Kauli ya Mbowe ilaaniwe na wapenda amani

Kauli ya Mbowe ilaaniwe na wapenda amani

Unakaa mita 200 unalinda kura, ndani wakala wako anakubaliana na matokeo, unayapinga na unaandamana, polisi wanatii amri ya mkuu wa majeshi, unavyunjwa mguu na kutolewa jicho, unaswekwa rumande na sio hospitali,watoto na mke wako wanalia sana, mgombea anaapishwa.umetolewa rumande upo nyumbani ni mwezi unapita,mtoto wako anarudishwa nyumbani kakosa mahitaji ya shule,unaendelea kuugulia maumivu,mkeo amekuchoka anakusimanga maana alikwambia ukipiga kura urudi, anataka kuondoka,aliyek
wambia linda kura yupo bungeni anawapa poleni wale wote walioumizwa wakati uchaguzi na kusaini posho anatuma pesa za ada kwa mwanae anayesoma kenya..." ushauri wangu, piga kura kwa mgombea wako kisha endelea na ratiba zako."

Mbowe mjanja sana, kaishapiga hela mabilioni, sasa kwa kuwa anajua baada ya oct 25 wana chadema watamuhoji, anaamua kuwasakizia wakapigwe waumie wawe bize kuuguza majeraha wasipate muda wa kumuhoji hayo mabilioni, wakatia atakua keshasepa nje nchi,! Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Mbowe mjanja sana, kaishapiga hela mabilioni, sasa kwa kuwa anajua baada ya oct 25 wana chadema watamuhoji, anaamua kuwasakizia wakapigwe waumie wawe bize kuuguza majeraha wasipate muda wa kumuhoji hayo mabilioni, wakatia atakua keshasepa nje nchi,! Akili za kuambiwa changanya na za kwako.

Acha kuweweseka, kura lazima zilindwe kwa gharama yoyote
 
wewe mwenyewe utaangalia hali ya usalama katika eneo lako, na ukijiridhisha kuwa dalili za kusababisha fujo hazipo, basi ukishapiga kura tembea mita 200 kutoka kituoni na ubaki ukiangazia macho kituoni kama utaona kinachoendelea humo ndani...! Lakini ukiona kuna dalili isiyo njema ni vema ukarudi nyumbani kabisa....! Unavyoambiwa piga kura then nenda nyumbani ijulikane tu kuwa ni ushauri tu ili kuepusha yanayoweza kutokea....!

Mfano: hivi ni nani aliwahi kulazimishwa asifanye biashara usiku? Si kweli kuwa kila mtu huangalia usalama wa biashara yake? Basi hii ni kwamba wengi wetu huwa hatuna uwezo wa kustahimili furaha au huzuni....!

Dalili za fujo ni kama ifuatavyo;
  1. Kuwepo kwa walevi katika eneo
  2. Ubishi au majibizano kati ya washabiki tofauti katika eneo
  3. Kuwepo baadhi ya watu wanaoshangilia kabla hata matokeo kutoka
  4. Kuwepo na maneno yanayoashiria, au kukumbusha matusi wakati wa kampeni, au majigambo, au chuki na hasira
  5. Kuonekana kwa wageni ambao sio wa kawaida katika eneo
  6. Dalili za kampeni kuendelea katika eneo
  7. Baadhi ya watu kutembea na picha za wagombea wao katika eneo
  8. Baadhi ya watu kutoa kauli za vitisho katika eneo
  9. Kujadili matokeo ya vituo vingine na kuanza kushangilia au kuchukia

So, jipime mwenyewe kama unaweza kukaa kusubiri matokeo au lahhh!

Kura lazima zilindwe kwa gharama yoyote, naona maccm yanaweweseka
 
Hivi ni kweli hakuna Sheri'a ya kuruhusu kukaa Mita Mia mbili? Maanake usikute ipo ila serikali ndiyo inajichanganya?
 
nani asiyemjua mbowe ni msanii? anataka kuvuruga amani tuliyonayo watanzania ..... Ukawa mshaurini mbowe awe na huruma na wananchi
Kwa nini msiishauri ccm iwe na huruma na wananchi baada YA miaka yote kutudhulumu kutunyanyasa na kutupuuza????! Mmeona ya Ukawa machafu ya ccm hamuyaoni acheni hizo. Mbowe ni mwananchi anayo haki ya kutetea kile anaamini ni kwa manufaa ya wananchi
 
Kwenye kampeni zenu mnatubeba na malori,fuso na ma-uda, tena mnatupa, elfu 10,tisheti na kofia! Kama haitoshi mnawapandisha akina daimondi na ali kiba jukwani ili watu wajae kwa wingi sana!!! Kiasi mnaita wenyewe mafuriko mara gharika! Yani safi hakuna shida amani haiwezi vunjika hapo!

Ajabu tukisha piga kura hamtutaki tena tukae vituoni tusubiri matokeo ya mlichokuwa mkitupigia kampeni! Eti tutahatarisha amani!

HIVI UNAWEZAJE KUISHI NA MKE ASIYE KUPENDA?? LAZIMISHENI MNAVYOWEZA KUTAWALA NCHI HII LAKINI JUENI WANANCHI WENGI HAWAWAPENDI.

Uvivu wako unakufanya uwe masikini hadi unalipwa 10,000 na kupandishwa malori. Badilika
 
Sheria nyingine za kipuuzi sana, eti watu wakae mita 200 kutoka vituo vya kupiga kura!
Sasa sisi wenye makazi yaliyo ndani ya mita 200 ina maana tusikae majumbani kwetu siku hiyo? Halafu wanasema matokeo yatabandikwda nje ya vituo baada ya kura kuhesabiwa, sasa wanamuwekea nani hayo matokeo ilhali hawataki watu wawepo eneo hilo? PUMBA KABISA

Mbona matokea ya mtihani wa darasa la saba yanabandikwa katika mbao elimu na watu hawapo,utayakuta siku ya pili
 
Wake na Watoto wa Lowasa,Mbowe,Mnyika,Tundu LISSU,Sumaye,Kingunge.Godbless Lema,Mchungaji msigwa n.k hawajawahi hata siku moja shiriki maandamano hatarishi.Wakati wa maandamano hatarishi huwa wako majumbani mwao au Ulaya wakila Kuku kwa mrija.

Hawa watu wamekuwa wakichochea wake na watoto wa watu wengine wakae vituoni kulinda kura huku wake zao na watoto wao wakiwa wameufya ndani wakila raha na kuachia watoto wa maskini ndio wakeshe kwenye mbu wakiumwa na mbu na kuvurumishwa na polisi.Wanataka kuwatumia wake na watoto wa watu wengine waumie ili watoto wao waishi maisha ya raha mustarehe baadaye.

Kijana kataa kuttumika kwa ajili ya wake na watoto wa Lowasa,Mbowe,Mnyika,Tundu LISSU,Sumaye,Kingunge.Godbless Lema,Mchungaji msigwa n.k wahamasishao vurugu wakati familia zao wamezificha.
 
Kwa nini ccm hampendi kulinda kura zenu?mimi nilidhani ulinzi wa kura ni muhimu kwa vyama vyote.Mbona ulinzi shirikishi huwa mnahimiza kwenye kura inakuaje hamtaki?
 
Kauli ya mwenyekiti wa CHADEMA mheshimiwa Mbowe ya kuwataka wapiga kura kupiga kura na kulinda kura zao ni ya uchochezi kwa kuwa serikali imeshatoa maelekezo na sheria ya uchaguzi iko wazi.

Lakini pia sheria nyingine kuhusu ulinzi na usalama zinakataza watu kukusanyika bila kubali kuwa ni kosa la jinai hivyo binafsi simuelewi Mbowe dhamira yake hasa katika hili ni nini.

Kweli huyu ni kiongozi wa kuaminiwa anayetaka kuchochea vurugu kwa kuwa vyama vyenye wagombea ni vingi.Je, iweje kila chama kiwaamuru wafuasi wake kukusanyika mita200 kulinda kura zao.Je, hali itakuwaje?

Busara itumike katika hili tupige kura turudi majumbani tuachane na ushabiki.

tuambieni tu mnahofia ulaji wenu huo uchochezi ni upi kusema walinde kura! ina maana kweli mna nia ya kuiba msingesema ni uchochezi kulinda kura kunachochea kitu gani na kwanini mbowe alisema hivyo?
 
Kauli ya mwenyekiti wa CHADEMA mheshimiwa Mbowe ya kuwataka wapiga kura kupiga kura na kulinda kura zao ni ya uchochezi kwa kuwa serikali imeshatoa maelekezo na sheria ya uchaguzi iko wazi.

Lakini pia sheria nyingine kuhusu ulinzi na usalama zinakataza watu kukusanyika bila kubali kuwa ni kosa la jinai hivyo binafsi simuelewi Mbowe dhamira yake hasa katika hili ni nini.

Kweli huyu ni kiongozi wa kuaminiwa anayetaka kuchochea vurugu kwa kuwa vyama vyenye wagombea ni vingi.Je, iweje kila chama kiwaamuru wafuasi wake kukusanyika mita200 kulinda kura zao.Je, hali itakuwaje?

Busara itumike katika hili tupige kura turudi majumbani tuachane na ushabiki.

kwa taarifa yako mbowe hajawawmbia wana chama amewaambia watanzania wapenda haki wasubiri matokeo na kuzuia yale magari ya Ghalib yasije na kura zao kwa hiyo kama wewe una maslahi yoyote ktk mpango wa wizi huo nenda kwako kalale hujalazimishwa tuache wanaumme tupambane kiitafuta haki
 
Back
Top Bottom