Bashungwa Awapa Nguvu Wawekezaji wa Viwanda Karagwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

BASHUNGWA AWAPA NGUVU WAWEKEZAJI WA VIWANDA KARAGWE.

Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa amewahakikishia Wawekezaji wa Viwanda katika Wilaya Karagwe mkoani Kagera kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Wawekezaji hao.

Ameeleza hayo katika ziara ya kutembelea Ujenzi wa kiwanda cha cha kusindika maziwa, vyakula vya mifugo, Shamba la mfano la mahindi, eneo la ufugaji wa ng’ombe, mbuzi pamoja na kondoo vya Kahama Fresh Ltd pamoja na kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Hlucky Kombucha Investment.

Akikagua Ujenzi wa Kiwanda cha Kusindika Maziwa chenye uwezo wa Kuchakata lita 20,000 kwa siku, Bashungwa amempongeza Mwekezaji kwa kuunga mkono Serikali katika jitihada za kujenga Uchumi wa Viwanda.

“Kwa niaba ya Serikali nakupongeza Jasam kwa kuleta uwekezaji mkubwa katika wilaya Karagwe, Kama mnavyofahamu mkoa wetu wa Kagera ndio wenye rachi nyingi za mifugo, Kupitia kiwanda hiki kitasaidia kuongeza thamani malighafi zote zinazotokana na mifugo na kilimo”

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa sehemu ya kiwanda hicho kinachosindika Mafuta ya alizeti pamoja na kuchatakata mahidi vitasaidia kuongeza bidhaa ambazo zitakuwa zimeongezea thamani mazao kwa ajili ya mauzo ya ndani na nje ya nchi.

Wakati huo, Bashungwa ametembelea kiwanda cha Kutengeza vinywaji cha Hlucky Kombucha investment ambao ni wazalishaji vinywaji vinavyotokana na mazao ya Kilimo.

Ameeleza kuwa kiwanda hicho kinachotumia malighafi zinazotokana na mazao mbalimbali, kinasaidia wakulima kuinua vipato vyao na kuwa na uhakika na mazao wanayolima katika mkoa wa Kagera

Bashungwa amesema Uwekezaji huo umesaidia kuzalisha ajira na kulipa kodi ambacho zinaiwezesha Serikali kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Wawekezaji hao, Mkurugenzi wa kampuni ya Kahama Fresh Limited, Jossam Ntangeki pamoja Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Hamis Jumanne katika nyakati tofauti wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kufanya uwekezaji ambao unasaidia kutoa kuongeza vipato vyao na pato kwa serikali kupitia ulipaji wa kodi.
 

Attachments

  • GBVrO-NXwAA2q6k.jpg
    GBVrO-NXwAA2q6k.jpg
    365.9 KB · Views: 6
  • GBVrO-dXUAAVrgX.jpg
    GBVrO-dXUAAVrgX.jpg
    374.6 KB · Views: 4
  • GBVrO-oWcAA5riA.jpg
    GBVrO-oWcAA5riA.jpg
    283.9 KB · Views: 5
  • GBVrO-TW4AACcSf.jpg
    GBVrO-TW4AACcSf.jpg
    243.4 KB · Views: 4
  • GBVrRsyXIAAtZfD.jpg
    GBVrRsyXIAAtZfD.jpg
    244.9 KB · Views: 5
  • GBVrRsyWUAAUpFZ.jpg
    GBVrRsyWUAAUpFZ.jpg
    454 KB · Views: 5
  • GBVrUf1WkAAVr8B.jpg
    GBVrUf1WkAAVr8B.jpg
    325.8 KB · Views: 5
  • GBVrUfxWIAAIZah.jpg
    GBVrUfxWIAAIZah.jpg
    305.6 KB · Views: 6
  • GBVrUf_XIAA7R9_.jpg
    GBVrUf_XIAA7R9_.jpg
    258.7 KB · Views: 5
Back
Top Bottom