fofofo said:Haya ni matusi kwa wagonjwa wa ukimwi kwani wao sio watu. Siri ya ukimwi ni kwamba ukiwa katika hatua ya mwanzo (window period) hakuna kati yetu anayeweza kujua hapa JF wagonjwa ni wangapi. Tabia hii ya kunyanyapaa wagonjwa wa ukimwi imechochea sana maambukizi hapa nchini kwa sababu wagonjwa wengi wanaogopa kujitokeza hadharani na hivyo kuendelea kuambukiza wengine kwa hofu ya unyanyapaa.
fofofo,
..kukiwa na mgombea mwenye HIV status halafu anaficha ukweli huo, na zaidi anausambaza, basi kuweka wazi status yake siyo unyanyapaa.
..pia kama kuna mgombea ana status hiyo ni bora aiweke wazi ili wananchi waweze kuelewa vema ile kauli mbiu kwamba kuwa na ukimwi siyo mwisho wa maisha ya mhusika.
..kwa mfano: Raisi alipima ukimwi na kuweka status yake hadharani. kila mahali alipotembelea alipongezwa kwa suala hilo. sasa akijitokeza mgombea Uraisi akasema yeye ana ukimwi na anagombea Uraisi nadhani wananchi wanaweza kuchukulia kuwa hicho ni kitendo cha kishujaa.