Duh hizi mita mia mbili zitaleta mkong'oto. Bado hoja ya kubaki vituoni ili kulinda kura nguvu yake kisharia ni ndogo. Utalindaje kura wakati kunakohesabiwa humo? Nimejaribu kusoma tafsiri binafsi humu jamvini kuhusu kinachokatazwa ni mikutano na nembo, je hakunatfsiri nyingine inayozuia mikusanyiko? Maana, kwa mtazamo wetu, twaweza kushikilia hilo lakini ikatolewa amri ya kuzuia mikusanyiko ambayao hushika kuwe na uchaguzi au la. Ulinzi wa kura wa uhakika ni kuwa na mawakala thabiti ambao hawatakubali kupepesa macho pembeni au kurubuniwa kwa kitu kidogo. CCM hilo wanaliweza karibu nchi nzima lakini upinzani bado. Tufuate kule ambapo upinzani wanashinda wanalindaje kura wakati wa kuhesabu, wanahakikishaje wasimamizi wao hawarubuniwi. Tukishazitambua hizo mbinu zitekelezwe kwenye majimbo yote. Pia tukubali tahadhari iliyotolewa na tume kuwa hawatambui UKAWA bali chama kilichomweka mgombea, hivyo atakayesimamia kura za urais awe wa CHADEMA. Je hili limefanyiwa kazi au ndio litalalamikiwa uonevu maana zaidi ya wiki mbili kauli hii imetolewa na Lubuva as a legal interpretation of the law. Tufanyie kazi haya mapungufu NCCR waliweza 1995 kwa nini leo isiwe. Ushindi ni zaidi ya kupiga kura ni organisation of the system as well to ensure the law is followed by closing loop holes. Mawakala ndio ufunguo wa ulinzi wa kura na si 200m.