Kauli ya upendeleo ya rais Kikwete clouds fm

Swali la msingi ni, je, alichosema ni kweli ama si kweli?

Kama ni kweli rais hawezi kushitakika kwa kusema ukweli.

Kama baba ambavyo hawezi kushitakika kwa kusema mtoto wake aliyefanya vizuri shuleni kafanya vizuri.Hata kama kuna wengine ambao hawajafanya vizuri.

Hiyo inaweza hata kuwa changamoto kwa yule ambaye hajafanya vizuri.

Of course kama kauli ya rais si ya kweli, atashitakika kwa kutosema ukweli.

Let's not let an overly sensitive political correctness cloud a valid sense of meritocracy.

And I am writing all this as someone who is not very impressed by Clouds FM.
 
Ukweli wa mambo ni kwamba Clouds FM iko juu. Lakini kwa vile kuna watu wachache humu hawaipendi hiyo redio kwa sababu zao za kisiasa, basi kila lisemwalo juu ya Clouds au kila litokealo wao hao watu hutafuta namna ya kuangalia sehemu ya ubaya wa hilo jambo.

Majuzi tu hapa kuna watu humu walidai eti Clouds ni meli inayozama. Clouds haiendi popote pale zaidi ya kuzidi kwenda juu. Mpende msipende.

Sasa hapa alichosema JK nacho kina ubaya gani? Kama mtu anadhani JK kasema jambo lisilo sahihi basi na atoe data zinazothibitisha hivyo. La sivyo itakuwa ni ule ule mwendelezo wa chuki unaofanywa na watu wachache sana humu JF.
 
Nimesikitishwa na kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete hivi majuzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee alipokuwa akihutubia Warsha ya "Kamata Fursa Twenzetu" iliyoandaliwa na kituo cha radio cha Clouds FM. Rais Kikwete katika mambo mengi aliyosema ni pamoja na kuwa hakuna kituo cha radio kinachosikilizwa nchini Tanzania zaidi ya CLOUDS FM.

Huenda Mh Rais ni kweli anao utafiti wa Kisayansi kuthibitisha hoja yake, lakini akiwa kama Rais ambapo katika nchi yake kuna vyombo vingi vya habari na vyenye ushindani, si busara kusimama hadharani na kutamka taasisi fulani ya kibiashara ni bora kuliko zote. Akitumia busara zaidi iwapo anaouthibitisho basi aseme kuwa CLOUDS FM ni miongoni wa vituo bora zaidi vya Radio nchini Tanzania.

Kwa upendeleo huo wa wazi na hata kupigia debe kituo hicho, huenda vituo vingine vikajisikia kutotendewa haki kama Rais wa nchi anasimama hadharani kutamka kituo bora kuliko vyote ni kipi.

Kama ni mshabiki na ana hisa katika kituo hicho, ni vyema Rais aweke kando kofia ya ukuu wa nchi na kisha atoe tamko kama KIKWETE na si RAIS WA NCHI.

Binafsi nawapenda CLOUDS FM, japokuwa si busara kama kiongozi mkuu wa nchi na mlezi wa taasisi zote nchini kutamka wazi kuwa wao ni bora kuliko wote.

Kwa vile hii thread inaonekana kushika moto, naona kuna haja ya kuunda timu ya watafiti wa kitaifa na kimataifa kutafuta kituo bora cha radio na Tv. Kwa hoja hii sioni nongwa kwa mh.JK kutoa hisia zake kama mzalendo wa TZ kwa walio mwalika. Unategemea aalikwe na clouds afu sifa wapewe radio imani,maria, tbc,magic au radio öne? Mlitaka asifie BBC, Deutch Welle au Cnn ndo furahie? Hebu ndugu zanguni tuache chuki mpaka za kujichukia wenyewe! Waswahili hatuigani maendeleo bali chuki na kurogana.Tumetawaliwa na roho ya "tukose wote" Kwa maendeleo inatubidi tuwe na wivu(+) Kama mwenzio kaandaa tukio lenye hadhi ya kumhusisha raisi wa nchi, nawe fanya hivo na zaidi kuliko kumjengea chuki. Ukijenga chuki sana unampa mwenzio nafasi ya kuibua fursa nawe kuwa kipofu wa fursa. Fursa haziletwi na roho ya kwanini bali mikono imara ikiöngozwa roho ya kudhubutu pamoja ubunifu. "Getting to the top isnt an easy task, it requires determination and hard working and these are the masters of victory"
 
kweli hapo ameteleza.Nadhani bado anafikiri Clouds hii ya sasa bado ina influence kwa vijana kama enzi za akina ML Chriss,Bobby,seven,Dj Boggie Master,Amina Chifupa n.k
Clouds sio radio ya burudani tena bali imejaa siasa na kufanya kazi za TBC.
Aisee, umenikumbusha mbali na hyo list hapo juu, ML Chriss yupo ChoiceFM radio ya inayotangaza kwa lugha ya kiingrereza, ni ndugu na CloudsFM
 
Nimesikitishwa na kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete hivi majuzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee alipokuwa akihutubia Warsha ya "Kamata Fursa Twenzetu" iliyoandaliwa na kituo cha radio cha Clouds FM. Rais Kikwete katika mambo mengi aliyosema ni pamoja na kuwa hakuna kituo cha radio kinachosikilizwa nchini Tanzania zaidi ya CLOUDS FM.

Huenda Mh Rais ni kweli anao utafiti wa Kisayansi kuthibitisha hoja yake, lakini akiwa kama Rais ambapo katika nchi yake kuna vyombo vingi vya habari na vyenye ushindani, si busara kusimama hadharani na kutamka taasisi fulani ya kibiashara ni bora kuliko zote. Akitumia busara zaidi iwapo anaouthibitisho basi aseme kuwa CLOUDS FM ni miongoni wa vituo bora zaidi vya Radio nchini Tanzania.

Kwa upendeleo huo wa wazi na hata kupigia debe kituo hicho, huenda vituo vingine vikajisikia kutotendewa haki kama Rais wa nchi anasimama hadharani kutamka kituo bora kuliko vyote ni kipi.

Kama ni mshabiki na ana hisa katika kituo hicho, ni vyema Rais aweke kando kofia ya ukuu wa nchi na kisha atoe tamko kama KIKWETE na si RAIS WA NCHI.

Binafsi nawapenda CLOUDS FM, japokuwa si busara kama kiongozi mkuu wa nchi na mlezi wa taasisi zote nchini kutamka wazi kuwa wao ni bora kuliko wote.
Huyo JK ameamua kuwapa promo hiyo Clouds, kwa kuwa anajua, kuanzia wamiliki wake Kusaga na Ruge, pamoja na watangazaji wao, akina Kibonde, Bonge na wengineo, nao ni kama wamekunywa maji ya bendera ya CCM.

Wao wakiingia studio ni kazi moja tu, kuwapamba magamba na kuwaponda wapinzani.

Hiyo radio, mimi binafsi naihate sana, kwa kuwa inajitahidi kwa kila hali kuchelewesha mabadiliko
 
vipi riz nae alikuwepo? maana nae ni mmoja kati ya vijana waliotumia fursa na kufanikiwa kibiashara
 
Ndio tatizo letu sisi binadamu roho ya kwanini mpaka lini wewe? Mpaka kufikia hatua ya kumualika mh Rais ni mojawapo ya juhudi na malengo yao ili waliopo nyuma yao wajifunze na kuiga kile wenzao walichofanya ama wabuni wazo lao la kutambulika kwa jamii,punguza lawama na chuki,chukua fursa twenzetu.
 
Kwa Tuliosoma Public Relations na Ikatuingia Vizuri na Kwa Wale Waliosoma Diplomacy na Wakaielewa Vizuri Kitendo Alichokifanya JK Kama Ni Kupewa Marks basi Angepata Alama Ya A. Kiongozi Unatakiwa Kuzungumza Kwa Mazingira Uliyopo na Alichokifanya ni Sahihi Kabisa na Ni Chachu Kwa Media Outlets Zingine Kuongeza Bidii na Inasaidia Mno ktk Kuwafanya na Wengine Pia Wawe Creative na Kuongeza Kiwango cha Competency. Kwa Akili Ya Kawaida tu Hivi Nyie Mlitaka Asifie Akina Nani Wakati Amealikwa na Hao Hao Clouds Media Group? Mlitaka Awasifie Baba zenu au Mama Zenu? Acheni UBWEGE NAZI! Kipi Mzee wa Watu Akifanya Mtamsifu? Na Nani Asiyejua Kuwa Clouds Fm ipo Juu na Wengine Mpo humu humu na Ni Wanafiki Wakubwa na Mkiwa Kwenu au Sehemu Zingine Mnasikiliza hiyo hiyo Redio. Wanaweza Wakawa na Mapungufu Fulani ila Generally Hiyo Radio Kwa Hapa Tanzania Inafanya Vizuri Sana na Nasikitika Tunavyohusisha Suala la Redio na Siasa Zetu. So Sad!!!!
 
Hata mseme vp coulds ndo redio iliyowapa ujanja wq kujua miziki kama ya akina 50 cent Dr dre snoop Dogg tupac na pia kupaisha mziki wetu wa dansi sababu mlikuwa mnasikiliza pepe kalee tuu na usisahau clouds media ndo walikupa ujuzi wa kucheza Mziki leo hii ukiingia kwanja kupitia zile beach na house party nyiingii enzi zilee so mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
Clouds FM is simply number one. Hata wale wanaoichukia hii radio au baadhi ya presenters wake wanajikuta wakisikiliza vipindi vyake. Jew them, sue them, kick them,kyke them but y'all know that Clouds FM is number one. Alichoongea mheshimiwa rais JK ni ukweli usiopingika.
 
Hata mseme vp coulds ndo redio iliyowapa ujanja wq kujua miziki kama ya akina 50 cent Dr dre snoop Dogg tupac na pia kupaisha mziki wetu wa dansi sababu mlikuwa mnasikiliza pepe kalee tuu na usisahau clouds media ndo walikupa ujuzi wa kucheza Mziki leo hii ukiingia kwanja kupitia zile beach na house party nyiingii enzi zilee so mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

yaan upuuzi unaoufanya ww ndo unajua wanafanya watu woote,ndo unaudhihirisha ushamba wako hapa,,,,pole
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom