Kauli za Sisi 'Wanasiasa' ndiyo muda mwingine zinatufanya 'Wananchi' wasituamini na waendelee kumpa 'Kura' Rais Magufuli na CCM yake tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,551
108,888
Kauli ya Mwanasiasa GENTAMYCINE wiki Mbili zilizopita....

"Namalizia Kampeni zangu za Kupambana na Magufuli ila Uchaguzi Mkuu ukiisha tu naenda Kijijini Butiama Mkoani Mara Kutibiwa zangu Kienyeji kutokana na Matatizo makubwa sana niliyoyapata ya Kung'atwa na Mbwa Mkali wa Ziwani na Meno yake Makali 38 nilipomuomba Dereva wangu anishushe nikojoe mara moja Porini japo Yeye Meno ya Mbwa Mkali hata Moja halijampata huku nikipumzika Siasa"

Kauli ya Mwanasiasa GENTAMYCINE leo tu alipokuwa akipanda zake Treni kuelekea Mkoani Mara ( Musoma ) kupitia Mwanza....

"Naondoka hivi na hii Treni kama mnavyoona ila pamoja na kwamba naenda Kutibiwa ila huko huko Kijijini Butiama hata kama nikiwa Wodini naoshwa Majeraha na Meno ya Mbwa Mkali wa Ziwani kwani kuna mengie kama Mawili hivi yamebaki na yamekaa pabaya nitaendeleza Mapambano dhidi ya Magufuli nikiwa huko huko mpaka atoke Madarakani japo nilipokuwa hapa Dar es Salaam nilishindwa Kumtoa"

RAI yangu tu kwa 'Wanasiasa' Wenzangu wengine wa Tanzania (hasa mliogombea Urais kama GENTAMYCINE ) Msiwe 'Ndumilakuwili' Kimaelezo.
 
Anaenda kumshtaki kwa baba na mama (USA x UN).

Sasa tunacho subiri kama baba na mama watatumia vyeo vyao kama wazazi kutoa adhabu kali, ili iwe fundisho kwa watoto wengine watukutu (Uganda n.k). Au wazazi watafunika kombe mwana-wa-haramu apite (Japokua baba ameshaonesha dalili za jazba toka awali).

Na leo wakati akisafiri alisindikizwa mpaka stendi na washenga (mabalozi) watatu, mmoja wa USA (Baba), wingine wa German (Ma-mdogo), na wa mwisho alikua wa Belgium (Mlezi)... Hii imekaaje kwa nyinyi wataalamu wa siasa???
 
Anaenda kumshtaki kwa baba na mama (USA x UN).

Sasa tunacho subiri kama baba na mama watatumia vyeo vyao kama wazazi kutoa adhabu kali, ili iwe fundisho kwa watoto wengine watukutu (Uganda n.k). Au wazazi watafunika kombe mwana-wa-haramu apite (Japokua baba ameshaonesha dalili za jazba).
Hivi USA huwa ana 'Rafiki' wa Kudumu na ni Mtu wa 'Kumuamini' kabisa kama ama ukimshtakia jambo au kuingia nae hata Makubaliano yoyote tu?
 
Kauli ya Mwanasiasa GENTAMYCINE wiki Mbili zilizopita....

"Namalizia Kampeni zangu za Kupambana na Magufuli ila Uchaguzi Mkuu ukiisha tu naenda Kijijini Butiama Mkoani Mara Kutibiwa zangu Kienyeji kutokana na Matatizo makubwa sana niliyoyapata ya Kung'atwa na Mbwa Mkali wa Ziwani na Meno yake Makali 38 nilipomuomba Dereva wangu anishushe nikojoe mara moja Porini japo Yeye Meno ya Mbwa Mkali hata Moja halijampata huku nikipumzika Siasa"....
Huwa unaazisha hoja kinafiki na kwa kujificha ficha lakini mwisho wa siku kama mchwa unaota mabawa, unakuwa kumbikumbi… maCCM mna hadaa za kitoto sana
 
Mbona na kwanini 'Unaumia' Wewe Pimbi? Katika nilichokiandika hapa katika 'Uzi' wangu huu kuna mahala nimekitaja Chama cha CCM au Chako?
Unafiki Nikuona Chombo Cha Habari Kinachambua Kwa Kina Uchaguzi Wa Marekani Lakini Wameshindwa Kabisa Kwenda TCRA Kupata Ufafanuzi Wa Tatizo La Mtandao.

Huwezi kutoboa bongo bila unafiki na kumiliki kiwango fulani cha ujinga kichwani mzee…
 
Mwache akapunguze maumivu tuu hamna namna

Amepingwa kwenye udiwani, ubunge na urais
Akapingwa kwenye maandamano ya bila kikomo
Mzee, wapinzani hawahitaji hisani ya KIKATIBA, kimarekani ,KISHERIA au CHAMA TAWALA kupata viti vya Ubunge na 12% ya viti ili waweze kuunda KAMBI RASMI RASMI UPINZANI Bungeni… wanahitaji UWANJA sawa kufanya siasa za ushindani, na kuondoa wapambe kama wale wa NEC
 
..Mabalozi waidhalilisha serikali, vyombo vya dola, na mahakama za Tanzania.

..haiwezekani wamuondoshe nchini mtu anayetakiwa kuwa mahakamani kujibu mashtaka.

..Nini maana ya kuwa nchi huru, kama mabalozi wa nchi za kigeni wanaweza kufanya wanavyotaka?
Zile bomba za makachero wa USA sio za mchezo,polisi waliokuwa wanamsubiri Lissu ilibidi waishie kuchungulia kwa mbali😁😁😁!
Namtakia kheri Lissu huko aliko,aachane na hizi maiti za Tanzania mpaka zitakapofufuka!
 
Mzee, wapinzani hawahitaji hisani ya KIKATIBA, kimarekani ,KISHERIA au CHAMA TAWALA kupata viti vya Ubunge na 12% ya viti ili waweze kuunda KAMBI RASMI RASMI UPINZANI Bungeni… wanahitaji UWANJA sawa kufanya siasa za ushindani, na kuondoa wapambe kama wale wa NEC
Kwanza hiyo Chadema ya 2020 ilikua chama pinzani kwa maslahi ya nani?
 
..Mabalozi waidhalilisha serikali, vyombo vya dola, na mahakama za Tanzania.

..haiwezekani wamuondoshe nchini mtu anayetakiwa kuwa mahakamani kujibu mashtaka.

..Nini maana ya kuwa nchi huru, kama mabalozi wa nchi za kigeni wanaweza kufanya wanavyotaka?
Unao ushahidi juu ya hili? Japokuwa mtoa mada ni mnafiki kama muimba taarabu
 
Unao ushahidi juu ya hili? Japokuwa mtoa mada ni mnafiki kama muimba taarabu

..TL alikuwa hana passport. serikali imekwenda kumtengenezea passport na kuwaruhusu mabeberu wamuondoe nchini.

..sasa huko siyo kujidhalilisha mbele ya mabeberu? TL si ana kesi 6 za kujibu mahakamani? imekuwaje serikali inayomshtaki imruhusu aondoke baada ya kukwepa kesi hizo kwa zaidi ya miaka mitatu?
 
Alikuwa hana passport? Alikuja vipi toka Ubeligiji?

Kwani kesi za jinai zina mwisho? Ipo siku wakimuhitaji watamuita tu. Habari za kujidhalilisha ni hoja za kitoto.
 
Alikuwa hana passport? Alikuja vipi toka Ubeligiji?

Kwani kesi za jinai zina mwisho? Ipo siku wakimuhitaji watamuita tu. Habari za kujidhalilisha ni hoja za kitoto.

..Ni aibu serikali kupokea amri na maelekezo ya mabalozi / wazungu kana kwamba Tanzania siyo nchi huru.

..Unafikiri balozi wetu Ujerumani au Marekani anaweza kuziamuru serikali za nchi hizo kama ilivyotokea hapa nyumbani?
 
Back
Top Bottom