Kauli ya JK "ukitaka kula lazima na wewe ukubali kuliwa" ina maana gani?

MZALAMO

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
1,758
1,967
Wana JF Kauli aliyoitoa JK ukitaka kula lazima na wewe ukubali kuliwa ina maana gani?
 
Wana JF Kauli aliyoitoa JK ukitaka kula lazima na wewe ukubali kuliwa ina maana gani?
Jamani mnapoleta hoja na mijadala jaribuni kuwa specific. Hivi umeshindwa nini kusema alikotolea hii kauli? be analytical plz
 
kwa hiyo yeye kwa sababu alitula( alitukula) 2005 na sisi sasa ni zamu yet
 
huelewi maana yake ni kuwa vaa kofia, vaa vitenge, kula Nyama, vaa mashati na wewe utaliwa tuu wakiingia madarakani.
WATAHITAJI KUZILUDISHA GHALAMA ZOOTE WALIZOTUMIA HAPO NDO TUTALIA KWA KUPNDA VYA KUPEWA.
 
Pia inaweza kutafsiriwa kuwa anaunga mkono dhana ya kutoa kitu kidogo. Ukitaka huduma ya kukusaidia na wewe toa kwanza kitu kidogo.
Kwa mantiki hii ufisadi unakuzwa na kiongozi wetu.
 
Halafu hata mkila nyasi , ndege kimeo ya Raisi lazima inunuliwe.
 
Wadau naomba tujadili hii kauli ya mheshimiwa maana kila ninapoikumbuka huwa sielewi alichota kumaanisha.Naelewa unapotaka kula ila KULIWA ndo kunakonitatiza.Kwa wadau mnaokumbuka alisema lini na wapi mnaweza pia kunisaidia.
Kama mtakumbuka akiwa kwenye mkutano wa kampeni huko mbeya alipokua anawajibu wanaoponda safari zake za nje alisema "Huko nje naenda kuhemea vibaba,kusingekua na hizo safari,watanzani wangekufa njaa"Sasa swali linakuja,Kama huko nje alienda akitaka watanzania Wale,je sisi TUMELIWA NINI?
Nawasilisha.
 
Rais alikuwa anahutubia bunge dodoma mwaka jana ndio alisema kula na kuliwa. Hotuba hiyo baadaye ilitakiwa ijadiliwe na wabunge lakini hadi leo, mpaka bunge limekwisha, hotuba hiyo haijajadiliwa. Eti ilipelekwa ikulu kuchakachuliwa kwanza.

Macinkus
 
Ina maana amekula miaka mitano ataliwa tarehe 31.
 
anatupa uzoefu wake, pengine alishaliwa sana,, sasa anatushawishi kutula kwa madai kuwa itafika kipindi na sisi tutakula. Kama yeye alikubali kuliwa shauri yake, Siko tayari kuliwa!!
 
Si alitoa kauli ii wakati anaongea na Taifa stars wakati wa mbrazil masikio maksimo! Taifa walikuwa wametiwa goli ndo mana kawaambia"ukitaka kula lazima uliwe,unataka kula bila kuliwa,haiwezekanii!" waswaili wakaongeza "ilo nalo neno" jaman uyu jamaa anaharibu kiswahili ile mbaya!
 
"mswhili" per-se ............................... he has never been serious - yaani anapenda jokes kama nini??? hata uongozi wake - waku-joke joke tu
Watanzania wana hali mbaya ...................yeye aaaaaaaaaaaaa .......................anaona utani tu.................ndio maana kauli zake za utani - utani- mafumbo - mafumbo.................................rais gani anahusudu taarab na waimba taarab anawapa uongozi?????????????????? he puts me off - and not only ME but majority of Tanzanians
 
Pia inaweza kutafsiriwa kuwa anaunga mkono dhana ya kutoa kitu kidogo. Ukitaka huduma ya kukusaidia na wewe toa kwanza kitu kidogo.
Kwa mantiki hii ufisadi unakuzwa na kiongozi wetu.

Kasema hana maana ya ile nyingine, Basi Maana yake ndo ile mkono mtupu haulambwi. Ndio maana anawapigia kampeni wazee wakitu kidogo.Chenge na mramba.
 
Mnataka kutuletea rais dhaifu na muhuni.................asiyejali watoto wetu!................
Hivi wanaoipenda ccm na kikwete ni watanzania?
 
anatupa uzoefu wake, pengine alishaliwa sana,, sasa anatushawishi kutula kwa madai kuwa itafika kipindi na sisi tutakula. Kama yeye alikubali kuliwa shauri yake, Siko tayari kuliwa!!

Ohoooo!!!!! Yale yale ya ZE UTAMU. Mie simo
 
Labda kwa wahisani....watupe misaada lakini wanapita mlango wa nyuma kupata madini na miradi mikubwa wanayotunyonya kurudisha gharama zao....nadhani kuna kitu hapo pia!!
 
Back
Top Bottom