FCR
JF-Expert Member
- Nov 7, 2018
- 213
- 177
Tatizo watendaji wake wanavichwa Kama vya kamongo hawajui jpm anataka nini
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
OSHA nnaosha nini?
Sifa moja ya mtu kuwa mwalimu Tanzania ni kufeli au ukilaza,Mimi sijawahi kuwa na imani na hawa watu kwenye issue yoyote zaidi ya kushika chakiMwalimu Magufuli
Tatizo hapa ni kuwa na Serikali ya Magufuli, Tanzania ya Magufuli, Wananchi wa Magufuli na CCM ya Magufuli. Wafanyakazi wake wanafanya kazi ya Magufuli.Mtu anataka kujenga kiwanda chake anatafuta ardhi mara sijui kuna NEMC sijui kuna OSHA, unaosha nini?, we umelikuta liardhi la Mungu hapo unaangalia sijui sijui! kuna vibali vya hovyo, tunajichelewesha wenyewe.
Na mimi ndio Rais nilisema nikiwa Kibaha na nasema sasa hivi hapa, Mwekezaji ukipata ardhi anza kujenga kiwanda, anza kujenga na mambo mengine yatafuata baadaye, halafu ndio niwaone hao OSHA sijui NEMC wanasumbua.
Uchumi wetu unakua kwa 7%, Tanzania ni moja ya nchi tano Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi sana.
Viwanda vinahitajika, mamlaka zote zinazohusika endeleeni kuhamasisha uwekezaji katika Sekta ya viwanda, tengenezeni mikakati ya kulinda viwanda vilivyojengwa, ni faida kwa Taifa letu.
Mtu akija anataka kuwekeza, kesho yake apewe eneo aanze kuwekeza, ni lazima twende na kasi hiyo.
Nataka nikimaliza kipindi changu niiache nchi ikiwa safi, tumechelewa mno.
Nimeambiwa na Balozi Sarah Cooke kuwa kuna matatizo katika mfumo wetu wa uwekezaji, ndio maana nawaambia watumishi wangu waache hayo, Mtu ana hela yake mnamzungusha mwaka mzima kisa kibali.
Nimefurahi kusikia kiwanda kimetoa Milioni 250 kwa ajili ya kuchangia shughuli za kijamii pamoja na azma yao ya kutaka kuwafundisha wakulima wa chai mbinu za kisasa za kilimo hicho.
Natoa wito kwa Mabalozi, kama kuna wawekezaji wanataka kuwekeza nchini na wanazungushwa, hata kwa siku 30 tu, nileteeni majina ya huyo anayewazungusha, niwazungushe na wao kama tairi.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kilikuwa hakifanyi vizuri ndio maana nikakipeleka chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, lakini kama wakiendelea hivyo, nitawaweka chini ya Ofisi yangu
Tanzania ni nchi ambayo wawekezaji wanapenda kuja kuwekeza, lakini kuna watu ambao ni vikwazo kwa uwekezaji nchini.
Nawapongeza sana Wastaafu hawa akina Makinda na akina Luhanjo kwa kuwashawishi Wawekezaji waje hapa, hawa wazee wamefanya vizuri sana kuwaleta Wawekezaji hapa, pengine hata hiki kiwanda kingejengwa kwingine.