya CCM inafanya makosa makubwa kwa kuifanya sekta ya elimu kuwa shamba la bibi la kufanyia siasa. Ni kweli kuwa zoezi la selection lilisimamishwa baada ya REO's kupokea maagizo toka juu na liliporudi kigezo cha mwanafunzi kuchaguliwa kilishushwa toka alama 100/250 hadi 70/250 sawa na 28%. Kabla zoezi halijasimamishwa hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba kuna shule zingepokea wanafunzi 20 kati ya 160 kwa mfano, ambao ni uwezo wa shule kuwa 'accomodate'. Kwa hiyo kitendo cha waziri kuutangazia umma kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na sekondari kimeongezeka kwa 8.8% kilikuwa na nia ya kuwaaminisha watu kuwa ufaulu umeongezeka kwa kuwa anayechaguliwa ni yule aliyefaulu. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba, je mwanafunzi aliyepata wastani wa 28% sawa na daraja D ana sifa zinazomwezesha kuchaguliwa kuingia kwenye ngazi ya elimu inayofuata?
 
Kiwango cha udanganyifu kwa viongozi wetu siku hizi ni kikubwa.
 
Muarobaini wa uozo wote huu ni kubadili mfumo tu. Tatizo linaanzia CCM na viongozi wake wa kujuana, ushemeji, ujomba nk. Vijana tujipange, 2015 tujitokeze, tupige kura tuiondoe CCM madarakani. 2015 tuna kazi moja, tuna kazi ya kuiondoa CCm madarakani, bila ya kujali sera nzuri za CCM au sera mbaya za CHADEMA ( kama zitakuwepo, kitu ambacho sikitegemei), agenda yetu kubwa iwe ni kuiondoa CCm madarakani. Hapa tutaweza kuijenga Tanzania tuitakayo.
 
hapa serikali inatayarisha watu wa kuja kuwa waalimu wa shule za msingi. Huu ndio ukweli mtupu kwani hawa waliopata ufaulu wa 28% wengi wao watakuja kuangukia kwenye division 4 na hatimaye kukimbilia kwenye ualimu kwani huko ndiko kunakowapokea watu wa aina hii. Unafikiri waalimu hawa watawezaje kuja kutoa msingi imara wa watoto wetu? watu wasio na msingi watawezaje kwenda kuweka msingi? ni ukweli kuwa tunazidi kuididimiza elimu yetu na kama hatutachukua hatua mapema, tutanyanyaswa sana katika ngazi za kitaifa na kimataifa. Narudia tena, muarobaini wa haya ni Kuiondoa tu ccm na Kuiweka CHADEMA madarakani 2015. hakuna haja ya kusikiliza sera za ccm wala za CHADEMA, agenda yetu ni moja tu, kuiondoa CCm madarakani. basi! Wewe ambaye hujachoshwa na uongozi wa CCM ni yule unayefaidika kifisadi, kirushwa na uongozi wa ccm.
 
Tusubiri kiama kingine cha matokeo ya form 2. Hapo watachukuliwa hadi watakao pata wastani wa 15.
Magamba wameshindwa kusimamia mfumo wa elimu Tanzania
 
Serikali ya CCM inafanya makosa makubwa kwa kuifanya sekta ya elimu kuwa shamba la bibi la kufanyia siasa. Ni kweli kuwa zoezi la selection lilisimamishwa baada ya REO's kupokea maagizo toka juu na liliporudi kigezo cha mwanafunzi kuchaguliwa kilishushwa toka alama 100/250 hadi 70/250 sawa na 28%. Kabla zoezi halijasimamishwa hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba kuna shule zingepokea wanafunzi 20 kati ya 160 kwa mfano, ambao ni uwezo wa shule kuwa 'accomodate'. Kwa hiyo kitendo cha waziri kuutangazia umma kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na sekondari kimeongezeka kwa 8.8% kilikuwa na nia ya kuwaaminisha watu kuwa ufaulu umeongezeka kwa kuwa anayechaguliwa ni yule aliyefaulu. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba, je mwanafunzi aliyepata wastani wa 28% sawa na daraja D ana sifa zinazomwezesha kuchaguliwa kuingia kwenye ngazi ya elimu inayofuata?

Kazi ipo
 
wanafunzi wakipitishwa kwa alama ndogo kiasi hiki inakuwa vigumu sana kusoma masomo ya sekondari. hali sekondari ni kukatisha tamaa tutaona matokeo ya fm 2 karibia nusu wanaweza kushindwa kupata wastani wa asilimia 30. sijui huko kurudia itakuwaje.
 
Hamjachakachuwa matokeo ya waislaam safari hii
 
Hamjachakachuwa matokeo ya waislaam safari hii
 
Maana ya kufaulu ni kupata maksi ambazo ni PASS na si maksi za kuchaguliwa. Mnaweza kumaliza kumaliza form four wote mwaka wenu mkapata division one, lakini kwa vile nafsi ni chache maksi za kuchaguliwa zikawekwa na wengine wenye division one wakaachwa.
Mwaka unaofuata wengi wao wakapata division three na wote wakachaguliwa. tofautisha maksi za ku pass na mstari unaochorwa kwa waliopass kwa ajiri ya kuchaguliwa.

Mkuu; hapo umenichanganya . Kama wote wana division one yet hawawezi kuchaguliwa wote maana yake nini? na kama wote division three wachaguliwe wote maana yake nini? Ninini maana ya mthiani? Ama kwreli kazi tunayo. Hivi ktk mfumo huu wangapi wamepotezwa? Je kama tungekuwa sahihi ktkt mfumo wetu waelimu tungekuwa wapi?
 
Mpaka tufikie 2015, mengi tutashuhudia. Time will tell, let's wait and see!!
 
Jaman wana janvi na watanzania wote kwa ujumla hili ni janga na hakuna siri tena ila ni dhahili kwamba ccm wamedhamilia kuliangamiza taifa la Tanzania na kuliuza kwa bei nafuu kwa walowezi walio soma kwan,
  • kumpeleka sekondari mtu aliyepata alama 70 {28%) kat ya 250 ni kuua elimu na kuua elimu = kuua Taifa eti kwa kisingizio cha KIJINGA Kwamba madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi hayatapata watoto na kwamba hizo nguvu za wananchi zitapotea bure. this is another nonsense and childish! NA KAMWE TUSIIKUBALI.

MY TAKE!
1. NAFIKILI HUU NI WAKATI MUAFAKA BADALA YA KUENDELEA KUTOA MAONI HUMU JAMVIN SASA WATANZANIA TUUNGANISHE NGUVU ZETU KWA PAMOJA NA KUYAPINGA MAKOTEO HAYA ILI WACHAGULIWE WATOTO WALIOPATA 40% NA KUINDELEA NA C VINGINEVYO. KWANZA NI VIKAO GANI HALALI VYA WADAU WA ELIMU PAMOJA NA BUNGE VILIVYOKAA NA KUKUBALIANA KUTELEMSHA VIWANGO VYA UFAURU?

2. TUUNGANISHE NGUVU KUSHINIKIZA WAZILI WA ELIMU KUSTEP DOWN KWAN AMEONESHA KUWA NA NIA MBAYA KWA TAIFA LETU.
 
Tanzania itaendelea kuporomoa elimu yake kwa sababu wanaopewa dhamana ya uwaziri wa elimu si walimu mfano huyu mheshimiwa ni mhandisi . Lakini pia sera ya elimu haina wasimamizi kwa sasa.
 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ameundaganya umma kuwa kiwango cha ufaulu kimeongezeka huku kukiw na habari za uhakika kutoka kwa Maafisa Elimu wa Mikoa kuwa baada ya kukamilisha zoezi la usajili walitakiwa wachague upya wanafunzi baada ya kuona hali ilikuwa mbaya sana. Waliagizwa kuchagua wanafunzi hadi waliopata alama 70/250.

Sasa kama mwaka 2011 walichagua hadi aliyepata alama 100/250, je Waziri wa Elimu yuko sahihi kudai kuwa idadi ya waliofaulu imeongezeka bila kuwaambia watanzania ukweli kuwa ufaulu wa mwaka huu ni kupata 28% badala ya 40% ya miaka yote?

Je hawa maafisa elimu wameamua kumsingizia Waziri kwa malengo yapi eti walipewa maelekezo? Wadau toeni ufafanuzi nimeshindwa kuelewa kilichotangazwa leo kuhusu matokeo ya darasa la 7

Hii habari niliiandika juzi kuhusu zoezi la uchakachuaji lililokuwa likendelea kwenye halmashauri, watu wakafikiri natania lakini leo limesemwa hadharani. Kuna kitu kidogo wameicha na ni kuwa wamechukau hadi maksi 60/250 kwa wastani wa maswali maksi kumi na mbili kwa kila mtoto eti ili kujaza madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi. je swali kujaza madarasa au kuchagua wanafunzi wanaostahili kuendelea na elimu ya sekondari, hii ndo Tanzania kila kitu blah blah tu. ndo serikali ya ccm bwana. na haya ndo matokeo ya mgomo wa ualimu.
 
Back
Top Bottom