Kauli ya upendeleo ya rais Kikwete clouds fm

Huyo JK ameamua kuwapa promo hiyo Clouds, kwa kuwa anajua, kuanzia wamiliki wake Kusaga na Ruge, pamoja na watangazaji wao, akina Kibonde, Bonge na wengineo, nao ni kama wamekunywa maji ya bendera ya CCM.

Wao wakiingia studio ni kazi moja tu, kuwapamba magamba na kuwaponda wapinzani.

Hiyo radio, mimi binafsi naihate sana, kwa kuwa inajitahidi kwa kila hali kuchelewesha mabadiliko

hehheheeee,,,,,na redio uhuru je???
 
kweli hapo ameteleza.Nadhani bado anafikiri Clouds hii ya sasa bado ina influence kwa vijana kama enzi za akina ML Chriss,Bobby,seven,Dj Boggie Master,Amina Chifupa n.k
Clouds sio radio ya burudani tena bali imejaa siasa na kufanya kazi za TBC.

Umenena vema kimtazamo mkuu. Watu wengi wameacha kusikiliza hii radio kwa sasa na naweza kukuhakikishia kuwa tangu mwaka huu uanze hawa jamaa wamepoteza wasikilizaji wengi sana. Ubunifu wao tayari ushafika kikomo limebaki jina tu na back up ya wanasiasa ambao nao wananufaika kimaslahi kwa style wanayoijua wao.
Wacha waendelee kujidanganya na hizo takwimu ili waendelee kupata soko lao kibiashara. Nani anajua huenda wanalipa hela kutengeneza hizi takwimu.

NB: Kama kuna mtu ana data za mauzo ya Fiesta tafadhali atujuze hapa.
 
Clous Fm mwisho Kongowe, Hata Bunju inapatikana kwa shida halafu mnasema inawasikilizaji wengu kuliko zote.?.hilo sikubaliani nalo.. naona hapa wamepata promo ya bure kutoka kwa presidaa..
 
Mkuu wa kaya amekosa hekima kidogo na kuteleza kwa kauli yake hiyo. Anachosahau ni kwamba ameharibu hata confidence ya vituo vya habari vya serikali kama TBC na Uhuru. Hili ni tatizo
 
Mkuu wa kaya amekosa hekima kidogo na kuteleza kwa kauli yake hiyo. Anachosahau ni kwamba ameharibu hata confidence ya vituo vya habari vya serikali kama TBC na Uhuru. Hili ni tatizo

We ukifanya biashara nzuri hufai kupongezwa? Hiyo TBC haiko kibiashara zaidi kama radio zingine
 
Mimi binafsi ile sehemu ilinikera pia. Na ninaamini kama rais hakutakiwa kuongea kwa namna alivoongea. Ingetosha tu kuweka kama mtoa mada alivyoshauri kwa lengo la kutambua mchango wao bila kushusha michango ya media zingine.

Mbaya zaidi wamechukua hicho kipande cha hotuba na kufanya kama tangazo.
 
jamani kuna kipindi gani kinaweza kunishawishi kuisikiliza hiyo station?
 
Nimesikitishwa na kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete hivi majuzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee alipokuwa akihutubia Warsha ya "Kamata Fursa Twenzetu" iliyoandaliwa na kituo cha radio cha Clouds FM. Rais Kikwete katika mambo mengi aliyosema ni pamoja na kuwa hakuna kituo cha radio kinachosikilizwa nchini Tanzania zaidi ya CLOUDS FM.

Huenda Mh Rais ni kweli anao utafiti wa Kisayansi kuthibitisha hoja yake, lakini akiwa kama Rais ambapo katika nchi yake kuna vyombo vingi vya habari na vyenye ushindani, si busara kusimama hadharani na kutamka taasisi fulani ya kibiashara ni bora kuliko zote. Akitumia busara zaidi iwapo anaouthibitisho basi aseme kuwa CLOUDS FM ni miongoni wa vituo bora zaidi vya Radio nchini Tanzania.

Kwa upendeleo huo wa wazi na hata kupigia debe kituo hicho, huenda vituo vingine vikajisikia kutotendewa haki kama Rais wa nchi anasimama hadharani kutamka kituo bora kuliko vyote ni kipi.

Kama ni mshabiki na ana hisa katika kituo hicho, ni vyema Rais aweke kando kofia ya ukuu wa nchi na kisha atoe tamko kama KIKWETE na si RAIS WA NCHI.

Binafsi nawapenda CLOUDS FM, japokuwa si busara kama kiongozi mkuu wa nchi na mlezi wa taasisi zote nchini kutamka wazi kuwa wao ni bora kuliko wote.

Hivi CLOUDS FM inamilikiwa na nani? Sio cha Master one? Nimekosea kidogo jina anayelijua anisaidie kurekebisha
 
Mimi binafsi ile sehemu ilinikera pia. Na ninaamini kama rais hakutakiwa kuongea kwa namna alivoongea. Ingetosha tu kuweka kama mtoa mada alivyoshauri kwa lengo la kutambua mchango wao bila kushusha michango ya media zingine.

Mbaya zaidi wamechukua hicho kipande cha hotuba na kufanya kama tangazo.

Jamani jamani narudia tena maana watu mmeishupalia hoja mfu hadi mnatokwa povu, Rais hakusema Clouds ndio radio inayoongoza kusikilizwa na watz wengi, bali alisema ni "media outlet inayoongoza kwa kusikilizwa na VIJANA wengi tz". Na ndo akachomekea kuwa na yeye alishaanza kuvutika akimaanisha japo yeye sio kundi la vijana lakini alishaanza kuvutika kusikiliza.
Unaweza kuprove maneno yangu kwa kusikiliza hii "jingle" yao wanayoweka kila mwisho au mwanzo wa kipindi anayosema "Kamata fursa...." Msisitizo upo kwenye neno vijana na sio kuwa amesema inaongoza kwa kusikilizwa na watu wote generally kama mnavyoanza kuconclude.
Mwingine ukute hata hajasikiliza, kasoma tu hii thread kama mleta uzi alivyoelewa vibaya basi na mwingine kabebwa na ushawishi wa mleta uzi mule mule kichwa kichwa. Sio kila uzi hapa uko sahihi 100%, wengine wanakuja na zenye personal bias zao na wengine wanakutega tu sasa na wewe usipochanganya na zako unakuwa easily carried away na hasty generalization.
Akili za mleta uzi changanya na zako ndipo utoe hoja.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Nimesikitishwa na kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete hivi majuzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee alipokuwa akihutubia Warsha ya "Kamata Fursa Twenzetu" iliyoandaliwa na kituo cha radio cha Clouds FM. Rais Kikwete katika mambo mengi aliyosema ni pamoja na kuwa hakuna kituo cha radio kinachosikilizwa nchini Tanzania zaidi ya CLOUDS FM.

Huenda Mh Rais ni kweli anao utafiti wa Kisayansi kuthibitisha hoja yake, lakini akiwa kama Rais ambapo katika nchi yake kuna vyombo vingi vya habari na vyenye ushindani, si busara kusimama hadharani na kutamka taasisi fulani ya kibiashara ni bora kuliko zote. Akitumia busara zaidi iwapo anaouthibitisho basi aseme kuwa CLOUDS FM ni miongoni wa vituo bora zaidi vya Radio nchini Tanzania.

Kwa upendeleo huo wa wazi na hata kupigia debe kituo hicho, huenda vituo vingine vikajisikia kutotendewa haki kama Rais wa nchi anasimama hadharani kutamka kituo bora kuliko vyote ni kipi.

Kama ni mshabiki na ana hisa katika kituo hicho, ni vyema Rais aweke kando kofia ya ukuu wa nchi na kisha atoe tamko kama KIKWETE na si RAIS WA NCHI.

Binafsi nawapenda CLOUDS FM, japokuwa si busara kama kiongozi mkuu wa nchi na mlezi wa taasisi zote nchini kutamka wazi kuwa wao ni bora kuliko wote.

kazungumzia kusikilizwa na watu wengi au ubora mbona hueleweki.
 
Back
Top Bottom