Kauli za Rais Magufuli akiongea na wananchi Njombe leo

Kwa style hii ya kauli na hotuba za namna hii itatuchukua miaka mingi sana kutoka hapa tulipo,sheria tuzitunge wenyewe Leo unazivunja hadharani kwa ajili ya kuwafurahisha wajinga,hivi kweli unaweza anza ujenzi kisha baadae ndio wake watu Wa aridhi,mazingira,afya n.k ndio mnaanza kujadili,this is a shame.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viva JPM, ungeenda mbali zaidi wawekezaji wote wapite katika ofisi yako, wewe ungewapa ardhi na vibali vya uwekezaji fasta fasta mambo yangeenda. Hawa watendaji wako wanachelewesha sana uwekezaji na viwanda.
 
Mtu anataka kujenga kiwanda chake anatafuta ardhi mara sijui kuna NEMC sijui kuna OSHA, unaosha nini?, we umelikuta liardhi la Mungu hapo unaangalia sijui sijui! kuna vibali vya hovyo, tunajichelewesha wenyewe.

Na mimi ndio Rais nilisema nikiwa Kibaha na nasema sasa hivi hapa, Mwekezaji ukipata ardhi anza kujenga kiwanda, anza kujenga na mambo mengine yatafuata baadaye, halafu ndio niwaone hao OSHA sijui NEMC wanasumbua.

Uchumi wetu unakua kwa 7%, Tanzania ni moja ya nchi tano Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi sana.

Viwanda vinahitajika, mamlaka zote zinazohusika endeleeni kuhamasisha uwekezaji katika Sekta ya viwanda, tengenezeni mikakati ya kulinda viwanda vilivyojengwa, ni faida kwa Taifa letu.

Mtu akija anataka kuwekeza, kesho yake apewe eneo aanze kuwekeza, ni lazima twende na kasi hiyo.

Nataka nikimaliza kipindi changu niiache nchi ikiwa safi, tumechelewa mno.

Nimeambiwa na Balozi Sarah Cooke kuwa kuna matatizo katika mfumo wetu wa uwekezaji, ndio maana nawaambia watumishi wangu waache hayo, Mtu ana hela yake mnamzungusha mwaka mzima kisa kibali.

Nimefurahi kusikia kiwanda kimetoa Milioni 250 kwa ajili ya kuchangia shughuli za kijamii pamoja na azma yao ya kutaka kuwafundisha wakulima wa chai mbinu za kisasa za kilimo hicho.

Natoa wito kwa Mabalozi, kama kuna wawekezaji wanataka kuwekeza nchini na wanazungushwa, hata kwa siku 30 tu, nileteeni majina ya huyo anayewazungusha, niwazungushe na wao kama tairi.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kilikuwa hakifanyi vizuri ndio maana nikakipeleka chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, lakini kama wakiendelea hivyo, nitawaweka chini ya Ofisi yangu

Tanzania ni nchi ambayo wawekezaji wanapenda kuja kuwekeza, lakini kuna watu ambao ni vikwazo kwa uwekezaji nchini.

Nawapongeza sana Wastaafu hawa akina Makinda na akina Luhanjo kwa kuwashawishi Wawekezaji waje hapa, hawa wazee wamefanya vizuri sana kuwaleta Wawekezaji hapa, pengine hata hiki kiwanda kingejengwa kwingine.
Tatizo hapa ni kuwa na Serikali ya Magufuli, Tanzania ya Magufuli, Wananchi wa Magufuli na CCM ya Magufuli. Wafanyakazi wake wanafanya kazi ya Magufuli.
 
Back
Top Bottom