Kawambwa Amechakachua matokeo ya Darasa la 7 2012

Kawambwa Amechakachua matokeo ya Darasa la 7 2012

Nimesoma gazeti la MWananchi wameandika kuwa MATOKEO YA DARASA LA SABA AIBU.
Waliopata Daraja D ano wachaguliwa kuendelea na Sekondari .
Hali ya ufaulu ni kama ifuatavyo
Daraja A (alama 201 - 250) - 0.34%
Daraja B ( alama 151 - 200) - 4.54%
Daraja C ( alama 101 - 150) - 24.82
Daraja D ( alama 51 -100) - 58.82%
Daraja E ( Alama 0-50) - 8.18%

Waziri wa Elimu Kivuli Kamanda wetu Susan Lyimo ameshaanza kuyafanyia kazi amesema anasubiri apate taarifa rasmi za kitaaluma za matokeo ili kambi ya upinzani iweze kutoa tamko rasmi. Kwa hiyo wale wenye taarifa za kuaminika wawasiliane naye ili aweze kufanyia kazi mara moja.
Simu yake ni 0715 582 414.

Source: Gazeti la Mwananchi 21/12/2012
Kwa hali hiyo kazi ipo madogo wanatia huruma safari yao ya miaka saba mavuno ndiyo hayo?? Na bado huko walikopelekwa watatoka na nini?
 
Kawambwa,Mulugo na wengne wa type hiyo wote ni mazao ya Mshua...na anafanana nao haswa.Tutegemee kuboronga zaidi.
 
hawa watoto wanajuana , na mtoto wa darasa la 6 anapomuona rafiki yake wa darasa la 7 asiyejiweza darasani amechaguliwa kwenda sekondari inamfanya huyu mtoto mwingine asione umuhimu wa kusoma kwa bidii kama hata "wajinga" wanaingia sekondari
 
Hivi hili jambo lina ukweli kwa kiasi gani maana nikisoma naona ni kama sinema za kanumba. Mtu mwenye dhamana kubwa namna hiyo anaweza kufanua hayo yaliyoandikwa kwenye thread hii. Kwani hana washauri?
 
acheni watoto waende secondary,elimu ya secondary ni ya lazima siku hizi,acheni watoto wapelekwe ata kama ni wote wasome,mbona mna wivu sana
 
Elimu ya tanzania imeshakufa, tunaizika sasa. Mwanafunzi wa kidato cha nne wa sasa anashindwa hata kuandika essay ya effects za slave trade on east africa. Wanabaki kufahamu lugha ya kuchati hasa na vijana wenzao.
 
Ni hatari sana kwa taifa linalohitaji maendeleo kufanya mchezo katika elimu. Tutajutia sana kwa kizazi hiki tunachokiharibu.siasa za magamba at work.
 
Nasikia hadi waliopata 60% nao wamechaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari,tatizo watoto wao hawasomi hapa.
Naomba nikusaidie zaidi,
Hiyo 60 ni kati ya 250 kwa maana kwmb 12 kati ya 50 kwa kila somo kwn kuna masomo matano. Kiukweli watanzania tunadanganywa na watendaji wasio na uwezo wa kutathmini mambo, km kiwango cha ufaulu kimeshuka na kusababisha wao kuwachagua hao waliopata Alana ndg ili wajaze shule za kata bas wasidanganye umma kwmb ufaulu umeongezeka bali waseme waliofeli wengi wamebebwa kwenda sekondari.
Inasikitisha sana doctor na waxed kishndwa kutathmini
 
Kawambwa hamna kitu pale, yafaa aende kuwa VC wa University of Bagamoyo ila Elimu anaiua


acheni kujibu hii hoja kishabiki......tatizo maticha wanafuataga mkumbo saaaana bila kufikiria kwa kina......
hebu mtutajie waziri mmoja tu wa elimu ambaye mlishawahi kumsifiaaa au mnataka waziri Malaika acheni ukilaza. kwa hiyo mnataka sekondari zikose watoto kisa alamaa...????
 
Wadau, matokeo yakiwa mazuri tunamlaumu Mh Waziri kuwa amechakachua, ametoa Kidato cha Nne kama yalivyo tunadai amechakachua, sasa yeye afanyeje?
 
Nashangaa hata mimi, watoto wa siku hiz hawasomi ni pasua kichwa, hebu fikiria wanachora picha na kuandika bongo flevar katika karatasi la kujibia mitihani
 
60/250 -70/250 = 24-28% ya masomo kwa kiswahili ni kweli tunainua elimu au tunadidimiza elimu. Kawambwa walah tena juzulu acha usanii. hivi wewe watoto wako wanasoma bongo kweli huu ni USANII MKUBWA. Tuambie hivi TASNIFU YAKO NI HAK'HI AU YA KUCHAKACHUA. WABONGO TUANZE UTAMADUNI WA KUJIUZULU.HII TABIA YA KUGANDA KWENYE SITI HALI HUNA SIFA NI MBAYA SANA KWA MUSTAKHABLI WA TAIFA HILI
 
effects za slave trade on east africa×××××
effects za slave trade in East Africa√√√√√
 
Tutegemee nini kwenye matokeo ya mtihani wa Darasa la saba utakaofanyika kesho baada ya wahusika kuapa kuwa ufaulu utafika asilimia 60 wakati hata matokeo ya mwaka jana ilikuwa ni uchakachuaji mtupu na kiwango kilimuwa cha chini sana hadi alama za kwenda Kiato cha I zikashushwa toka 100 hadi 70 kati ya 250? kuna muujiza gani umefanyika hadi wizara inategemea ufaulu upande mara 2 ya mwaka jana?

Ni vema kufuatilia kwa makini hatua zote za mtihani huu kwani ipo hatari kubwa ya kujenga taifa la mbumbumbu ndani ya kivuli cha uchakachuaji
 
Back
Top Bottom