Kauli ya First Lady wa Dk. Slaa, Josephine

Kauli ya First Lady wa Dk. Slaa, Josephine

"[FONT=ArialMT, sans-serif]Hatutaki hata kuzungumzia ‘status' ya ukimwi kwa baadhi ya wagombea, ana wake wangapi, ana vimada wangapi...nani anakwenda nje kubadilisha damu kila miezi sita, hatutazungumzia siasa za chumbani kama wanavyotaka tufanye, kwa sababu hayatatatua matatizo tuliyonayo," alisema.[/FONT]

haya ni maneno mabaya sana kuyazungumza,kwanza status ya afya ya mtu ni confidential,na ni breach kubwa ya medical ethics kuzungumzia afya ya mtu bila idhini yake wala ya wanafamilia wake, unaweza kushtakiwa na kutiwa hatiani wewe na huyo mtaalamu wa afya aliekupa taarifa nawe kuzitoa nje,so tuzungumze kwa lugha isiyo na jazba wala kukiuka mipaka.

pili kuwa na virusi vya ukimwi au ukimwi si tatizo tena katika ulimwengu tulionao leo, ni wale wajinga wa medical profession ndo wanaoweza kuzungumza kuwa ukimwi unaua. kwa maendeleo ya sayansi ya tiba yaliyofikiwa hivi sasa,ukimwi si tatizo tena la kutisha rather imekuwa ni chronic disease just like hypertension,diabetes mellitus, cancer etc. kusema "fulani ana virusi huyo" hiyo ni unyanyapaa mkubwa. so mtu mwenye virusi vya ukimwi au mwenye ukimwi ana haki sawa na fursa sawa katika kushiriki shughuli zote ziwe za kijamii,kisiasa,michezo na mengineyo kwani ukimwi upo manageable na wapo wengi tu wenye ukimwi au virusi vya ukimwi lakini wanaafya na siha njema pengine kuliko wewe au mimi tuliopo kwenye kompyuta. kuna mengi sana unaweza kuongea mtu lakini haina faida bali namaliza na ujumbe wangu hapa chini

binafsi naamini hatumchagui mtu kwa mambo yake binafsi sisi tutamchagua mtu ikiwa tu anaonyesha dhamira ya kweli ya kuwasaidia watanzania wote bila ubaguzi wa aina yoyote,tutamchagua mtu kwa busara yake na uwezo wake wa kutunganisha watanzania wote kama ndugu na pia kusimamia rasilimali za taifa zitumike ipasavyo na keki ya taifa igawiwe ipasavyo

Hivi Slaa alipoingiliwa mambo yake binafsi ulipinga kiasi gani?Halafu nani katajwa,hakuna jina lililotajwa kwa hiyo hakuna mtuhumiwa.
 
Ushauri kwa Dr Slaa; ili kuongeza attention ya hili swala;

Dr na Mama Josephine; waende publically kupima, wayaonyeshe majibu yao kwa waandishi wa habari na kuwaomba wagombea wote kufanya hivyo; kama njia ya kuhakikisha tuna kiongozi salama; najua CCM watapinga lakini hatutaki kiongozi ambaye maisha yake hayaeleweki; so najua hili l inaweza kufanyiwa kazi; na hii naamini itageuza kashfa ile ya kutunga imgeukie mkubwa wetu yuleeeeeeeeee; lazima chali chakachua ya maneno mwakaa huu haina nafasi

Kuna uchunguzi umefanywa na JK anao inasemekana; Slaa kijijini anatambulika sana kuliko mgombea yeyote;
Malunde-Malundi nakuunga mkono kwa 100%,

Dr. Slaa kama utanisoma nisikilize maana sisi ndio wapigakura wako tulio nje ya ulingo tunaona mwelekeo ukoje. Wewe binafsi hata kama ulishapima nenda tena kapime iwe public ikiwezekana uongozane na Josephine. Ila usizungumze chochote kuhusu afya ya mpinzani wako ile wewe kupima na kuonyesha hadharani itakuwa bonge la habari na message itakuwa imefika kwa walengwa yaani wapigakura na mhusika mwenyewe.
 
Ebu tujikite na sera za vyama vyetu na namna ya kumkomboa mtanzania katika dimbwi la umasikini
 
Hivi Slaa alipoingiliwa mambo yake binafsi ulipinga kiasi gani?Halafu nani katajwa,hakuna jina lililotajwa kwa hiyo hakuna mtuhumiwa.
Hakuna jina lililotajwa na Lissu ila siku ile Makamba anaongea kuhusu upadri na ndoa alimtaja Slaa. Kama kuna mgombea atajihisi kulengwa aseme tujue au wapambe wake watuambie mgombea wao ananyanyaswa.
 
Duh hatari kubwa ina maana mkuuluu ana kale kaugonjwa nyumbani.Hapana hapana mkuu alipima ngoma Mnazi mmoja akakutwa mzima wa afya labda kama ana ugonjwa mwingine.
 
Ushauri kwa Dr Slaa; ili kuongeza attention ya hili swala;

Dr na Mama Josephine; waende publically kupima, wayaonyeshe majibu yao kwa waandishi wa habari na kuwaomba wagombea wote kufanya hivyo; kama njia ya kuhakikisha tuna kiongozi salama; najua CCM watapinga lakini hatutaki kiongozi ambaye maisha yake hayaeleweki; so najua hili l inaweza kufanyiwa kazi; na hii naamini itageuza kashfa ile ya kutunga imgeukie mkubwa wetu yuleeeeeeeeee; lazima chali chakachua ya maneno mwakaa huu haina nafasi

Kuna uchunguzi umefanywa na JK anao inasemekana; Slaa kijijini anatambulika sana kuliko mgombea yeyote;

hizo taratibu hazipo Tanzania hii, labda waje wapitishe miaka ijayo. lakini suala si kuumwa - katiba inasema ithibitishwe na jopo la madaktari kuwa mtu huyo hana uwezo wa kufanya kazi. kuna watu wengi wanaumwa (maradhi mbalimbali) lakini wameshikiria nyadhifa private na serikalini
 
Binti Zion
Ndio maana siasa za maisha binafsi zinatakiwa kukemewa kwa nguvu zote maana zina madhara sana. Na madhara yanakwenda si kwa wanaorushiana maneno bali kwa watu wao wa karibu hasa familia. Hili suala la "umechukua mke wa mtu" basi na "wewe una VVU" ni mambo binafsi, ila kwa kuwa mambo ni mwaga ugali, nami nimwage mboga siasa zinasonga ndo tumefika hapa

Sio hao tu, madhara yanakuja pia kwa wengi kama unavyoona inaonekana sasa ni unyanyapaaji!!
 
..kupiga kampeni kwamba fulani ana ukimwi ni makosa.

..kampeni nzuri ni ile inayosema mgombea fulani anasambaza ukimwi.
 
(According to Nipashe Newspapers)

[FONT=ArialMT, sans-serif]Lissu alisema, kuna mambo binafsi kadhaa ya baadhi ya wagombea urais, ikiwemo matatizo ya afya yanayojulikana chanzo chake, lakini Chadema haiwezi kuyazungumzia jukwaani ama kuyatumia kama njia ya kupata kura.[/FONT]

“[FONT=ArialMT, sans-serif]Hatutaki hata kuzungumzia ‘status’ ya ukimwi kwa baadhi ya wagombea, ana wake wangapi, ana vimada wangapi...nani anakwenda nje kubadilisha damu kila miezi sita, hatutazungumzia siasa za chumbani kama wanavyotaka tufanye, kwa sababu hayatatatua matatizo tuliyonayo,” alisema.[/FONT]

My take, kama kweli anayoyasema Tundu Lissu (kubadilisha damu kila miezi sita) ni ya kweli (it is serious issue) na vielelezo vipo kwanini wananchi wasielezwe wazi afya ya kiongozi wanayetaka kumchagua? Huo ndio ujumbe wangu kwanini tufiche ugonjwa.

Ukishasema "hatutaki kuongelea status ya ukimwi ya wagombea" tayari ushaongelea status hiyo.

Ukishasema "no comment" ushatoa comment. Kama unataka kutoongelea issue usiiongelee tu, usijifanye hutaki kuongelea huku unaongelea.
 
.

Huwezi kujua Tundu Lisu mwenyewe anaweza kuwa ana ukimwi ni siri yake na daktari. Alipokuwa anasomea degree yake ya sheria pale chuo kikuu cha Dar es salaam (bila shaka 1992 hadi 1995) inadaiwa alitembea na dada mwenye ukimwi. Huyo dada alikuwa anaitwa Maria na alishakufa. Hebu tuache haya mambo hakuna atakayesalikimka.
 
Kiranga,
You are so right. Mwaka 1984 Reagan akishindana na Walter Mondale alimmaliza kwa kusema " I will not talk about his youth and inexperience." Things went downhill from thereon for Mondale.
 
.

Huwezi kujua Tundu Lisu mwenyewe anaweza kuwa ana ukimwi ni siri yake na daktari. Alipokuwa anasomea degree yake ya sheria pale chuo kikuu cha Dar es salaam (bila shaka 1992 hadi 1995) inadaiwa alitembea na dada mwenye ukimwi. Huyo dada alikuwa anaitwa Maria na alishakufa. Hebu tuache haya mambo hakuna atakayesalikimka.
Fofofo,
Tindu Lissu is not running for President.
 
Sasa huo utakuwa ni unyanyapaa kwa waathirika.kwani mgonjwa wa ukimwi haruhusiwi kuwa kiongozi? si anaishi kwa matumaini?Acheni hizo bwana.
.

Haya ni matusi kwa wagonjwa wa ukimwi kwani wao sio watu. Siri ya ukimwi ni kwamba ukiwa katika hatua ya mwanzo (window period) hakuna kati yetu anayeweza kujua hapa JF wagonjwa ni wangapi. Tabia hii ya kunyanyapaa wagonjwa wa ukimwi imechochea sana maambukizi hapa nchini kwa sababu wagonjwa wengi wanaogopa kujitokeza hadharani na hivyo kuendelea kuambukiza wengine kwa hofu ya unyanyapaa.
 
Mi naona mama kikwete naye amtetee mumewe na CCM sijui angesemaje?...

I really wonder

Mama Salma Kikwete alishawahi kumtetea mumewe mwaka 2005 alipoandamwa kwa tuhuma za kuwa na vimada wengi na watoto kadhaa nje ya ndoa, utetetezi wake ilikuwa " ni sawa tu sababu mume wake ni handsome hivo wanajipendekeza wenyewe"
 
ndio maana CHADEMA wanasema ni upuuzi kuzungumza siasa za namna hiyo kama CCM wanavyofanya

chadema nao wana siasa za maji taka. mfano ni wanachadema/mashabiki na wakereketwa wa chadema wa hapa JF. Hili jukwaa wanachadema mmeligeuza la chama chenu wakati ni la watanzania wote bila kujali anatoka chama gani kati ya vyama vya siasa 18 vilivyopata usajili wa kudumu hapa nchini.
 
Hebu tueleweshe vema...Katiba inasemaje kuhusu afya ya mgombea na suala zima la uathirika wa VVU kwa ujumla??tuwekee hicho kipengele cha katiba.

Katiba iko kimya kuhusu magonjwa na sio Tanzania tu na nchi zote duniani.
 
Zion, nakuunga mkono kwa asilimia 100,kwa sababu ukimwi siyo ugonjwa bali ni upungufu wa kinga mwilini ambapo mwathirika anaweza akaishi zaidi ya miaka 20 huku akiendelea kufanya shughuri zake kama kawaida iwapo atazingatia masharti ya matumizi ya dawa za kuongeza kinga mwilini. Je? tumewaona watanzania wangapi wanafanya kazi na wanatumia dawa kila siku kulingana na magojwa waliyonayo huku utendaji wao ukiwa mzuri na wa kuigwa.
Unajifariji sio au unamfariji?
Afya ya kiongozi wa nchi ni concern ya kila mwananchi, yeye ndie anayetoa maamuzi ambayo si tu yanaathiri mstakabari wa nchi lakini pia maamuzi yake yanamgusa kila mwananchi. Kama rais ni mgonjwa na ugonjwa huo unaathri utendaji hafai kuendelea kuongoza nchi! Maathalani suala la kuanguka mbele ya halaiki si mara moja ni zaidi ya mara tano sasa. Mtu anapohoji hilo kwangu mimi huo sio unyanyapaa ni haki ya kikatiba. Wananchi tunapaswa kujua nini kinamsibu Rais wetu?
 
Tatizo Chadema wamejeruhiwa pabaya na mambo yeshakuwa makubwa ,hapa ipite huruma tu mahakama iamuriwe kutupiliaa mbali shitaka hilo ,yaani ccm wapite nyuma ya pazia na bila ya shaka itakuwa ni blackmail

kwenye siasa mbinu zote halali zinaweza kutumika kupata ushindi, sio makosa kwa CCM kutuhabalisha kwamba Dk. Slaa amekiuka sheria ya ndoa ya mwaka 1970 kwa kuwa wananchi tuna haki ya kujua wasifu wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi nchini.Kama huu ni uongo basi mahakama itatupa jibu.
 
Back
Top Bottom