Kauli ya upendeleo ya rais Kikwete clouds fm

Sawa Radio inayosikilizwa zaidi kweli.Ila kwanini yeye kama Rais aiseme hadharani inamaanisha hata TBC ambayo ni mali ya Serekali ni tupa kule takataka haina kitu.Kwahiyo hizi nyingine wasindikizaji tuu wapo wapo.Aaaah ''come on'' hayo maneno sio ya rais kunyasema hadharani kesho akialikwa na TBC atasema katika redio zisizokuwa na ushawishi nyie mojawapo?Wait and see......................!
 
hahahaha ukweli unauma. rais yuko sahihi ata yeye anasikiliza. mimi na miaka 5 sijasikiliza radio yoyote ya Tanzania na muda sina ni mwendo wa music na movies tu
 
wapuuzi wengi sana ktk taifa hili ndo maana wanasikiliza sana radio ya wapuuzi wenzao wanaoshabikia ushoga mpaka TCRA ikawapiga adhabu!
 
Mjomba wa Taifa hukusikiliza vizuri alichoongea Mh. Rais, alisema hakuna media inayoongoza kwa kusikilizwa na VIJANA wengi kama clouds fm. Msisitizo upo hapo kwenye neno lenye herufi kubwa, hakusema inaongoza kwa kusikilizwa na watu wengi (generally) alikuwa specific kwa vijana, ww ndo umekuja na personal bias kwa huu uzi wako.

Halafu unauliza amefanya utafiti gani kujua ndio kituo kinachoongoza Tanzania, labda ww tu ndo hujui kuwa hiki kituo kwa miaka 3 mfululizo kimekuwa Super Brand Radio station kwa Tanzania. Wewe ndo ufanye utafiti kujua hilo acha chuki bana Comrade.


Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
jamani punguzeni ngebe, clouds fm haina mshindani. ni redio ya vijana. fanya utafiti dogo. mimi sina hisa clouds fm lakini huwezi kunichomoa huko....ni mkereketwa haswa.
 
Nimesikitishwa na kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete hivi majuzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee alipokuwa akihutubia Warsha ya "Kamata Fursa Twenzetu" iliyoandaliwa na kituo cha radio cha Clouds FM. Rais Kikwete katika mambo mengi aliyosema ni pamoja na kuwa hakuna kituo cha radio kinachosikilizwa nchini Tanzania zaidi ya CLOUDS FM.

Huenda Mh Rais ni kweli anao utafiti wa Kisayansi kuthibitisha hoja yake, lakini akiwa kama Rais ambapo katika nchi yake kuna vyombo vingi vya habari na vyenye ushindani, si busara kusimama hadharani na kutamka taasisi fulani ya kibiashara ni bora kuliko zote. Akitumia busara zaidi iwapo anaouthibitisho basi aseme kuwa CLOUDS FM ni miongoni wa vituo bora zaidi vya Radio nchini Tanzania.

Kwa upendeleo huo wa wazi na hata kupigia debe kituo hicho, huenda vituo vingine vikajisikia kutotendewa haki kama Rais wa nchi anasimama hadharani kutamka kituo bora kuliko vyote ni kipi.

Kama ni mshabiki na ana hisa katika kituo hicho, ni vyema Rais aweke kando kofia ya ukuu wa nchi na kisha atoe tamko kama KIKWETE na si RAIS WA NCHI.

Binafsi nawapenda CLOUDS FM, japokuwa si busara kama kiongozi mkuu wa nchi na mlezi wa taasisi zote nchini kutamka wazi kuwa wao ni bora kuliko wote.

Acha woga Mkuu. Hapo alikuwa anaelezea hisia zake. Sidhani kama itaathiri chochote kwa vituo vingine vya redio, labda wawe na akili kama za kwako.
 
Back
Top Bottom